Kwa masikitiko makubwa bado siamini kwa macho wala masikio yangu kile nachoendelea kukitazama na kukisikia NEC
#MILIONI 10 HELA YA MBOGA
Jamani Watanzania tumelogwa na nani??Hata yule aliewatukana na kuwakashifu?? nitamnukuu (''Sihitaji kura zenu na sina shida nazo hata msiponipa'') huku kwa mbwembwe na nyodo akisema mbele ya umma kwamba MILIONI 10 kwake ni kama hela ya MBOGA.Mmemrudisha Bungeni??kweli??Ili akapate hela ya UNGA sasa si ndio??Dah jambo hili limenisikitisha saana tena saanaa!!Sina cha kufanya pengine wananchi wa jimboni kwake mmeona ni sawa kumpa kura zenu tena!!
MWANZA,,MUSOMA,,GEITA
Binafsi nimesoma Mwanza kimafanikio katika taaluma (Nsumba Boys 2009_2011) na nilipiga kura kwa mara ya kwanza mwaka 2010 kwa EZEKIA WENYE nikiwa mwanafunzi wa kidato cha 6 katika shule tajwa hapo juu kwenye kituo cha NYAMARANGO!Nimeishi mwanza kwa muda mrefu japo nyumbani ni Arusha.Mkoa au jiji hili ni moja kati ya Nguzo nilizoziamini kwa asilimia nuingi katika kutafuta mabadiliko ya kweli,,hasa baada ya kushuhudia Hamasa katika mikutano mikubwa ya Ukawa pale viwanja vya Furahisha.Nini kimetokea mwanza??NYAMAGANA TUMEIPOTEZA,,Kana kwamba haitoshi ILEMELA pia TUMEIPOTEZA!!Madiwani wengi wa ccm wameshinda uongozi katika kata nyingi kuliko upinzani!!Nini sababu??Je mlibadili gia angani??Au kwa kua Mgombea wa Ccm ni wa nyumbani kwenu ndugu zangu??Au ndio Goli la Mkono limepata nafasi sana ukanda huo??Bado sipati jibu!!
#Musoma ndugu zangu Mlideki hadi barabara!!Mbona matokeo yanakua tofauti jamani??Je ni Goli la mkono?Kama ni hivyo je,mlishindwa kuziba mianya ya udanganyifu vituoni?Au mliogopa ile ya MITA200??
Nashindwa kuwalaumu moja kwa moja kwa sababu sijafanya utafiti kugundua nini kimetukwamisha!Sitaki kuingolea Mbeya kiundani kwa sababu kimatokeo imegeuka 100% kua ngome ya ccm!!
NINI KINAENDELEA ZANZIBAR??
Matokeo yalianza kutolewa jana lakini katika hali isio ya kawaida wanasema umeme ulikatika na waliahidi kurudi saa 2 usiku wa jana,jambo ambalo halikufanyika mpaka mida huu naandika uzi huu bado kimya,ol tuvute subira japo sioni mantiki ya ucheleweshwaji wa matokeo ile hali zanzibar ina wapiga kura wasiozidi Laki 5 ambayo ni idadi ndogo sana ukilinganisha na bara
Majuzi Maalim Seif Mgombea wa kiti cha urais Kwa chama ya CUF aliiitisha mkutano na vyombo vya habari na kujitangaza kama mshindi halali kwa kua alimzidi mpinzani wake kwa kura karibu 30,000!
Tukiqchana na hay,hapo usiku nilipokea waraka unaoeleza kua Maaskari na wanajeshi walivamia chumba kile cha mikutano ambapo matokeo yalikua yakitangazwa na ZEC na kulazimisha usitishwaji wa utoaji matokeo mpaka pale watakapoarifiwa!Sina uhakika na hili na wala sitaki kuonekana mchochezi katika hili!Lakini Mtanzania jiulize tu nini kinachelewesha mapaka Muda huu??Zec isitoe matokeo??ile hali zoezi la kuhesabu kura limekwisha malizika??Haihitaji shule wala chuo kujua jibu hapa!!
Mwisho tu nimalize kwa kuipongeza mikoa iliyodhihirisha kutaka mabadiliko kiukweli ikiwemo Arusha,Dar es salaam na Kilimanjaro (moshi),pamoja na ZANZIBAR!!Japo kuna malalamiko ya Uchakachuaji wa hali ya juu wacha tuendelee kusubiri na kuona Hatua gani zitachkuliwa,binafsi bado sioni DEMOKRASIA YA KWELI TANZANIA!!