Matukio mawili yaliyoniacha na tafakuri kubwa

Kweli jpm alikua raisi wa wanyonge, sasa hivi tunaona maraisi wakipeana mema ya nchi huku maskin hata mia ya kula hawana, magufuli upumzike kwa amani, ulikua dictator ila uliwakumbuka maskini
Mother Theresa yeye anagawa takrima za nchi kwa wastaafu km njugu, jamani mie naumia mno [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Naomba nisipingane na asili ambayo inalandana hata mitazamo ya kiimani kwamba ALIYE NACHO HUONGEZEWA! Kuna uwezekano mkubwa mabepari walijifunzia huku.

Matukio haya mawili ni ya ma rais wetu wastaafu ambao kupitia kwao weekend iliyopita walisababisha mijadala mipana mitandaoni

1.TUKIO LA KWANZA
Aliyekuwa rais wa pili wa Tanzania baada ya uhuru wa Tanganyika mzee Ali Hassan Mwinyi alizindua kitabu cha maisha yake..! Hili si tukio la dharura ni tukio lililoandaliwa kwa muda mrefu na kwa kuzingatia protokali mgeni rasmi si mwingine bali ni rais aliyeko madarakani

Mipango ya Mungu si ya mwanadamu hivyo inawezekana kabisa aliyekuwa kaandaliwa kuwa mgeni rasmi kwenye tukio hili kubwa ni aliyekuwa rais wa awamu ya tano hayati Pombe John Magufuli na inawezekana kabisa na zawadi ya mgeni rasmi kwenda kwa mhusika ilikuwa imeshaandaliwa!

Kudra za Mwenyezi Mungu zikamuangukia aliyekuwa makamu wa rais kuwa rais kamili wa Tanzania baada ya kifo cha maradhi cha mtangulizi wake..Na huyu ndio kawa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa kitabu cha mzee Mwinyi

Kilicholeta mjadala ni ukarimu wa zawadi aliyotunukiwa na rais Samia Hassan Suluhu..zawadi ya gari la kifahari la bei ghali aina ya Mercedes Benz linalofikia kiasi cha Tsh milion 250 kabla ya usafiri na usajili na kodi

Lawama zimeenda kwa mama kwa matumizi mabaya ya pesa za wananchi.. Lakini pengine si kosa lake inawezekana kabisa ni kitu kilichokuwa kimeshapangwa kitambo

Wengine wamesema sababu iliyotolewa haikidhi ama angetafutiwa walau gari la bei ndogo zaidi... Ama la angepewa zawadi nyingine... Waswahel wanasema usimuingilie aliyepewa kapewa! Mzee mwinyi hana shida ya chochote ana kila kitu cha kimaisha katika level ya kibinadamu... Zawadi aliyopewa ni bakshish tu... Aliye nacho huongezewa! Tafakuri yangu kwenye hili tukio ni kile kitendo cha mzee Mwinyi kugoma kupokea zawadi ile! (Tetesi)!!! Pengine kaona ni kufuru sasa tena ukizingatia huu ni mwezi wa toba kwa imani yake!

2.TUKIO LA PILI
Mzee Jakaya Kikwete rais mstaafu wa awamu ya nne kukabidhiwa nyumba aliyojengewa na serikali...Hii ni kwa marais wote wastaafu wamefanyiwa hivyo...! Kwa picha tu za nje si nyumba ya kitoto bali ni jumba kubwa la kifahari

Hili nalo si tukio la dharura ni tukio lililokuwa limepangwa kitambo na kwa muktadha uleule mgeni rasmi angekuwa JPM kama angekuwa hai!

Tafakuri yangu kwenye hili..! Hivi ni kweli kabisa JK anashida na nyumba? Tena lijumba kubwa kama lile? Lakini tukirejea kwenye ile kanuni ya asili ya aliyenacho huongezewa basi kauli inakata na mjadala unaisha

JK pia ana kitabu cha maisha yake.. Sina kumbukumbu kama alishakizindua na katika hafla ile alipewa zawadi gani na mgeni rasmi!

Mzee Mwinyi kwa tetesi ni kwamba kaikataa zawadi nzuri ya gari la kifahari .. Sina hakika kama atakapokabidhiwa jumba lake la kifahari nalo atalikataa... Nasema sina hakika.

Viongozi wakuu wa nchi ni viongozi ambao hulelewa na serikali zao mpaka kifo... Na kwa viongozi wetu wa Afrika huingia madarakani wakiwa watupu na kutoka wakiwa na ukwasi wa kutisha wao na ndugu zao na familia zao...Lakini bado katika kulelewa huko na ukwasi huo bado huongezewa bakshish ya hiki na kile

Yaani ni kama vile wananyang'anya kile kidogo ambacho kingewasaidia wanyonge fukara na maskini wa Taifa hili...!!! Na hawajali ama macho yao yamejaa upofu kuyaona haya... Ni kilevi cha madaraka na kupata hupofusha mpaka weledi wetu..!!!
Hi nchi isiyo na katiba hai inahuzunisha
 
Gari sio lolote kulinganisha na mchango wa Mzee Mwinyi aliyekuwa ameachiwa nchi na Hayati Nyerere ikiwa hoi kiuchumi.

