Matukio yanayoonesha uongo kwenye vitabu vya dini

Achana na ngonjera za dini, mungu hayupo.
Hakika wengi katika watu ni wenye kuzikufuru neema za Mola Mlezi ikiwemo wewe...

Wewe unafikiri Muumba aliuumba ulimwengu huu na kutuweka burebure tu, wafanye WEMA wafanyao au wafanye maovu wafanyao ndiyo iishie hapo tu!!! Au wote wawe sawa???!!!
 
Har
Kwa kukusaidia, angalau kupanua akili yako.

Sijui kama uliwahi kwenda shule ya juu, ungesoma somo la mantiki/logic.

Kwenye mantiki ama logic and reasoning jambo lile lile leo useme yes, kesho useme noo basi jibu ni no.

Hata kwenye hesabu, tulisoma true, true jibu ni true, true false jibu ni false.

Ikishatokea contradiction basi hapo hakuna ukweli, ni uongo. Kitu kilichonyooka hakina contradiction.

Ndio maana nikakushauri, rudi shule uongeze ufahamu zaidi ndio uje kujadili haya mambo boss.
Hata we pia nmegundua huna akili pia Sina zaodi, mantik/logic ulosoma kaisome zaid
 
Kwa kukusaidia, angalau kupanua akili yako.

Sijui kama uliwahi kwenda shule ya juu, ungesoma somo la mantiki/logic.

Kwenye mantiki ama logic and reasoning jambo lile lile leo useme yes, kesho useme noo basi jibu ni no.

Hata kwenye hesabu, tulisoma true, true jibu ni true, true false jibu ni false.

Ikishatokea contradiction basi hapo hakuna ukweli, ni uongo. Kitu kilichonyooka hakina contradiction.

Ndio maana nikakushauri, rudi shule uongeze ufahamu zaidi ndio uje kujadili haya mambo boss.
Only those with great minds can understand that, you just reminded me mathematics: "Double t (TT) is true otherwise is false (FT, TF, FF). BIG UP.
 
Mkuu evil Genius unavyoamini kuhusu wewe binafsi wewe ni evil genius au ni EVIL peke yake? Maana umejidhihirisha kwamba ni nini kilichojaa ndani ya nafsi Yako.
 
Tokea yesu anazaliwa mpake Leo ni miaka 2000, tokea ibrahimu mpaka YESU ni miaka 4200 bado upo

Dunia Ina miaka 2000 we ndo mjinga wa mwisho
hahahahaa umenichekesha sana mkuu kwamba yeye ndio mjinga wa mwisho hapa duniani
 
mkuu umeokoka maybe, au wewe ni mkamilifu sana maybe hadi kufikia kutaka kujua kuhusu Mungu, Mungu huwezi mjadili kwa akili ya kawaida ya kibinadamu ukapata majibu sahihi, uwezo wa kibinadamu una kiwango chake cha mwisho kama uwezo wa macho yako ulivyoishia kuona anga ni ya bluu
 
Kwavile uwezowako wakufikiri umeishia hapo hata ukifundishwa huwezi ukaelewa mana unajifunza kwa lengo la kumkataa Mungu. Ukisoma maandiko kwautakavyo wewe yatakupeleka hukohuko unakotaka ila ukitaka uongozwe na uweza was Mungu utafahamu. Hakuna point hata moja hapo kwa mtu anaetumia tu akili yakawaida iliyoko timamu
 
Matukio haya yanaonyesha kwamba dini imejaa uongo.

Tuanze na Biblia.
1. Biblia inasema mungu ni alpha na Omega, mwanzo na mwisho, ni yeye aliepo na ataendelea kuwepo. Kwa maana kwamba mungu ndio chanzo cha vitu vyote, hakuna kitu kilianza bila yeye. Mungu ni mjuzi wa kila kitu.

Tukiamini hivyo ni sawa, lakini tukienda mbele zaidi kutafakari, kama mungu anajua vyote, je alijua kama shetani atakuja kumuasi? Kama alijua ni kwa nini bado alimuumba?

2. Kama mungu aliamua tu kumuumba shetani pamoja na kujua kua atakuja kuasi, alikua na maana gani? Biblia inasema yeye ni mkamilifu, hakuna kitu kidhaifu/kibovu kinatoka kwake, sasa unajiuliza shetani alietoka kwake ni mbovu ama mzima ama mkamilifu?

Hapo jibu ni moja tu, mungu hakujua kama shetani atakuja kumuasi hivyo mungu hajui kila kitu.

3. Baada ya shetani kuasi na malaika zake, kwa maelezo ya biblia shetani alitupwa Duniani. Kwa maana kwamba Dunia haikua na kiumbe ila shetani alitupwa huku kukiwa ni empty.

Baadae mungu akamuumba binadamu na kumuweka Duniani. Kwa maana kwamba Adam amekuja Duniani tayari shetani yupo muda mrefu anakula maisha. So Adam kamkuta shetani Duniani.

4. Baada ya Adam kuletwa Duniani, hakuwahi kuambiwa kwamba kuna kiumbe mwingine anaeishi Duniani tofauti na yeye, so hakupewa tahadhari yoyote. Kwa maana nyingine aliachwa kua vulnerable kwa shetani kumshambulia. Swali, kwa nini mungu hakumuonya Adam kuhusu uwepo wa shetani Duniani? Kwa nini alikaa kimia, lengo lake ilikua nini?. Mbaya zaidi mungu hakumuonya shetani asimrubuni adam, so akaacha loop hole ya shetani kujifanyia anayoyataka, baada ya shetani kufanikiwa, lawama ni kwa Adam.

Tu-assume alipewa maelekezo kidogo, lakini alipewa yeye, hakuna maonyo aliyopewa Eva mke wa Adam ambae shetani alimtumia kama kichochoro, je hawa makosa yao ni nini?

Jibu: Mungu aliwaingiza kwenye mtego maksudi, kuanguka kwa adam ilikua ni maksudi ya mungu kutafta justification ya kumlaumu Adam.

5. Kati ya binadamu na malaika mungu anampenda nani zaidi. Biblia inasema shetani alikua malaika mkuu, alipoasi alipata baadhi ya malaika waliomuunga mkono. Maelezo mazuri kabisa.

Biblia inaenda mbali na kusema baada ya shetani na malaika zake kuasi mungu aliwatupa Duniani watatange take. Tunakubali sawa kabisa.

Swali, kati ya binadamu na malaika ni nani anamjua vizuri shetani? Jibu ni malaika kwa sababu wameumbwa pamoja, wameishi pamoja hivyo wanajuana vizuri.

Swali lingine, kwa akili ya kawaida, ni nani alipaswa kuletwa Duniani kupambana na shetani? Jibu, alipaswa iwe ni malaika kwa sababu wanamjua vizuri zaidi shetani kuliko binadamu. Kwa maana kwamba ingekua rahisi sana kwao kumkataa shetani mapema na akakosa wafuasi kwa sababu wanamjua.

Masikitiko ni kwamba, mungu hakutaka kuwaleta viumbe wake anaowapenda Duniani akaamua kuumba viumbe wengine ambao hawajui lolote na kuja kuwapambanisha na shetani ambae ana superiority knowledge kuliko wao.

Ni sawa na wewe una rungu unaenda kupigana na mtu ana mizinga, drones, fighter jets, na kila kitu halafu utegemee utashinda. Hiki ndio mungu alichoamua kuwafanyia binadamu.

B. Nitakuja kuelezea upande wa quran(huku ndio madudu yalikojaa). Mkitaka na vifungu nitaweka.
Maswali unayojiuliza huulizwa na kila mtu anapoanza kuwa na akili ya kujua jema na baya. Lakini unapotaka kuendelea kutafakari juu ya Mungu ni vema ukazingatia maandiko yafuatayo ya Biblia:

Andiko la kwanza: Kumbu. 29:29
"Mambo ya siri ni ya BWANA, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii."

Andiko la pili: 1 Kor 1:25
"Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu."

1. Tukitafakari Andiko la kwanza, tunakumbuka kwamba yapo mambo ambayo mzazi wako hawezi kukwambia yanabaki kuwa Siri yake milele. