Elections 2015 Matukio na Matokeo toka maeneo mbalimbali ya Tanzania - Uchaguzi Mkuu 2015

Elections 2015 Matukio na Matokeo toka maeneo mbalimbali ya Tanzania - Uchaguzi Mkuu 2015

MGOMBEA ubunge jimbo la Kilombero, mkoani Morogoro, Peter Lijualikali ambaye ana hukumu mbili anazozitumikia kwa sasa, kesho anatarajiwa kusikiliza hukumu ya tatu katika kesi inayomkabili kwenye Mahakama ya Wilaya Kilombero. Anaandika Charles William ? (Lijualikali anayegombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), anatumikia adhabu ya kifungo cha nje kwa miezi sita na nyingine aliyolipa faini ya Sh. 520,000.


Muhalifu , jamabazi sugu amekua mbunge hii si sawa kwa mustakabali wa nchi yetu

Kama fisadi anavyoenda kuwa Rais wa nchi,hii si sawa kwa mustakabali wa tanzania yetu.
 
Jamani uongozi wa jf mmekumbwa na tatizo gani hakuna updates ya matokeo katika nyuzi mlizoanzisha, tatizo nini?

Hii kama haina maana ten, matokeo ya saa moja asubuhi ninyi mpaka sasa hamja update
 
Viti vya ubunge.
CCM - 104
CDM - 28
CUF - 18
Urais
Magufuli - 59%
Lowassa - 39%
Wengine - 02%
Kuna swali zaidi?
 
Nilipata kuwaambieni ninyi CHADEMA kwamba huyo jamaa ni sumu kwa chama hata kama mnadhani mtapata faida kwake. CHADEMA imeramba sumu kali. Tumbo limeanza kukata. Kifo cha chama ki mbele yenu.
 
Vijana kama kina vicent nyerere na wenje nimewaonea huruma sana
 
Waliwaona CCM ni wajinga walipomkata. Matokeo halisi wameyaona toka kwa wananchi
 
Toa ushahidi wa Takwimu kuwa chama kimefanya vibaya kuliko hapo nyuma
 
Mh. Freeman Mbowe Chadema Jimbo la Hai Kilimanjaro ameshinda kwa kupata kura 51,124.

Mh. James Mbatia NCCR Jimbo la Vunjo Kilimanjaro ameshinda kwa kupata kura 60,187.

Hongera sana, natumai hii itakuwa combination nzuri sana bungeni.
 
Back
Top Bottom