Tatizo ni mtazamo wako kuhusu sayansi ndio bado tatizo. wewe ndio unasema unaamini sayansi kitu ambacho si sahihi kusema hivyo, huwezi kusema unaamini sayansi kwa sababu sayansi si imani.
Tatizo la kuamini sayansi inakuwa unaifanya sayansi kama dini au ni kama mtu ambaye ndio anakuamulia kipi uamini ndio maana unatumia kauli kama hizo kusema "..sayansi haiyakubali hadi ithibitishwe". Ni rahisi hapo kusema kitu fulani si kweli kisa hakuna ushahidi wa kisayansi ila mara nyingi the person who says that has no training in science or the scientific method and wouldn't know a good experimental design if it sat on him.
Kama hadi sasa kusingekuwa na maelezo ya kisayansi kwenye meditation basi ungekuwa unaona wanaoamini kwenye meditation ni wajinga kisa hakuna maelezo ya kisayansi(ambayo yamekuja miaka ya juzi tu) kwa sababu mmefanya Science is somehow the arbiter of truth. Kwa jinsi unavyoichukulia sayansi hakuna tofauti na dini kabisa na ndio maana mmefanya sayansi ni mbadala wa kuamini dini au uchawi.
Hayo mambo ya sijui watu zamani hivi na
vile, mbona umeacha na kuweka mifano ya nadharia za kisayansi ambazo zilikuwa zikiaminika pia huko zamani ila sasa haziaminiki tena?
unashambulia mtazamo wangu kuhusu sayansi badala ya kujibu hoja zangu kuhusu uchawi..
Kwanza kabisa sijasema imani yangu ni sayansi, lakini sayansi mimi kwangu ni njia ya kupata ukweli.
Sio kwamba naamini sayansi kama dini, ni kwamba nafuata njia bora ya kugundua ukweli , na hiyo njia ni sayansi. Kama uchawi upo, basi uthibitisho wake upo wapi?
Hadi sasa hakuna mtu aliyewahi kuonyesha ushahidi unaoweza kurudiwa na kuthibitishwa, wewe una ushahidi gani kuhusu uchawi? hapo ndipo nakushinda hoja na naamua kusema uchawi haupo.. huna hoja ya kupinga hilo
Hayo mambo ya sijui watu zamani hivi na vile, mbona umeacha na kuweka mifano ya nadharia za kisayansi ambazo zilikuwa zikiaminika pia huko zamani ila sasa haziaminiki tena?
Ukiangalia historia, sayansi inarekebisha makosa yake kwa ushahidi mpya. Lakini uchawi haujawahi hata kuthibitishwa, sasa tungeuachaje?
Turudi kwenye hoja kuu na unijibu Kama uchawi upo, kwa nini hakuna mtu aliyewahi kuthibitisha kisayansi ama njia nyingine yeyote kwa mazingira yanayoweza kurudiwa na kuthibitishwa na wengine?
Wewe huna tofauti na wagiriki wa kale waliamini miungu yao, Zeus, Hades, Poseido walikuwa wanadhibiti dunia, hadi sayansi ilipokuja na kueleza hali ya hewa, radi na tsunami kwa njia ya kisayansi...
Kuna watu wa zama za kati hapo waliamini magonjwa yanatokana na mapepo au laana, lakini baadaye
sayansi iligundua vijidudu na chanzo halisi cha magonjwa... na ikapatikana tiba mfano:
Katika karne za nyuma, watu waliamini kuwa TB ni laana au uchawi, hasa kwa sababu wagonjwa walikuwa
wanadhoofika polepole na kudhoofika kwa mwili kulionekana kama wamefanyiwa ushirikina ama mambo ya
mizimu n.k wengine waliamini ni adhabu ya Mungu, Lakini mnamo 1882, mwanasayansi Robert Koch aligundua
kuwa TB inasababishwa na bakteria Mycobacterium tuberculosis, sio laana wala uchawi... Baada ya kugundua
chanzo cha kisayansi, watu walianza kutumia chanjo na antibiotics kuzuia na kutibu TB badala ya kutegemea
tiba za kimila au ibada za kuondoa laana... na walipona...
Kuna ugnjwa uliitwa tauni uliua zaidi ya watu milioni 50 barani Ulaya, wengine waliamin ugonjwa huu ni adhabu ya Mungu kwa dhambi za watu, wengine waliamini umeletwa na wachawi na mashetani, wengine
waliona ni laana imetokakwa wayahudi na wageni na wakaanza kwaangamiza, Lakini baadaye, sayansi
iligundua kuwa Tauni ilisababishwa na bakteriaYersinia pestis, wanaoenezwa na viroboto kutoka kwa panya...
baada ya hapo watu walianza kutumia dawa, kufuata kanuni za usafi na wakapona kweli...
je ni kitu gani kinachofanya uchawi uwe wa kweli zaidi kuliko imani hizo zingine ambazo watu walikuwa wanaamini lakini baadaye zikathibitishwa kuwa si kweli?
Kwa hiyo, kuendelea kuamini uchawi hauna tofauti na hao watu ambao waliishi katika nyakati za giza, huna tofauti...
Njoo kwenye vita, kwa maana uchawi unasadikika watu kuutumia kuroga maadui au kuroga mtu yeyote... nasikia wanaroga hata wezi... sasa:
Kama uchawi kweli upo na unafanya kazi, kwa nini haujawahi kutumika vitani kuangusha maadui? Kwa nini nchi hazitumii uchawi badala ya silaha za kisasa kama mabomu, drones, au silaha za nyuklia?
WWII hakuna taifa lolote lililotumia uchawi kushinda, waliotumia teknolojia bora kama ndege za kivita, mizinga, na silaha za kisasa ndio walioshinda.
Wazulu walikuwa na imani kubwa katika tiba za kichawi na kinga za sanaai za vita(art of war), lakini waingereza waliwashinda kwa urahisi kwa kutumia bunduki na mizingga... hawa ni wale wapiganaji wa jadi unakuta wana mganga anawapa dawan.k, lakini walibondwa mbaya mbovu..
Vita ya sasa Ukrine na Russia hakuna uchawi unaotumika, ni teknolojia na mbinu za kivita zinazotawala...
Kama uchawi unafanya kazi kweli, kwanini hautumiki vitani badala ya silaha? Kwanini hakuna mtu aliyewahi kushinda vita kwa kutumia uchawi?
Kinjekitile aliamini nguvu za uchawi, na wafuasi wake waliingia vitani wakiamini risasi zitageuka maji , lakini ukweli wa kisayansi ukashinda, risasi zilibaki kuwa risasi, na maelfu walikufa, Hii ni mfano halisi wa jinsi imani zisizo na msingi wa kisayansi zinavyoweza kuwaangamiza watu...
Kama uchawi upo na unafanya kazi kweli, kwa nini dawa ya maji ya Kinjekitile hayakufanya risasi kuwa maji? Kwa nini hawakushinda vita?
Naomba majibu tafadhali...