Duh! Ndio maana nakwambia ufungue akili ili uweze kuelewa na sio kufuata mambo kimkumbo mkumbo. Sayansi ina kanuni zake ushahidi wake umejikita kwenye ushahidi wa kimwili na majaribio ambayo yanaweza kudhibitiwa na kurudiwa rudiwa kitu ambacho ni tofauti na uchawi ulivyo hali ambayo huleta ugumu kufanyia tafiti za kisayansi. Na ndio maana hata hiyo meditation faida zinazoelezwa kwa ushahidi wa kisayansi ni zile za kisaikolojia na kimwili tu ila meditation inatumika kwa mambo hadi ya kiroho kitu ambacho hakuna ushahidi wa kisayansi kuelezea faida hizo.
Wakati wewe unaifanya sayansi kama dini unasubiri uambiwe kipi uamini na kipi usiamini na kuacha kufungua akili yako, watu kama Doctor Joe dispenza anafundisha jinsi ambavyo tunaweza kujitibu pasina dawa wala upasuaji kwa kutumia meditation tu, hapo mwanzo alikuwa akisubiri sana kujaribu kushawishi tafiti zake za kazi anazofanya ili zikubaliwe kwanza ila amekuwa akipingwa.
Watu hawawezi kuka tu kusubiri mpaka ushahidi wa kisayansi upatikane ndio maana watu walikuwa wakifaidika na meditation toka karne hizo bila kusubiri sayansi iprove na ndio sawa na sasa watu wanafaidika na dowsing pamoja na energy healing, wewe unayesubiri hadi sayansi ije kuprove endelea kusubiri ila utambue pia kuwa sayansi haija disprove hivyo vitu ikiwemo na uchawi pia.
Najaribu tu kukuonyesha kwamba hata kama jambo halina ushahidi wa kisayansi usipende kuhitimisha kuwa hicho kitu hakipo au ni uongo na ndio maana nakuwa nataka tujadili hayo matukio yenye kuhusishwa na uchawi, lakini hapo ndio mnaanza kusema mara sijui ni mambo tu tusiyoyaelewa ila sio uchawi, mara inaweza ikawa ni placebo effect mara sijui tunachoona na kusema uchawi sijui akili inaweza kuwa inadanganywa n.k
Kifupi mnakwepa huu upande ndio maana mnalazimisha ushahidi wa sayansi.
Huna hoja kiongozi...
Bado unazunguka kwenye hoja zile zile , unakataa kuweka vigezo vya kuthibitisha uchawi lakini unataka uamini upo.
Umekomaa na meditation wakati nimekuelezea huko juu kuhusu meditation, halafu hapo hapo unasema meditation inaweza ponya mtu pasipo dawa au upasuaji, unarudi pale pale kwenye hoja zangu za biology of beliefs na placebo effect..
watu walikuwa wakifaidika na meditation toka karne hizo bila kusubiri sayansi iprove na ndio sawa na sasa watu wanafaidika na dowsing pamoja na energy healing, wewe unayesubiri hadi sayansi ije kuprove endelea kusubiri ila utambue pia kuwa sayansi haija disprove hivyo vitu ikiwemo na uchawi pia.
Hoja umeishiwa kiongozi..
Meditation nimekuelezea kiongozi inaweza kuwa explained kisayansi, nimeeleza pia masuala ya biology of beliefs, nimeeleza pia placebo effect, nimeeleza yote hayo lakini bado umekuwa king'ang'anizi kama zombie..
ipo hivi meditation ni masuala ya kuiprogram akili na ubongo kwa ujumla, meditation inaweza affect brain physically na kugusa maeneo tofauti ya ubongo mfano yanayohusika na stress na emotional control. Nenda kasome concept of neuroplasticity...
Hizo practices za meditation zinaweza pelekea kupunguza anxiety, ku improve focus, nakuongeza emotional resilience.