Wenzangu na mimi tuliokuwa tunaelewa nini kinaendelea duniani miaka ile ya 1980 mwanzoni tutakumbuka kula ugali wa Yanga na yale maduka ya kaya, kila nyumba inakuwa na daftari la bidhaa za kununuliwa hapo dukani. Mwinyi alifanya mengi mpaka hali ikaanza kuwa njema.

Zawadi ya Nyumba ya Mzee Kikwete sio lolote kulinganisha na miradi aliyoianzisha na yenye kuendelea kuleta mabadiliko ya kijamii.

Hiyo nyumba haina thamani kulinganisha na wagonjwa wa moyo wanaotibiwa na kupona pale MOI.

Hiyo nyumba haina thamani kulinganisha na wasafiri wote wanaotumia mwendo kasi asubuhi mchana na jioni.

Hiyo nyumba haina thamani kulinganisha na namna umeme wa REA unavyoibadilisha kabisa Tanzania kiuchumi.

Umaskini wa kichwani ni mbaya sana, kwani siku zote mtu analalamika mpaka anasahau kuwa kwa kufanya hivyo anamkufuru Mungu aliyemjalia vipaji vingi.
Mwendokasi REA ni pesa ya walipa kodi si pesa ya wastaafu
Kila mtumishi wa umma akistaafu apewe zawadi kwani nao walichangia kuinua uchumi halafu tuone.......

Ni kufuru ndio
Ilikuwa ni kazi sio huduma
Walilipwa mshahara na marupurupu na bado wanalipwa na kutunzwa
Hizi ni bhakshishi ni bahasha za kaki
Si sahihi si sawa si uungwana si haki kwa mlipa kodi
 
Katiba tunayo ila ndio hii hapa...hawaishi kuinajisi..[emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
IMG-20210510-WA0106.jpg
 
hizo habari kwamba amegoma sijui umezitoa wapi!!!

kama amegoma basi itakuwa kwa minajiri kwamba hakudhani litamfaa kwa sababu zilizomfanya akapewa.lakini haiwezikuwa ni kwa minajiri ya mwezi wa toba kama ambavyo unafikiri.

nyumba nzuri aliishaichukua.tena yenye thamani kubwa maradufu ya gari hilo,bado kila baada ya miaka 5 gari hizo hubadirishwa,angezikataa hata zilizopita.
 
Mwendokasi REA ni pesa ya walipa kodi si pesa ya wastaafu
Kila mtumishi wa umma akistaafu apewe zawadi kwani nao walichangia kuinua uchumi halafu tuone.......

Ni kufuru ndio
Ilikuwa ni kazi sio huduma
Walilipwa mshahara na marupurupu na bado wanalipwa na kutunzwa
Hizi ni bhakshishi ni bahasha za kaki
Si sahihi si sawa si uungwana si haki kwa mlipa kodi
Wajibu wa mtumishi wa umma unageuzwa kuwa hisani kwa mwananchi mkamuliwa kodi[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
hizo habari kwamba amegoma sijui umezitoa wapi!!!

kama amegoma basi itakuwa kwa minajiri kwamba hakudhani litamfaa kwa sababu zilizomfanya akapewa.lakini haiwezikuwa ni kwa minajiri ya mwezi wa toba kama ambavyo unafikiri.

nyumba nzuri aliishaichukua.tena yenye thamani kubwa maradufu ya gari hilo,bado kila baada ya miaka 5 gari hizo hubadirishwa,angezikataa hata zilizopita.
Zingatia kusoma kwa makini[emoji1541][emoji1541][emoji1541]
Tafakuri yangu kwenye hili tukio ni kile kitendo cha mzee Mwinyi kugoma kupokea zawadi ile! (Tetesi)!!!
 
ndicho nimejikita nacho hicho.
 
Mi naona sawa btu. Mbona Magufuli alikuwa anagawa mabulungutu ya fedha kwenye ziara zake zote. Kwenye miaka 6 amegawa sh ngapi? Na mbona watu hawakuuliza. Pili Magufuli "amezipoteza" trillion 1.5 mpaka leo hazijulikani zilipo. Mbona hakuna anayehoji? Mwacheni mama nae afanye anavyoona inafaa.
 
Kweli jpm alikua raisi wa wanyonge, sasa hivi tunaona maraisi wakipeana mema ya nchi huku maskin hata mia ya kula hawana, magufuli upumzike kwa amani, ulikua dictator ila uliwakumbuka maskini
Hiyo nyumba nani aliwajengea hao marais waastafu!

Ova
 
Gari sio lolote kulinganisha na mchango wa Mzee Mwinyi aliyekuwa ameachiwa nchi na Hayati Nyerere ikiwa hoi kiuchumi.

