Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Yaani kwa ujumla inauma mno kwa wapenda mabadiliko kwa namna majimbo kama hayo ya Ilala, Segerea, Kigamboni na lile jimbo la Nyamagana la jijini Mwanza, ambapo majimbo yote hayo yalikiuka makubaliano ya Ukawa ambapo waliweka wagombea wawili kwa kila jimbo wa vyama vya Chadema na CUF.
Kwa hesabu zilizotolewa na NEC kuhusu ushindi wa wagombea hao wa CCM, ambao wote wamepata ushindi wa kiduchu, ni dhahiri kwa sasa Ukawa wangekuwa na plus 4 ya idadi waliyo nayo ya idadi ya wabunge.
Yote hiyo inatokana na hao wagombea kuweka mbele ubinafsi badala ya kuweka mbele maslahi ya kutaka mabadilko nchini.
Vivyo hivyo hao wagombea waliogomea makubaliano hayo ni wasaliti wakubwa wa Umma wa watanzania waliojitokeza kwa wingi mno siku ya kupiga kura kwa ajili ya kutaka mabadiliko.
Hata hivyo kuna harufu ya mchezo mchafu ambao unadaiwa kuchezwa na CCM ya kuwashawishi na 'kuwajaza' manoti wagombea hao ili wakomae na waendelee kugombea ili wazigawe kura za upinzani na kuwafanya wagombea wa CCM washinde kiulaini.