Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Hebu leo twende huku na kule duniani tuangalie matukio yaliyotokea miaka ya nyuma, yanayoaminika kuwa yalisababishwa na uchawi au nguvu za giza. Baadaye ntakueleza njia za kuwashinda wachawi na mashetani kama umekuwa ukiwaogopa.
Uingereza:
Poltergeist ni tukio lililotokea Uingereza. Tukio hili lilihusisha familia moja iliyodai kuwa nyumba yao ilikuwa ikisumbuliwa na mizimu au nguvu zisizo za kawaida (poltergeist). Familia hiyo iliripoti kwamba ilisikia sauti zisizoeleweka na kuona meza, viti, makochi, makabati na vitanda vikihama hama vyenyewe na kurushwa rushwa hewani na nguvu zisizoonekana.
Marekani:
Kesi za kichawi za Salem(Salem Witch Trials) ni msururu wa kesi za uchawi zilizotokea katika mji wa Salem, Massachusetts. Kilikuwa kipindi cha hofu kubwa iliyosababishwa na wasichana kadhaa waliodai kuathiriwa na uchawi. Watu zaidi ya 200 walituhumiwa kuwa wachawi. Kati ya hao 19 walihukumiwa kifo kwa kunyongwa, na mmoja aliuawa kwa kukandamizwa na mawe. Mji wa Salem ni kivutio kikubwa cha watalii, hasa kwa wale wanaopenda kujua mambo ya kichawi. Mji huo una makumbusho mengi yanayohusiana na kesi hizo za uchawi.
Ufaransa:
Napoleon Bonaparte alikuwa kiongozi mashuhuri wa Ufaransa(Emperor of France). Alijulikana kwa ujuzi wake mkubwa wa kijeshi. Ilidaiwa Napoleon alilaaniwa au kulogwa na wachawi, kwani alikufa katika hali ya kutatanisha.
Misri:
Nchini Misri kulikuwa na imani kwamba yeyote atakayefungua au kuvuruga kaburi la Farao Tutankhamun atapatwa na laana na mikosi au kifo cha ghafla. “Archaeologist” Howard Carter na timu yake walifukua kaburi la Mfalme Tutankhamun. Baada ya ufukuzi huo, watu kadhaa waliohusika walifariki kwa njia zisizoeleweka. Habari za vifo hivyo zilisababisha watu waamini kuwa waliofukua kaburi hilo waliathiriwa na laana ya wachawi wa Misri.
Italia:
Tarantism ni ugonjwa wa ajabu uliotokea huko Italia, ambapo watu waliamini kuwa ugonjwa huo ulisababishwa na kung’atwa na buibui wa kichawi aina ya tarantula. Ugonjwa huo ulisababisha msongo wa akili na hali ya ajabu mwilini kama vile kupooza, huzuni kali, au mhemko wa ghafla. Waliamini kuwa tiba pekee ilikuwa kucheza muziki wa haraka(tarantella) kwa nguvu ili kutoa sumu hiyo nje ya mwili. Hadi leo muziki wa tarantella bado ni sehemu ya utamaduni wa Italia.
Ufaransa:
Nchini Ufaransa kulikuwa na msiba mkubwa uliojulikana kama Msiba wa Dansi wa Strasbourg. Katika tukio hilo, watu walishikwa na wazimu wa kucheza bila kusimama(non stop) kwa siku nyingi, na baadhi walifariki kwa uchovu au mshtuko wa moyo. Hakuna maelezo ya kisayansi yaliyoeleweka kuhusiana na tukio hilo kwa wakati huo, hivyo watu waliamini kuwa ni uchawi au laana.
Matukio yanayoaminika kuwa ni ya kichawi bado yanaendelea kushuhudiwa huku na kule duniani. Kuna watu wameshuhudia kwamba walipoamka asubuhi walijikuta wamelala kwenye kitanda nje ya nyumba. Kitanda kilitolewaje nje hawajui. Wengine wamekiri kunyolewa nywele usiku bila kuona mtu anayewanyoa. Kuna watu wameona moshi ukifuka katikati yao bila kuwepo chochote kinachoweza kusababisha moshi. Mara kwa mara tunasikia wachawi wamekamatwa alfajiri nje ya nyumba wakiwa na nyungo wanazodai zinawawezesha kuruka hewani usiku. Mara kadhaa tumeona vichaa wakiokota makopo kutokana na madai kuwa wamelogwa na wachawi.
Uchawi upo? Kwa wanaoamini Biblia, ni kweli uchawi upo. Katika kitabu cha Kutoka 7:10-12 imeandikwa hivi:
"Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, wakafanya kama vile Bwana alivyowaagiza; Haruni akatupa fimbo yake mbele ya Farao, na mbele ya watumishi wake, ikawa nyoka. Farao naye akawaita wenye hekima na wachawi; na hao waganga wa Misri, wakafanya vivyo hivyo kwa uchawi wao. Wakatoa kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao."
Kitabu cha Matendo 8:9-11 kinaeleza juu ya Simoni mchawi aliyekuwa akiwashangaza watu wengi kwa uchawi wake. Ukisoma pia Matendo ya Mitume 16:16-18 utaona habari za msichana(kijakazi) aliyekuwa anaagua au kutoa unabii kwa kutumia nguvu za giza(pepo wa utambuzi). Msichana huyo aliwaingizia pesa nyingi bwana zake hadi pale pepo walipomtoka.
Matendo ya kichawi yanafanyika kutokana na nguvu za giza za shetani na mapepo. Shetani na mapepo ni roho chafu. Kwa sababu hiyo huwezi kuwaona kwa macho wanapotenda mambo ya kichawi kwa kushirikiana na wachawi au washirikina.
Huna haja ya kumuogopa shetani wala wachawi. Mungu wetu nguvu zake ni kuu kuliko nguvu za giza. Hivyo, mtu akikutishia kukuloga, usibabaike. Ukiingia katika nyumba inayosemekana ina wachawi, usiogope kulala humo. Ukivamiwa usiku na wachawi, usihofu. Fanya haya yafuatayo utaona ushindi:
Mwamini Yesu Kristo na uishi maisha matakatifu. Shetani anawaogopa watu wanaoishi maisha matakatifu kwakuwa wamepewa amri ya kumkemea(Mt 10:1-25).
Sali(omba) bila kukoma. Maombi ni silaha kubwa ya kiroho dhidi ya wachawi. (Waefeso 6:18; 2 Wakorintho 10:4). Omba asubuhi, omba mchana, omba usiku kabla hujalala Mungu akufunike kwa ulinzi wake. Ukiona mashambulizi yanazidi, funga na kuomba upambane na nguvu za giza.
Tumia Damu ya Yesu kwa imani. Damu ya Yesu ina nguvu ya kutuokoa na kutulinda dhidi ya kila shambulio la wachawi. Kitabu cha Ufunuo 12:11 kinasema: "Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo na kwa neno la ushuhuda wao." Itumie/itamke damu ya Yesu katika maombi ili kuharibu mipango yote ya giza.
Soma Neno la Mungu kila siku. Neno la Mungu ni upanga wa Roho (Waefeso 6:17). Ukilisoma kila siku litakuongezea imani. Mchawi akikupa vitisho mtamkie Neno la Mungu. Mwambie: “Imeandikwa katika Isaya 54:17: "Silaha yoyote itakayofanyika juu yangu haitafanikiwa."
Hiyo ni kinga tosha.
Mkemee(mpinge) shetani. Kemea wachawi na mapepo kwa Jina la Yesu. Kukemea ni kuamuru yatoke. Tamka hivi: “Wewe mchawi, nakuamuru kwa Jina la Yesu, toka hapa.” Nakwambia atatimua mbio. Ukisikia au ukiona vitu vinavyokutisha tisha, fanya hivyo hivyo. Jina la Yesu lina nguvu sana kuliko nguvu za kichawi. Katika kitabu cha Yakobo 4:7 imeandikwa: "Mtiini Mungu, mpingeni Shetani, naye atawakimbia." Tunapokuwa thabiti katika Mungu na kumkataa shetani kwa imani, wachawi na nguvu zao wanasalimu amri.
Naamini kuanzia leo hutaogopa tena wachawi, mapepo na shetani. Ubarikiwe!