Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sababu mojawapo ya kuacha ni kutokana na sauti kubwa za mashirika ya kutetea haki za binadamu yaliyopo sasa. Sababu nyingine ni kwamba mahakama za leo ili mtu ahukumiwe lazima uwepo ushahidi usiotia shaka. Ni nani sasa anayeweza kuthibitisha mbele ya jaji kuwa amemuona shetani akiingia nyumbani mwake. Katika uzi huu nimekueleza kuwa matendo ya kichawi yanatokana na shetani na mapepo. Shetani huwezi kumuona kwa macho. Hivyo kuacha kuhukumu sio kwamba uchawi haupo.Hiyo mifano kama Salem witch trials zilikuwa zama za giza.. jiulize leo hii kwa nini wazungu wameacha kuhukumu na kuua wachawi ?
Nachomaanisha ni kwamba yapo mambo ni uchawi na mengine ni vitimbi tu vya majini wenyewe sio uchawi, lakini sio kila uchawi unafanywa na mchawi kwa maana hata wewe usiye mchawi unaweza ukafanya kitu kidogo tu na ukawa umemfanyia mtu uchawi pasina kushirikiana na majini.Tuko pamoja. Katika bandiko langu nimeeleza kuwa uchawi unatokana na shetani na mapepo(majini). Mchawi ni mtu anayeshirikiana kiutendaji na majini/mapepo
Swali lako ni zuri sana. Kama kuna wengine wana tiba watuelezee hizo tiba zao tuzijue. Mimi nimeongea kulingana na imani yangu. Mimi naamini kwamba nguvu ya kushinda wachawi na mashetani inapatikana kwa uwezo wa Yesu Kristo aliyepewa mamlaka yote mbinguni na duniani (Mathayo 28:18) na kwamba kwa jina lake, waumini wanaweza kushinda nguvu za giza (Luka 10:19, Wakolosai 2:15).Kwahiyo mkuu unataka kusema hakuna tiba yeyote ya mambo ya kichawi wala majini isipokuwa tiba hiyo inapatikana kwa wakristo tu?
Thibitisha kwa hoja kuwa uchawi haupo
Kama huiamini Biblia una haki ya kusema uliyoyasema, sio kosa lako.
Kwa sababu unasema jini hawezi kutolewa na jini lenzake hapo ndio pamenishangaza kidogo.Swali lako ni zuri sana. Kama kuna wengine wana tiba watuelezee hizo tiba zao tuzijue. Mimi nimeongea kulingana na imani yangu. Mimi naamini kwamba nguvu ya kushinda wachawi na mashetani inapatikana kwa uwezo wa Yesu Kristo aliyepewa mamlaka yote mbinguni na duniani (Mathayo 28:18) na kwamba kwa jina lake, waumini wanaweza kushinda nguvu za giza (Luka 10:19, Wakolosai 2:15).
Sasa utasemaje tu kitu fulani hakipo hali ya kuwa hauna uhakika? Hivi kipi chenye kufanya watu waseme hakuna uchawi?Anayesema kitu kipo ndiye mwenye mzigo wa kuthibitisha kitu kipo.
Kwa sababu kilichopo ndicho kinathibitika kipo.
Kisichopo, nje ya nadharia tupu, hakithibitiki hakipo, kwa sababu hakipo na kama hakipo, hakithibitishiki kwamba hakipo.
Ukitaka mtu anayesema uchawi haupo athibitishe uchawi haupo, ni sawa na kumwambia mtu ambaye hajavamiwa na wezi na kuibiwa athibitishe kwamba hajavamiwa na wezi na kuibiwa.
Atathibitishaje?
Anayeweza kuthibitisha ni yule anayesema jambo limetokea. Anayesema kavamiwa na wezi na kaibiwa anaweza kuthibitisha kwa alama za vidole za hao wezi, anaweza kutoa video ya kuonesha wezi wakiingia kwake.
Sasa mtu anayesema hakuna wezi walioingia kwake unamtaka athibitishaje kuwa hakuna wezi walioingia kwake?
Unataka atoe alama za vidole za wezi ambao hawapo? Unataka atoe video ya wezi ambao hawapo?
Polisi wakisema una madawa ya kulevya nyumbani kwako, wao ndio wana wajibu wa kuyasaka na kuyapata.
Hawakuambii wewe mtuhumiwa ambaye unasema huna madawa ya julevya uthibitishe huna madawa ya kulevya.
Utathibitishaje huna madawa ya kulevya?
You can't prove a negative.
Wewe unayesema uchawi upo ndiye mwenye wajibu wa kuthibitisha uchawi upo.
Anayesema uchawi haupo yeye kazi yake ni kutaka uthibitisho tu kuwa uchawi upo.
Wapi nimesema sina uhakika ?Sasa utasemaje tu kitu fulani hakipo hali ya kuwa hauna uhakika? Hivi kipi chenye kufanya watu waseme hakuna uchawi?
Mbona athari za uchawi tunaziona kwa macho mkuu kama tunavyoona athari za stress au addiction, au wewe unaelewa uchawi ni nini?Wapi nimesema sina uhakika ?
Ukitaka mtu anayesema uchawi haupo athibitishe uchawi haupo, ni sawa na kumwambia mtu ambaye hajavamiwa na wezi na kuibiwa athibitishe kwamba hajavamiwa na wezi na kuibiwa.
Atathibitishaje?
Ninasema kitu hakipo sababu hakionekani kwenye na organ za utambuzi.. ambazo ni macho, pua na sikio
Imani juu ya uwepo wa uchawi ni aawa na Imani juu ya uwepo Upako wa kiroho maana vyote ni non scientific proven. Tambua uchawi ni haupo, ila imani juu ya uchawi ipo kwenye vichwa vya watu
There is no scientific evidence to support the existence of witches.
- UCHAWI ,, Hizi ni imani zilizotokana na ujinga. Mjinga asipoelewa kitu anasingizia uchawi. Zamani magonjwa yote yalihusishwa na uchawi. Hata wazungu walikuwa hivyo nyakati za giza ( middle age / Victorian era.
- Watu wengi wanaoamini uchawi sababu kuu ni wana misunderstanding of science, superstition is “an irrational belief arising from ignorance or fear.”
- Dictionary inasema superstition (ushirikina) is abelief that is not based on human reason or scientific knowledge, but is connected with old ideas about magic, etc.:
- superstition
- a belief that is not based on reason or scientific thinking and that explains the causes for events in ways that are connected to magic:
Haupo sahihi kwa sababu unachomaanisha ni kwamba unataka kusema ili uchawi uwepo ni hadi hayo mambo uliyoyataja yangefanyika au yafanyike ndio tukubali uwepo wa uchawi, cha ajabu hapo ukitajiwa yanayofanyika kwa uchawi utakataa utasema sio uchawi ni imani tu.Kila siku nauliza swali hapa, kama uchawi upo kwanini babu zenu wakabebwa na kuvushwa bahari kwenda kupigwa mijeledi na kufanyishwa kazi za shamba huko nchi za mbali, na hili limefanyika karne na karne, hadi uingereza ilipoleta mapinduzi ya viwanda ndipo hayo mambo yakaisha.
Hao babu zenu wataalamu wa kuroga walishindwa kuroga wazungu? kama uchawi upo waitwe wachawi wote waroge team ya taifa ichukue kombe la dunia...
Hayo mambo ni imani, wenzenu wametoka huko, Mobutu world cup 1974 alienda Germany world cup na wachawi kama wote kutoka Zaire(Congo), huko ndiko wanasema kuna wachawi, kawaambia waroge wafunge magoli, badala yake Zaire ilipigwa jumla mabao 8...
so the qn is Why cant we use this juju thing we claim can do anything win ordinary world cup?
Kama uchawi upo na hao warogaji, kwanini wasiroge viongozi wala rushwa hii nchi wafe?
Kwanini wasiroge TANESCO wanaokata umeme hovyo ili wasirudie tena kukata umeme?
Kwanini wasiroge kuwepo na uchaguzi wa uhuru na haki?
Watoto wa waganga na wachawi watumie uchawi wanao washinde mitihani...
Thats because these things dont work, they dont exist.. mtu anaye amini huu upuuzi huwa namuona ni mjinga..
Kama uchawi kweli una nguvu, mbona hautumiki kuleta maendeleo ya maana na kubadili mambo makubwa yanayoathiri jamii? Kwa sababu kama uchawi unafanya kazi kwenye mambo madogo, basi ungetarajiwa ufanye kazi pia kwenye mambo makubwa.Haupo sahihi kwa sababu unachomaanisha ni kwamba unataka kusema ili uchawi uwepo ni hadi hayo mambo uliyoyataja yangefanyika au yafanyike ndio tukubali uwepo wa uchawi, cha ajabu hapo ukitajiwa yanayofanyika kwa uchawi utakataa utasema sio uchawi ni imani tu.
Kuna mambo mengi tu yanahusishwa na uchawi na ni makubwa tu, sasa kwanini uchague kutaja hayo mambo ili kutaka ionekane hakuna uchawi kisa hayo tu hayajafanyika?