Matukio ya kusikitisha katika Uongozi wa Kikwete {2010 - 2015}

Matukio ya kusikitisha katika Uongozi wa Kikwete {2010 - 2015}

TETEMA

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2013
Posts
219
Reaction score
38
TAREHE 05-01-2011
Police wawapiga risasi watu zaidi ya 11 ktk maandamano ya CHADEMA. Waua watu 3.

TAREHE_10-2011
Dk.Mwakyembe aenda India kutibiwa kutokana na Kupewa Sumu.PoliCCM walipotezea kisiasa.

TAREHE_02-2012
Shehe Ali khamis Kuuawa kwa mapanga.

TAREHE 26-06-2012
Dr.Ulimboka akatekwa na kufanyiwa unyama.

TAREHE 18-07-2012
Mv spice yazama.

TAREHE 02-09-2012
Daudi Mwangosi auliwa na polisi Iringa.

TAREHE 28-09-2012
LHRC Waishtaki serikali ya K.. ICC

TAREHE 12-10-2012
Mtoto kudhihaki Kitabu kitakatifu (haijawahi kutokea Tz)

TAREHE 16-10-2012
Shehe Farid A. Hadi kiongozi wa Uhamsho kutekwa na kupotea(Alipatikana)

TAREHE _12-2012
Padre Ambrose apigwa risasi Zanzibar

TAREHE _02-2013
Padre Evarist Mushi apigwa risasi Zanzibar.

TAREHE 18-02-2013
Matokeo kidato cha 4 mabovu,haijawahi kutokea duniani tangu kuumbwa kwa Adam na Hawa.
Waliopata div 4 na 0 ni takriban 95%

TAREHE 05-03-2013
Kibanda afanyiwa ya Ulimboka.

TAREHE _03-2013
Lwakatale (mkurugenzi wa usalama CHADEMA) atuhumiwa kwa Ugaidi.

TAREHE 17-04-2013
wabunge 6 wa CHADEMA watolewa nje ya bunge,Ndugai/naibu spika awapa adhabu ya kutoingia bungeni siku 5 kinyume na kanuni za bunge.

Siku hiyohiyo mh.Lema amtaja Rais kuwa ndie mwanzilishi wa udini.

TAREHE 25-04-2013
Lema avamiwa usiku wa manane na polisi kwa amri ya Mulongo/mkuu wa mkoa wa Arusha

UPDATE,

TAREHE 05-05-2013
Mlipuko watokea kanisani Arusha...
Mheshimiwa rais akiwa angani na ndege kuelekea Kuwait kuta..


TAREHE 08-05-2013
Lwakatale/mkulugenzi wa usalama wa CHADEMA afutiwa mashtaka ya ugaidi.

MWAKA 2013
.Deni la taifa lafikia tril.22 wakati Kikwete alikuta deni ni tril.5

.Dola moja=1,600 tshs wakat alikuta dola moja=600tshs.

TAREHE 14-05-2013
tetesi za
Kikwete kuandaliwa mpango wa kuwa rais wa Tz hadi mwaka 2017 badala ya mwaka 2015,ili asimamie kukamilika kwa uundwaji wa katiba mpya.
Source,Mh.Pro.Lipumba.

UPDATES:

TAREHE 18-05-2013
Tetesi: Kanisa la TAG ladaiwa kuchomwa moto leo hii....


TAREHE 19-05-2013
Iringa, Police wawashambulia Wamachinga kwa Mabomu ya machozi kuwaondoa eneo wanalofanyia kazi.
Mh.Mch.Msigwa Mbunge wa Iringa Mjini akamatwa na Police.
Tare.20-05-2013 Mhe.Msigwa atolewa Lupango kwa dhamana.


TAREHE 22-05-2013
Ukaidi wa Kikwete na waziri wake wa nishati na madini wasababisha vurugu Mtwara watu wakipinga ujenz wa bomba la gesi kwenda Dar.
Zaidi ya watu 6 wakiwemo Police wauawa.

(kama kunanilichokisahau ama kukosea nikumbusheni at)

mfano,Tarehe aliyosema hajui kwanini Tz ni maskin,msongamano wa magali dar ni ishara ya maisha bora,n.k
pia anaekumbuka idadi ya safar za mheshimiwa.
 
JK mnamuandama lakini ni zaidi ya NYERERE wenu....haya yanayotokea ni sababu ya shina bovu alopanda nyerere ...na yeyey mambo yalimshinda , alikoswa kupinduliwa mara 3
alifunga watu hovyo
watu walipotea hovyo
hakukuwa na wa kumsema kama unavosema wewe leo
wote walikua ni zidumu fikra za Nyerere
na zimwi lake limewafanye wengi kama wewe kuto fikiri zaidi ya nyerere....
 
JK mnamuandama lakini ni zaidi ya nYERERE wenu....haya yanayotokea ni sababu ya shina bovu alopanda nyerere ...na yeyey mambo yalimshinda , alikoswa kupinduliwa mara 3
alifunga watu hovyo
watu walipotea hovyo
hakukuwa na wa kumsema kama unavosema wewe leo
wote walikua ni zidumu fikra za nyerere
na zimwi lake limewafanye wengi kama wewe kuto fikiri zaidi ya nyerere....

Mkuu hapa kuna arufu ya genocide.wakati viongozi wakichukulia "upepo unapita"
Obama wakati kunatokea janga la sundy alikuwa na ziara Izraeli,lakini arirudi.Mkuu kwa hili mh.hana budi kurudi.hata kama unasafari gani nyunbani kukitokea msiba, lazima urudi msibani!!!!!
 
kuwa makini na uandishi wako maana unamislead watu,haijawahi tokea kwenye maandamano ya chadema wakauawa watu 27
 
kipindi cha nyerere hatukuona mabomu misikitini au kuuwawa kwa masheikh,,,,,kama kukandamizwa uislamu ulifanywa na ukoloni, mwarabu hakujenga shule ila misikiti. mkoloni alijenga shule ambazo nyerere alizipokonya kutoka kwa wakristo na kufanya ziwe za serikali. kama hujajua impact ya elimu mpaka sasa hauwezi ungaongea suala lolote dunia ya sasa ukaeleweka,
 
Rais anapo taka kuliacha taifa katika hali mbaya, anamadhumuni gani?
Anatukomoa?
Tutajiokoaje kama taifa?
 
Kama kunanilichokisahau naomba mkiandike ili tujitathmini kama taifa
 
Unajua wewe akili yako ndogo,Rais wangu hawajamaa kuwapa UHURU wa kuongea wanakosa ustaarabu,upende usipende mamlaka yoyote ile iwe mbaya au Nzuri imewekwa na MUNGU,maneno yako hayo machafu unayotoa unashindana na MUNGU aliyemweka HAPO alipo.Ndugu hutakiwi kumlaumu Rais wako hata kidogo,mimi sio mshabiki wa vyama ila lazima ukweli niseme.

KIKWETE NI RAIS SAFI,SIKULAZIMISHI UAMINI LAKINI HUO NDIO UKWELI.


MUNGU IBARIKI TANZANIA,WASEMEE WOTE WALIO KINYUME NA SERIKALI ULIYOWEKA WEWE
 
Zile nguvu alizotumia kuingia ikulu ...alichoenda kufanya ndio hiki?aibu sana!chama wabadilishe utaratibu,wachague wao mtu ataefaa kamati ya maadili wapendekeze watu 3 waliaondaliwa kuwa wagombea (China) hao ndio wakapigiwe kura kwa wajumbe wa NEC na Mkutano Mkuu!sio watafute wafanya biashara wenye pesa haramu kuwasaidia kuingia madarakani!watawalipaje hao wafanya biashara??kama si richmonduli na EPA?sasa wanatunga vitengo na kuchota 29Bil ikulu ili walipe wafadhili pesa zao!
 
Nijuacho ni kuwa JK hakuwa chaguo la Mwl.
Na haya yanatukuta bse tumekiuka maagizo ya mwalimu Ben analijua ilo!
 
kuwa makini na uandishi wako maana unamislead watu,haijawahi tokea kwenye maandamano ya chadema wakauawa watu 27

nashukuru mkuu,naomba kurekebishwa pale ninapo kosea.
Hii thred inamaana kubwa sana kwa taifa letu.
 
Jifikilie kwanini hatumsemi mhe.Mwinyi au Mkapa?
Udhalimu wa serikali ya awamu ya 4 kwa miaka 3 tu, unazidi udhalimu wa miaka ya viongozi wote waliotangulia.
 
JK mnamuandama lakini ni zaidi ya NYERERE wenu....haya yanayotokea ni sababu ya shina bovu alopanda nyerere ...na yeyey mambo yalimshinda , alikoswa kupinduliwa mara 3
alifunga watu hovyo
watu walipotea hovyo
hakukuwa na wa kumsema kama unavosema wewe leo
wote walikua ni zidumu fikra za Nyerere
na zimwi lake limewafanye wengi kama wewe kuto fikiri zaidi ya nyerere....

Huyu jamaa sijui anafikiria kwa kutumia nin..maana si makalio tu hi ni low zaidi ya makalio. hapa nyerere kaingiaje? ndugu na wewe ni mmoja ya wanaosubir matokeo KUREKEBISHWA nin? maana huna hoja unakurupuka tu wewe naona kichwan umejaa mapepo ya ujinga na umaamuma. usitetee mtu kama huna hoja ni kumdhalilisha hata unayemtetea maana anaonekana ana watu hopeless na kama kiongoz ana wafuasi hopeless naye anaonekana ni hope less.acha kumdhalilisha rais kwa kutoa hoja za kijinga kama hizo nyerere nyerere kitu gan? kusoma hujui hata kuangalia picha? kama huna hoja za kumtetea rais acha sisi tutajipanga kumtetea kwa hoja siyo maneno ya kijinga kama yako
 
Kumbukumbu nzuri sana tuwaombe mods watuwekee kwenye Sticky
Wakuu Paw, tusaidieni kuweka hii records sawa Sticky.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hapa kuna arufu ya genocide.wakati viongozi wakichukulia "upepo unapita"
Obama wakati kunatokea janga la sundy alikuwa na ziara Izraeli,lakini arirudi.Mkuu kwa hili mh.hana budi kurudi.hata kama unasafari gani nyunbani kukitokea msiba, lazima urudi msibani!!!!!

hauko sawa sana kwenye maelezo yako jk unayembeza aliyofanya hajawahi kufanya rais yeyote waliomtangulia.haya matukio unayotaja mbona hata awamu zilizopita yalikuwepo au unachuki na jk.
 
Ukiona mtu anakuwa na mawazo ya kupinga kila kitu atakuwa na shida kwenye tafiti zake huwezi kuwa mtu mwema kwa kupinga kila kitu sijawahi kuona.
 
Back
Top Bottom