Matukio yanayokumbukwa wakati wa ''infidelity''...

Matukio yanayokumbukwa wakati wa ''infidelity''...

tumalizane na 'mwizi' wangu, aliyeniibia with intent to do so.........ndicho nilichomaanisha kwa kumalizana, then huyo baba watoto sasa tutalonga nayeye, kikieleweka haya kisipoeleweka verdict itatoka either case.

ha ha ha mamushka naona move yake itakua kama ivi....

Mkazi mmoja wa kitongoji cha Madimka Maditeza wilayani Mkuranga mkoani Pwani Mariamu Ramadhani ameuawa kwa kuchomwa kisu kwenye titi la kushoto baada ya kufumaniwa nyumbani kwake akifanya mapenzi na mume wa mtu. Akisimulia mkasa huo, Kamanda Mwakyoma amesema Aisha alipata tetesi za kuibiwa mumewe ndipo alipoanza kufuatili nyendo za mumewe na kupata habari kuwa yuko nyumbani kwa Mariam.
Amesema Aisha aliwafuma mumewe Mohamed Ningwe na mwanamke huyo wakifanya mapenzi na ndipo zilizuka purukushani zilizosababisha mauaji hayo.
 
Mbu I feel your pain!

Na pengine kuna siku mkuu kwa kutambua kuwa ni yatima ulitoa pesa amabyo ulikuwa wewe ukamlipe mdogo wake halali school fees lakini kwa kujua kuwa huyo yupo hapo home atasubiri kwanza ukaona bora umsaidie aliye kwenye mazingira magumu!

Asa siku ya cku umetonywa unaenda kukakuta kajamaa kamevaa ile boxer yako uliyoipenda sana ulinunua 30 usd pale Woolworth JHB na katika hali ya kutatanisha baada ya kuivaa mara moja ikapotea ukaambiwa umeipoteza safarini kwa nini yeye aliipack the last safari you went!

...ha ha ha! duuu, Mw'Mungu apishilie mbali aiseee...kisasi chake nitakula sahani moja na mashoga zake na wadogo zake wote, na bado kilio kitabakia rohoni!
(am joking!)

Arrggh, Mw'Mungu atanilipia bana. :lie:
 
nimefurahi kuskia uko mzima, mimi niko fiti kuliko kampeni za chadema.

kwakweli hali inatisha sana! wengi wanaingia kwenye ndoa kwa kushawishiwa na michezo ya majuto. hawako serious kabisa.

klorokwini una vijimaneno jamani,atleast nimecheka coz hii thread imenikumbusha machungu mengi.
 
tumalizane na 'mwizi' wangu, aliyeniibia with intent to do so.........ndicho nilichomaanisha kwa kumalizana, then huyo baba watoto sasa tutalonga nayeye, kikieleweka haya kisipoeleweka verdict itatoka either case.

Mwizi ni baba watoto wako; huyo bibie yeye kajikinga jua ama mvua hapo asa weye uko katika ya mvua kubwa ikatokea mssada wakuokolewa usilowane...................ku deal na huyo ni kumuonea haijalishi hata ukimkuta ndo anamkatikia cha mwisho!
 
kuna mdada kenya alijitangazia redio ya kijijini kwamba katekwa nyara na jamaa anataka ransom ndio amuachie. khaaaa ! baada ya kufuatiliwa kumbe jamaa alikuwa kamuweka kinyumba mdada wa watu na raha wanakula alfajiri na usiku. yule bwana wake baada ya kushtukizia mpaka leo kapata stroke hata jina la rais wake "mwai kibaki" hawezi kulitamka. Muumba amponyeshe haraka(tusemeni amen)
 
Mbu...hiyo ni mikiki mikiki ya ndoa, yaani nimejifunza mengi sana kwenye hii sekta, baada ya hilo tukio kwa upande wake nimepumzika kabisa kwa sasa.....

Pole sana bana.
Mapenzi na Ndoa ni PROMISES, zikishavunjwa sidhani hata AM SORRY kwa lugha yeyote inasaidia lolote.
Ngumu sana kusamehe, itakuwa kujisahaulisha?
 
nilihic nikienda na gari akiiona tu anaweza kwenda kushinda ******, nikaenda na tax, mwendo wa pole kabisa tena wa kujichanganya na meza nyingine nakunywa ballantin yangu pole pole, nilivyoona kichwa kimeanza kupata moto ndio nikawa nawasogelea taratibu tu.....cku zile ashukuru alikimbia mana sasa hvi ungenikuta mie cna ndoa, alimuomba mama nyamayao akae japo wiki moja hapo home mana haamini kama mke wake kamsamehe, ucku naona alikuwa hapati ucngizi mana nikijigeuza tu na mwenyewe anageuka, cjui alidhani nitamfunika na mto, ckuwahi kumuuliza/kuhoji tena mpaka leo kuanzia mama nyamayao alivyotupatanisha, hakuamini kama nimeweza kumsamehe....yule dada nae bora alitimika coz nilipata hacra kujua kadada kanakonisumbua ndio haka, yaani kalipata wazo zuri la kutimka......

lol!!! jamni huyo shemeji alipata adhabu kubwa mno
 
kuna mdada kenya alijitangazia redio ya kijijini kwamba katekwa nyara na jamaa anataka ransom ndio amuachie. khaaaa ! baada ya kufuatiliwa kumbe jamaa alikuwa kamuweka kinyumba mdada wa watu na raha wanakula alfajiri na usiku. yule bwana wake baada ya kushtukizia mpaka leo kapata stroke hata jina la rais wake "mwai kibaki" hawezi kulitamka. Muumba amponyeshe haraka(tusemeni amen)

...astaghafirullah, astaghafirullah, astaghafirullah!!!
yaani nimecheka wakati nasikitika. Klorokwini acha masihara bana...!