Wenzangu na mimi tuliokuwa tunaelewa nini kinaendelea duniani miaka ile ya 1980 mwanzoni tutakumbuka kula ugali wa Yanga na yale maduka ya kaya, kila nyumba inakuwa na daftari la bidhaa za kununuliwa hapo dukani. Mwinyi alifanya mengi mpaka hali ikaanza kuwa njema.

Zawadi ya Nyumba ya Mzee Kikwete sio lolote kulinganisha na miradi aliyoianzisha na yenye kuendelea kuleta mabadiliko ya kijamii.

Hiyo nyumba haina thamani kulinganisha na wagonjwa wa moyo wanaotibiwa na kupona pale MOI.

Hiyo nyumba haina thamani kulinganisha na wasafiri wote wanaotumia mwendo kasi asubuhi mchana na jioni.

Hiyo nyumba haina thamani kulinganisha na namna umeme wa REA unavyoibadilisha kabisa Tanzania kiuchumi.

Umaskini wa kichwani ni mbaya sana, kwani siku zote mtu analalamika mpaka anasahau kuwa kwa kufanya hivyo anamkufuru Mungu aliyemjalia vipaji vingi.
mbona nyerere hakua navyo hivyo licha ya kutupatia uhuru sio ukisaidia nchi ndo uchukue vyote watakavyo kupa masikini wakafie mbali na umasikini wao kisa umewasaidia kuendesha nchi sio haki wakati hao maraisi wanawategemea wana nchi
 
Mkuu mtoa mada hakuwa na maana hiyo unayofikiria wewe. Yeye kaeleza wazi kuwa Wastaafu wale wanalelewa na Serikali kwa maisha yao yote yaliyosalia Duniani pamoja na wenzi wao. Nyumba na magari wanayoyatumia hivi sasa yanahudumiwa na Serikali kwa 100%.

Tukiachilia mbali magari watakapohamia kwenye makazi yao mapya bado huko yataendelea kuhudumiwa. Hata zile nyumba za awali zitaendelea kuhudumiwa na Serikali. Kwako wewe huoni ni mzigo usio wa lazima kwa nchi kama hii yenye hospt zisizokuwa na madawa? Na shule zisizokuwa na madawati??

Kwa tafsiri yangu mimi hii ni namna ya Kiongozi aliyeko Madarakani kuwaziba midomo Watangulizi wake ili wasimkosoe pale anapoboronga. Nasema hivyo kwasababu nyumba hizi hazina uwiano kwenye dhamani bali hutegemea utashi wa Rais aliyeko Madarakani. "Katiba Mpya ni Muhimu".

Tena hununuliwa magari mapya kila baada ya miaka minne.
 
mbona nyerere hakua navyo hivyo licha ya kutupatia uhuru sio ukisaidia nchi ndo uchukue vyote watakavyo kupa masikini wakafie mbali na umasikini wao kisa umewasaidia kuendesha nchi sio haki wakati hao maraisi wanawategemea wana nchi
Nongwa zile zile zisizo na sababu za msingi.
 
Mi naona sawa btu. Mbona Magufuli alikuwa anagawa mabulungutu ya fedha kwenye ziara zake zote. Kwenye miaka 6 amegawa sh ngapi? Na mbona watu hawakuuliza. Pili Magufuli "amezipoteza" trillion 1.5 mpaka leo hazijulikani zilipo. Mbona hakuna anayehoji? Mwacheni mama nae afanye anavyoona inafaa.
Haya si ya mama... Tusimtwishe mzigo usio wake...KAYAKUTA ... Kumlaumu yeye ni kukosea sana
 
Gari sio lolote kulinganisha na mchango wa Mzee Mwinyi aliyekuwa ameachiwa nchi na Hayati Nyerere ikiwa hoi kiuchumi.

Wenzangu na mimi tuliokuwa tunaelewa nini kinaendelea duniani miaka ile ya 1980 mwanzoni tutakumbuka kula ugali wa Yanga na yale maduka ya kaya, kila nyumba inakuwa na daftari la bidhaa za kununuliwa hapo dukani. Mwinyi alifanya mengi mpaka hali ikaanza kuwa njema.

Zawadi ya Nyumba ya Mzee Kikwete sio lolote kulinganisha na miradi aliyoianzisha na yenye kuendelea kuleta mabadiliko ya kijamii.

Hiyo nyumba haina thamani kulinganisha na wagonjwa wa moyo wanaotibiwa na kupona pale MOI.

Hiyo nyumba haina thamani kulinganisha na wasafiri wote wanaotumia mwendo kasi asubuhi mchana na jioni.

Hiyo nyumba haina thamani kulinganisha na namna umeme wa REA unavyoibadilisha kabisa Tanzania kiuchumi.

Umaskini wa kichwani ni mbaya sana, kwani siku zote mtu analalamika mpaka anasahau kuwa kwa kufanya hivyo anamkufuru Mungu aliyemjalia vipaji vingi.
Vema sana
 
Back
Top Bottom