Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Inaonesha hata hujaisoma post yangu.
Kwaheri
Nimeisoma.
Ila nilikuwa najibu hoja ya Izrael pekee,
Kuhusu ufufuo siku ya kiyama, Wakristo wanajua wazi Kabisa aliyepewa jukumu la kufufua Watu siku za mwisho, ambaye ni Yesu Kristo, huku ndugu zao Waislam wakiwa gizani wakiamini kuwa kutakuwa na ufufuo lakini hawajui atakayefufua ni Nani.
Uislam unategemea zaidi Ukristo na uyahudi katika visa vyake. Kwa maana uislam umechukua visa vya wanawaisrael kama msingi Mkuu wa masimulizi yake.
Bila waisrael hakuna uislam, hata hivyo sio kosa dini moja kunukuu au kujenga msingi wake katika Dini zingine.
Hata katika kipengele cha ufufuo wa mara ya pili, uislam hauwezi kujitegemea wenyewe bila Ukristo Kwa sababu Kristo ndiye msingi Mkuu wa Ufufuo. Hiyo ndio maana halisi ya kitabu cha INJILI "yaani habari njema" kwamba Kristo amefufuka katika wafu na atakuja mara ya pili kufufua waliowake.
Uislam haumtambui Yesu Kama mhusika Mkuu katika Ufufuo wa kiyama n hapo ndipo nikasema hauamini na hauna tumaini la ufufuo Kwa wafu.
Huwezi sema kuwa unaamini katika ufufuo wa pili alafu muda huohuo haumuamini Kristo atakayefufua wafu.
Ni Sawa na Mtu ambaye anaamini katika uumbaji wa mwanadamu lakini haamini kuwa Adamu ndiye alikuwa mtu wa Kwanza kuumbwa.
Uislam haujui umuhimu wa kitabu cha Injili lakini muda huohuo unaamini katika Neema ya ufufuo wa wanadamu siku ya kiyama.