Matukio ya Kushangaza Duniani Yanayodaiwa Kusababishwa na Uchawi

Kwanza mkuu hii mitazamo ya kupambanisha sayansi na uchawi au na dini huwa inatoka wapi? kila kitu hapo kina nafasi yake. Uchawi utabaki kuwa ni uchawi na una kanuni zake na sayansi itabaki kuwa ni sayansi na ina kanuni zake.

Na ndio maana hata huo uchawi unaweza kupingwa kwa sababu ya kukosa maelezo ya kisayansi au ushahidi wa kisayansi, ni sawa na baadhi ya dawa za mitishamba ambazo watu wamekuwa wakitumia na kujitibu maradhi ila hakuna ushahidi wa kisayansi wa mitishamba hiyo kutibu hayo maradhi kwa sababu hakujafanyiwa uchunguzi wa kisayansi. Na kuna mambo mengi tu kama ya kitiba na kutatua changamoto mbalimbali ambayo bado kwa sasa hayana maelezo ya kisayansi lakini watu wamekuwa wakitumia na kufaidika nayo.

Hao wenzetu ambao ndio wagunduzi wa hivyo vifaa vya kiteknolojia ulivyovitaja ila ndio hao hao wamekuwa wakitumia energy healing kama Reiki ambapo unaweza kumtibu mtu kwa kutumia mikono peke tu au distant healing ambapo unaweza ukamtibu mtu aliye mbali huko, pia wanatumia remote viewing kupata taarifa za mtu,kitu au mahali fulani ukiwa mbali kabisa hii hadi serikali ya Marekani imetumia, kuna Dowsing ambapo huko zamani ilitumika kutafutia maji ardini kwa ajiri kuchimba visima ila sasa inatumika kwa mambo mengi sana. Vitu vyote hivyo havina ushahidi wa kisayansi ila vipo na vinatumika pengine siku vitakuja kupata maelezo ya kisayansi kama ilivyo kwa meditation sasa hivi wakati ilikuwepo toka enzi na enzi.

Kwahiyo sayansi inabaki kama ilivyo ndio maana hata waumini wa dini hufuata sayansi, huko kusema unaamini katika sayansi ndio huleta shida maana mnafanya sayansi kama aina fulani ya imani.
 
Kama kitu hakijathibitisshwa kisayansi kinabaki kuwa dai lisilo na uthibitisho, hoja yako kuhusu energy healing, remote viewing, au dowsing ni mifano ya madai yasiyo na ushahidi wa kisayansi wa kuaminika na ndio maana sayansi haiyakubali hadi ithibitishwe.

Kwahiyo sayansi inabaki kama ilivyo ndio maana hata waumini wa dini hufuata sayansi, huko kusema unaamini katika sayansi ndio huleta shida maana mnafanya sayansi kama aina fulani ya imani.
Sayansi haijengi imani bali inatafuta ukweli, unaposema "unasema unaamini sayansi," unajaribu kuifanya ionekane kama dini, lakini sayansi haitegemei imani kipofu , inatokana na ushahidi unaoweza kupimika na kuthibitishwa mara kwa mara....

Kuna mitishamba mingi ambayo imefanyiwa utafiti na kuthibitishwa kisayansi kuwa na madhara au manufaa, tofauti ni kwamba tiba inayothibitishwa na sayansi hupitia vipimo, tafiti, na majaribio makali kuhakikisha inafanya kazi kweli, siyo tu kwa mazoea au imani...
Hio mitishamba pia kuna ambao walijaribu na ikaleta matokeo, hio tayari ni moja ya njia ya kisayansi kufanya majaribio.

pengine siku vitakuja kupata maelezo ya kisayansi kama ilivyo kwa meditation sasa hivi wakati ilikuwepo toka enzi na enzi.
Meditation ilikuwepo tangu zamani, lakini sasa imeanza kuthibitishwa kisayansi kwa vipimo vya jinsi inavyoathiri ubongo na mwili. Hiyo ni tofauti kabisa na uchawi, ambao haujawahi kuonesha ushahidi wowote wa kisayansi toka zamani.