Khaaa? huyo mwanamke ibilisi mkubwa, ndugu wa mume wanamtizamaje?
duuuh, haki ya mungu kupenda mtihani wallah! ha ha ha....
 
Mwizi ni baba watoto wako; huyo bibie yeye kajikinga jua ama mvua hapo asa weye uko katika ya mvua kubwa ikatokea mssada wakuokolewa usilowane...................ku deal na huyo ni kumuonea haijalishi hata ukimkuta ndo anamkatikia cha mwisho!

wewe wasema!!!!
 
Pole sana bana.
Mapenzi na Ndoa ni PROMISES, zikishavunjwa sidhani hata AM SORRY kwa lugha yeyote inasaidia lolote.
Ngumu sana kusamehe, itakuwa kujisahaulisha?

ni hapo tu dear Mbu!!!! asante
 
...wewe bana weee, hebu achana na hizo dua mbaya bana. Kina mama wakileta jinsi wanavyotudanganya mbona ndoa nyingi zitavunjika wiki hii!... DNA results ni ushahidi tosha. Ukiambiwa siku ile ulipoharibu bajeti na kumpeleka salooni ndio siku mimba ilipotungwa si tutauana bure?

Kina mama, kwa hisani zenu msiseme mnavyotudanganya, Inauma sana.
Wanawake wameumbiwa ustahmilivu wa hali ya juu, ...sie mnh!?, bado kwanza.
hapa moskwito umeongea kweli tupu.
 
kuna mdada kenya alijitangazia redio ya kijijini kwamba katekwa nyara na jamaa anataka ransom ndio amuachie. khaaaa ! baada ya kufuatiliwa kumbe jamaa alikuwa kamuweka kinyumba mdada wa watu na raha wanakula alfajiri na usiku. yule bwana wake baada ya kushtukizia mpaka leo kapata stroke hata jina la rais wake "mwai kibaki" hawezi kulitamka. Muumba amponyeshe haraka(tusemeni amen)

haki ya nani klorokwini unanivunja mbavu...nipo kwenye majnzi mie na hii thread.
 
jamani tuache masihara, hii dhambi kweli inawgharimu watu hata maisha yao.............

ona sasa kama hivi!!!!

tena hii kitu bana ikishatokea, nothing will ever ever be the same again, hata ujidai eti nimekusamehe mi nadhani kuna vichembe chembeme vya hasira vitabaki moyoni mwa mtu aisee!!!
 
...astaghafirullah, astaghafirullah, astaghafirullah!!!
yaani nimecheka wakati nasikitika. Klorokwini acha masihara bana...!

Khaaa? huyo mwanamke ibilisi mkubwa, ndugu wa mume wanamtizamaje?
duuuh, haki ya mungu kupenda mtihani wallah! ha ha ha....
hii dunia ina tamsilia nyingi sana, ndio maana magazeti ya udaku yana profit kubwa kuliko nyumba za ibada. mimi nimeamua kuchukulia maisha kama joke flani ili angalau niishi mpaka kuota mvi bila heart attack.
 
ha ha ha mamushka naona move yake itakua kama ivi....

God, the Almighty, the Omnipotent, the All Knowing, the Incomparable...........aniepushe na hili!!!
 
hii dunia ina tamsilia nyingi sana, ndio maana magazeti ya udaku yana profit kubwa kuliko nyumba za ibada. mimi nimeamua kuchukulia maisha kama joke flani ili angalau niishi mpaka kuota mvi bila heart attack.

inabidi unishirikishe wangu........huu uzoefu nauhitaji sana!!!
 
...hehehe,...nyamayao unaniacha hoi na masahiba yaliyokupata maishani.
Anyway, kwa uzoefu wangu hapo uliposema "...mwenye kukuheshimu/kukupenda atatumia akili zake zote za ziada ucmbambe, unadhani kwanini watu hatuwabambi japo wanafanya" ndio tofauti waliyonayo Cheaters wanawake compared na Cheaters wanaume.

By the time unakuja gundua Mkeo aliku cheat, tayari jua lishakuchwa na hata nguvu ya ushahidi upande wa mashtaka hakuna tena.

Na ukiona cheater wa kike kaanika ambo ujue hakuheshimu keshaamua liwalo na liwe na hapo ndoa yenu haina mashiko tena kwani hata suala la kumfumania kwake linakuwa halimuumizi kichwa! Hatari sana!
 
haki ya nani klorokwini unanivunja mbavu...nipo kwenye majnzi mie na hii thread.
dah pole sana sis. sikujua kama na wewe umekuwa viktim wa hii sredi. lakini someni post za "mbu" zinaleta unafuu flani kidogo. hizi post za teamo na aspirin zinaweza zikapeleka kinadada wenye mioyo miepesi ICU.
 
hii dunia ina tamsilia nyingi sana, ndio maana magazeti ya udaku yana profit kubwa kuliko nyumba za ibada. mimi nimeamua kuchukulia maisha kama joke flani ili angalau niishi mpaka kuota mvi bila heart attack.

Thats the way!

Vinginevyo utajifia bure kwa michezo ya kitoto!
 
Back
Top Bottom