1. Ziara ya PM Njombe kukatishwa na Kauli Tata kumhusu JPM iliyotolewa Masjid (kuwa Mpendwa wetu yupo kazini anachapa kazi).
2. Ndege kadhaa za kijeshi kuonekana sana angani uelekeo Nairobi,
3. Kauli za kutisha wananchi wanaotaka kujua Hali ya mpendwa wao (Kauli ya Bashungwa),
**Kila nikikumbuka napata simanzi.
**RIP Shujaa
Tanzania lost a very good president despite the blame by a few people whose interests were stormed.
It is believed from independent sources that JPM passed away on 12th March 2021 around 1730hrs, but his death was strategically held secret until the internal power struggling by influencing figures was addressed.
Akitangazia Taifa jana Jumatano 17, 2021 kupitia Shirika la Taifa la Utangazaji(TBC1), Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa masikitiko na hali ya majonzi alisema siku 12 kabla ya umauti wake, Rais Magufuli alilazwa Machi 6 mwaka huu katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
Hata hivyo, siku tisa kabla ya kuanza matibabu yake Rais John Magufuli alikutana na wakazi jiji hilo la Dar es Salaam Februari 26, akishiriki uzinduzi huku akitoa ahadi zake kwa Watanzania ambazo zilikuwa za mwisho kabla umauti kumkuta.
Akiwa katika manispaa ya Temeke, Rais John Magufuli aliagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza mkopo wa Sh12 bilioni uliotolewa na benki ya CRDB kwa halmashauri ya Temeke.
Siku mbili kabla ya tukio hilo, Rais John Magufuli alizindua daraja la juu la Ubungo alilolitambulisha rasmi kuitwa Daraja la Kijazi Interchange ili kutambua utumishi uliotukuka wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Marehemu Balozi Mhandisi, John William Kijazi ambaye pia alifariki dunia Februari, 17 mwaka huu.
Siku ya uzinduzi huo, Rais John Magufuli aliwahakikishia wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuwa dhamira yake ya kuliboresha jiji hilo ipo palepale na kwamba baada ya kazi nzuri ya kuzijenga barabara kuu.
“Serikali itajielekeza kujenga barabara za mitaani kwa kiwango cha lami, kujenga barabara za juu katika makutano 10 ya barabara na kuimarisha huduma nyingine za kijamii,” alisema John Magufuli akiwa katika ziara hiyo.
Alisema anakusudia kuivunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na badala yake halmashauri mojawapo ya Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam itapandishwa hadhi na kuwa Jiji ili kuondoa hali ya sasa ambapo kuna halmashauri ya jiji inayotumia maeneo ya utawala ya halmashauri za Manispaa ambapo baadaye alikuja kufanya hivyo na kuifanya Ilala kuwa halmasahauri ya jiji.
RIP The son of Rubambangwa, Chato, the pumpkin of Tanzania and Africa
Watanzania wanakukumbuka sana kwa ucheshi na maamuzi kwa maslahi ya nchi na wananchi bila kujali utu wa watu wachache waliokuwa wanasababisha shida kwa wengine.
Kwa kuwa kifo cha JPM kina utata kwa mjibu wa wananchi wenyewe; ili kuiondoa nadharia kadhaa ovu utawala uliopo ni sharti wachunguze na kutoa majibu ya uhalisia na uwajibikaji ufanyike.
Je, alifariki tarehe
1. 10 Machi 2021?
2. 12 Machi 2021?
3. 17 Machi 2021?
4. Aliugua nini?
5. Kwanini Watanzania walifichwa?
6. Kwanini baada ya kifo chake kuna baadhi ya viongzoi waandamizi wa serikali , vyama vya siasa na wafanyabiashara walisherehekea hadharani na vifichoni?
7. Je, Utawala uliopo kwa sasa una uhakika gani baada ya kutoka madarakani hatakabiliwa na mashtaka kwa kushindwa kwa kushindwa kudumisha utengamano miongoni mwa watawaliwa huku baadhi ya watu waliokuwa na chuki binafsi na JPM wakitazamwa bila hatua zozote wakiendelea kumdhalilisha na kumzushia tuhuma zisizo na uthibitishona bila uwepo wa mtuhumiwa aijitetee binafsi?