Hivi unaelewa sasa kuna vifaa maalum kama fMRI (Functional Magnetic Resonance Imaging) na EEG (Electroencephalogram) vinavyoweza kusoma shughuli za ubongo na kugundua ikiwa mtu ana huzuni, furaha, au hata msongo wa mawazo. Hivi ni vifaa vya kisayansi, si vya uchawi
Meditation inatumika kuiprogramu akili, na tunao ushahidi wa kisayansi unaoonyesha jinsi inavyoathiri mawimbi ya ubongo, lakini hiyo haimaanishi meditation ni nguvu isiyoeleweka au ni uchawi , ni mchakato wa kisaikolojia unaoweza kupimwa..
Sayansi imeweza kueleza jinsi meditation inavyofanya kazi kwa kutumia data halisi. Kama uchawi ungekuwa halisi, tungeweza kuutumia vifaa hivi kuuchunguza na kupima matokeo yake , lakini hakuna ushahidi wowote wa kisayansi unaoonyesha kwamba uchawi upo.
***Kama uchawi upo na una nguvu, kwa nini hauwezi kupimwa kama vile tunavyopima athari za meditation kwa ubongo?
Kingine tambua meditation inaweza kuelezeka kisayansi vizuri tu, na pia meditation ni ka kitu kadooogo sana mbele ya sayansi..
Uwepo wa meditation hauwezi replace sayansi, lakini sayansi ina replace meditation.
Meditation haitumiki kutengeneza madawa, magari, simu, au kutatua matatizo ya kihandisi. Sayansi inatumika kila sehemu, lakini meditation ni ndogo na haina matumizi mapana kama sayansi...
Meditation sio kila kitu. Huwezi kutumia meditation kutengeneza daraja, kupima vimelea vya ugonjwa, au kupeleka roketi mwezini. Lakini sayansi imewezesha yote hayo.
Meditation inaweza kusaidia kisaikolojia, lakini haina nguvu ya kimazingira inayoweza kupimika na kufuatiliwa kama nguvu ya sayansi. Ukiwa na kidonda, unaweza kufanya meditation siku nzima, lakini bila antibiotics, kinaweza kuoza...
Hivyo usiiweke meditation na uchawi kundi moja....
Tofauti ya uchawi na meditation.
Meditation haikuwahi kudai kuwa ni nguvu ya ajabu isiyoelezeka kama uchawi unavyodaiwa kuwa, ilikuwa inajulikana tangu zamani kama mbinu ya utulivu wa akili na mwili, watu hawakudai kuwa meditation inageuza risasi kuwa maji au inafanya mtu aruke angani...
Uchawi, kwa upande mwingine, unadai kuwa na uwezo wa kufanya mambo ya kimujiza yanayoshinda sheria za asili, kama kupaa, kutuma mapepo, au kugeuza vitu bila mawasiliano yoyote ya kimwili, hadi sasa, hakuna ushahidi wowote unaothibitisha haya...
**Ikiwa uchawi ni kweli na unaweza kuthibitishwa kisayansi, kwanini hakuna hata mshindi mmoja wa Tuzo ya Nobel aliyeonyesha uwepo wa uchawi?
Acha kujilisha upepo?
Najaribu tu kukuonyesha kwamba hata kama jambo halina ushahidi wa kisayansi usipende kuhitimisha kuwa hicho kitu hakipo au ni uongo na ndio maana nakuwa nataka tujadili hayo matukio yenye kuhusishwa na uchawi, lakini hapo ndio mnaanza kusema mara sijui ni mambo tu tusiyoyaelewa ila sio uchawi, mara inaweza ikawa ni placebo effect mara sijui tunachoona na kusema uchawi sijui akili inaweza kuwa inadanganywa n.k
Kifupi mnakwepa huu upande ndio maana mnalazimisha ushahidi wa sayansi.
1-Nini tofauti kati ya jambo la kweli na jambo la kufikirika?
Kama jambo ni la kweli, linapaswa kuwa na njia ya kuthibitishwa nje ya hisia za mtu binafsi au simulizi za watu. Vinginevyo, tunakubali kuwa kila imani ni kweli, hata zile zinazopingana, au hata uongo utakubali ni kweli, mtu akisema ameona nyoka ana vichwa saba naye asipingwe kwani ni mkweli.
2-Je, Unaweza kutofautishaje uchawi na udanganyifu au uongo wa kawaida?
Kazi kwako...