Unasema uchawi una kanuni zake kama unavyodai, basi kwanini hakuna uchawi ulioweza kuthibitishwa kwa kutumia njia yoyote inayokubalika iwe kisayansi n.k? kama kweli ni mfumo wa kweli unaofanya kazi, kwanini hautumiwi rasmi kutatua matatizo ya dunia?

James Randi(magician) aliwahi kutoa $1M kwa yeyote anayeweza kuthibitisha uchawi au nguvu za kipekee, alitangaza yeyote mwenye hizo nguvu athibitishe, walenda watu wengi walishindwa, hakuna mtu aliyeweza kuthibitisha hata mmoja!

Zamani, watu waliamini magonjwa kama kifafa na kichaa cha mbwa ni laana za uchawi, lakini leo tunajua zinatokana na virusi na matatizo ya mfumo wa neva.

Zamani mtu akipata schizophrenia (kusikia sauti, kuona vitu ambavyo havipo), iliaminika kuwa amerogwa, lakini sasa tunajua ni ugonjwa wa ubongo unaoweza kutibiwa kwa dawa.

Watu waliamini ukoma ni laana, lakini sayansi iligundua kuwa ni ugonjwa wa bakteria (Mycobacterium leprae).

Mtu anayeamini uchawi huwa namuona ni mjinga.
 
Tatizo ni mtazamo wako kuhusu sayansi ndio bado tatizo. wewe ndio unasema unaamini sayansi kitu ambacho si sahihi kusema hivyo, huwezi kusema unaamini sayansi kwa sababu sayansi si imani.
Tatizo la kuamini sayansi inakuwa unaifanya sayansi kama dini au ni kama mtu ambaye ndio anakuamulia kipi uamini ndio maana unatumia kauli kama hizo kusema "..sayansi haiyakubali hadi ithibitishwe". Ni rahisi hapo kusema kitu fulani si kweli kisa hakuna ushahidi wa kisayansi ila mara nyingi the person who says that has no training in science or the scientific method and wouldn't know a good experimental design if it sat on him.

Kama hadi sasa kusingekuwa na maelezo ya kisayansi kwenye meditation basi ungekuwa unaona wanaoamini kwenye meditation ni wajinga kisa hakuna maelezo ya kisayansi(ambayo yamekuja miaka ya juzi tu) kwa sababu mmefanya Science is somehow the arbiter of truth. Kwa jinsi unavyoichukulia sayansi hakuna tofauti na dini kabisa na ndio maana mmefanya sayansi ni mbadala wa kuamini dini au uchawi.

Hayo mambo ya sijui watu zamani hivi na vile, mbona umeacha na kuweka mifano ya nadharia za kisayansi ambazo zilikuwa zikiaminika pia huko zamani ila sasa haziaminiki tena?
 
Hatari
 
Bila tukio la Africa hii ni batili kabisaa.
KAZI ni kipimo cha utu
 
unashambulia mtazamo wangu kuhusu sayansi badala ya kujibu hoja zangu kuhusu uchawi..

Kwanza kabisa sijasema imani yangu ni sayansi, lakini sayansi mimi kwangu ni njia ya kupata ukweli.

Sio kwamba naamini sayansi kama dini, ni kwamba nafuata njia bora ya kugundua ukweli , na hiyo njia ni sayansi. Kama uchawi upo, basi uthibitisho wake upo wapi?

Hadi sasa hakuna mtu aliyewahi kuonyesha ushahidi unaoweza kurudiwa na kuthibitishwa, wewe una ushahidi gani kuhusu uchawi? hapo ndipo nakushinda hoja na naamua kusema uchawi haupo.. huna hoja ya kupinga hilo
Hayo mambo ya sijui watu zamani hivi na vile, mbona umeacha na kuweka mifano ya nadharia za kisayansi ambazo zilikuwa zikiaminika pia huko zamani ila sasa haziaminiki tena?
Ukiangalia historia, sayansi inarekebisha makosa yake kwa ushahidi mpya. Lakini uchawi haujawahi hata kuthibitishwa, sasa tungeuachaje?

Turudi kwenye hoja kuu na unijibu Kama uchawi upo, kwa nini hakuna mtu aliyewahi kuthibitisha kisayansi ama njia nyingine yeyote kwa mazingira yanayoweza kurudiwa na kuthibitishwa na wengine?

Wewe huna tofauti na wagiriki wa kale waliamini miungu yao, Zeus, Hades, Poseido walikuwa wanadhibiti dunia, hadi sayansi ilipokuja na kueleza hali ya hewa, radi na tsunami kwa njia ya kisayansi...

Kuna watu wa zama za kati hapo waliamini magonjwa yanatokana na mapepo au laana, lakini baadaye

sayansi iligundua vijidudu na chanzo halisi cha magonjwa... na ikapatikana tiba mfano:
Katika karne za nyuma, watu waliamini kuwa TB ni laana au uchawi, hasa kwa sababu wagonjwa walikuwa

wanadhoofika polepole na kudhoofika kwa mwili kulionekana kama wamefanyiwa ushirikina ama mambo ya

mizimu n.k wengine waliamini ni adhabu ya Mungu, Lakini mnamo 1882, mwanasayansi Robert Koch aligundua

kuwa TB inasababishwa na bakteria Mycobacterium tuberculosis, sio laana wala uchawi... Baada ya kugundua

chanzo cha kisayansi, watu walianza kutumia chanjo na antibiotics kuzuia na kutibu TB badala ya kutegemea

tiba za kimila au ibada za kuondoa laana... na walipona...

Kuna ugnjwa uliitwa tauni uliua zaidi ya watu milioni 50 barani Ulaya, wengine waliamin ugonjwa huu ni adhabu ya Mungu kwa dhambi za watu, wengine waliamini umeletwa na wachawi na mashetani, wengine

waliona ni laana imetokakwa wayahudi na wageni na wakaanza kwaangamiza, Lakini baadaye, sayansi

iligundua kuwa Tauni ilisababishwa na bakteriaYersinia pestis, wanaoenezwa na viroboto kutoka kwa panya...

baada ya hapo watu walianza kutumia dawa, kufuata kanuni za usafi na wakapona kweli...

je ni kitu gani kinachofanya uchawi uwe wa kweli zaidi kuliko imani hizo zingine ambazo watu walikuwa wanaamini lakini baadaye zikathibitishwa kuwa si kweli?
Kwa hiyo, kuendelea kuamini uchawi hauna tofauti na hao watu ambao waliishi katika nyakati za giza, huna tofauti...

Njoo kwenye vita, kwa maana uchawi unasadikika watu kuutumia kuroga maadui au kuroga mtu yeyote... nasikia wanaroga hata wezi... sasa:
Kama uchawi kweli upo na unafanya kazi, kwa nini haujawahi kutumika vitani kuangusha maadui? Kwa nini nchi hazitumii uchawi badala ya silaha za kisasa kama mabomu, drones, au silaha za nyuklia?

WWII hakuna taifa lolote lililotumia uchawi kushinda, waliotumia teknolojia bora kama ndege za kivita, mizinga, na silaha za kisasa ndio walioshinda.

Wazulu walikuwa na imani kubwa katika tiba za kichawi na kinga za sanaai za vita(art of war), lakini waingereza waliwashinda kwa urahisi kwa kutumia bunduki na mizingga... hawa ni wale wapiganaji wa jadi unakuta wana mganga anawapa dawan.k, lakini walibondwa mbaya mbovu..

Vita ya sasa Ukrine na Russia hakuna uchawi unaotumika, ni teknolojia na mbinu za kivita zinazotawala...


Kama uchawi unafanya kazi kweli, kwanini hautumiki vitani badala ya silaha? Kwanini hakuna mtu aliyewahi kushinda vita kwa kutumia uchawi?

Kinjekitile aliamini nguvu za uchawi, na wafuasi wake waliingia vitani wakiamini risasi zitageuka maji , lakini ukweli wa kisayansi ukashinda, risasi zilibaki kuwa risasi, na maelfu walikufa, Hii ni mfano halisi wa jinsi imani zisizo na msingi wa kisayansi zinavyoweza kuwaangamiza watu...

Kama uchawi upo na unafanya kazi kweli, kwa nini dawa ya maji ya Kinjekitile hayakufanya risasi kuwa maji? Kwa nini hawakushinda vita?


Naomba majibu tafadhali...
 
Kuna vitu unashindwa kuelewa unajichanganya, hauweleweki hoja yako ni kwamba hakuna uchawi kabisa? Au hakuna ushahidi wa kisayansi kuhusiana na uchawi? Au unalinganisha manufaa ya sayansi na uchawi? Au unapinga tu kila ambacho hakina maelezo ya kisayansi kwa sababu wewe unaamini sayansi?

Hebu kwanza nijibu ili twende sawa.
 
Nasema kwamba uchawi haupo kwa sababu hizo zote nilizotaja huko juu, ambacho huelewi nini hapo kiongozi?
Ni kwamba hakuna uchawi na hakuna uthibitisho wowote wa kisayansi au namna yeyote uaothibitisha uchawi upo.. kumbuka hivyo vinategemeana, kama uthibitisho upo basi uchawi upo, hapo the key ni uthibitisho uwe wa kisayansi au hata kwa kushuhudia tu...

Naendelea kukuuliza ama huo uchawi unaleta utajiri kwanini hauna wachawi wanaopata pesa kimaajabu kuwazidi kina Elon Musk na Jeff Bezos, n.k


Kuamini uchawi huna tofauti na wale wazee wa zamaniwaliokuwa hawana elimu yeyote wakiamini kuzaa albino ni mikosi, laana n.k
Hizo hizo imani ndizo hizo hao wajinga huua albino kwa imani za kipuuzi...
 
Umeandika vyote ila umesahau kuhusu 'TRASMOZ' nenda google kwa taarifa zaidi 😀
 
Wewe uliwahi kufanya uchunguzi kujua ukweli kuhusu uchawi? Hebu nieleze ni yapi uliwahi kufanya kujiridhisha hakuna uchawi na hayo yenye kudhaniwa kuwa ni uchawi si uchawi ni nini? Hebu tuanzie hapo kwanza.

Hayo ya kusema kama uchawi upo mbona haujafanya hiki na kile si hoja ya msingi maana hata sasa kuna magonjwa ambayo hakuna tiba kisayansi ila zipo tiba mbadala.
 
We unaamini uchawi upo? tuanzie hapo halafu na mimi nitasema...
 
We unaamini uchawi upo? tuanzie hapo halafu na mimi nitasema...
Ndio naamini uchawi upo, binafsi nimeshuhudia masuala ya uchawi kwa namna mbalimbali na pia nimepata kusimuliwa matukio ya kweli ya kifamilia yenye kuhusu uchawi.
 
Ndio naamini uchawi upo, binafsi nimeshuhudia masuala ya uchawi kwa namna mbalimbali na pia nimepata kusimuliwa matukio ya kweli ya kifamilia yenye kuhusu uchawi.
Wewe huna tofauti na wale waliosema kuna ndege za UFO na viumbe wanaoitwa aliens,wana akili nyingi sana na wana sayansi ya hali ya juu...

Ikiwa uchawi upo, kwa nini hauwezi kuthibitishwa kwa njia ya kisayansi au njia yeyote ile? Kwa mfano, tunaweza kupima dawa hospitalini na kuona jinsi inavyofanya kazi kwa watu mbalimbali kwa njia thabiti. Lakini hakuna mtu aliyewahi kuonyesha uchawi ukifanya kazi katika mazingira ya maabara au kupitia utafiti huru unaoweza kurudiwa na wengine. Kwa nini uchawi hauwezi kupimwa na kuthibitishwa kama ilivyo kwa tiba, teknolojia, au fizikia?

Naomba majibu...
NB:
Siamini kama uchawi upo, naamini sayansi..
 
Hebu nieleze ni yapi uliwahi kufanya kujiridhisha hakuna uchawi na hayo yenye kudhaniwa kuwa ni uchawi si uchawi ni nini? Hebu tuanzie hapo kwanza.
 
Hebu nieleze ni yapi uliwahi kufanya kujiridhisha hakuna uchawi na hayo yenye kudhaniwa kuwa ni uchawi si uchawi ni nini? Hebu tuanzie hapo kwanza.
Mkuu, unaelewa dhana ya burden of proof?
ushahidi uko kwa yule anayefanya madai ya kuwepo kwa kitu fulani, si yule anayepinga. Kama unasema uchawi upo, basi ni jukumu lako kuleta uthibitisho wa kisayansi unaoweza kurudiwa reproducible evidence, kuthibitisha madai yako.

Kwanini Siwezi kudhibitisha kitu kisichopo? , Mimi kusema kuwa uchawi haupo ni sawa na kusema hakuna dragons duniani , kama mtu anasema dragons zipo, basi ni kazi yake kuonyesha ushahidi wa dragon moja, si kazi yangu kuzunguka dunia nzima kuhakikisha hakuna dragon , ukisema uchawi upo, ni kazi yako kuleta ushahidi wa kisayansi kuthibitisha, si kazi yangu kuthibitisha kuwa haupo..

Jinsi Nilivyojiridhisha uchawi haupo, Uchawi ungekuwa upo, tungeweza kuupima kwa njia za kisayansi kama tunavyofanya kwa dawa au teknolojia. Lakini hadi leo hakuna mtu aliyewahi kuonyesha uchawi ukifanya kazi katika mazingira yaliyodhibitiwa kisayansi. Kuna majaribio mengi yaliyowahi kufanywa na watu wakiahidi kuonyesha uchawi, lakini wote wameshindwa kuthibitisha..

James Randi alitoa tuzo ya $1,000,000 kwa yeyote anayeweza kuthibitisha kwa njia ya kisayansi kuwa uchawi unafanya kazi, watu wengi walijaribu, hakuna aliyefanikiwa..

Sasa, badala ya kuniambia nijiridhishe kuwa uchawi haupo, naomba wewe uniletee ushahidi wa kisayansi unaoweza kurudiwa kuthibitisha uchawi upo. Tafadhali, leta angalau utafiti mmoja huru uliochapishwa na kuthibitishwa na wataalamu wengine unaoonyesha uchawi unafanya kazi. Kama huwezi, basi hilo linamaanisha kuwa unaamini katika kitu ambacho hakina ushahidi, sawa na mtu anayeamini kuwa UFO zipo ns huwa zinabeba watu bila uthibitisho wowote..
 

Uchawi haupo. Ila imani juu ya uchawi ipo kwenye vichwa vya wajinga kama wewe
 
Hebu nieleze ni yapi uliwahi kufanya kujiridhisha hakuna uchawi na hayo yenye kudhaniwa kuwa ni uchawi si uchawi ni nini? Hebu tuanzie hapo kwanza.

Umezidiwa hoja sasa Unaleta logical fallacy inaitwa burden of proof.

Tambua humu hakuna wajinga wa kuwadanganya kwa ujanja ujanja.

Shifting the Burden of Proof (Kubadili Mzigo wa Ushahidi)

Kudai kuwa huwezi kuthibitisha madai yako, bali mpinzani wako lazima athibitishe kuwa ni ya uongo.

Ndio maana umehamisha magoli unasema
  • “Wewe thibitisha kuwa uchawi haupo.”
 
Mkuu sikufichi... Hii chuki yako kwa shetani haina kipimo..

Nashauri.. Ungana na Rose Muhando. Mumpige pande zote mpaka Muhakikishe Shetani hatauona uchaguzi huu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…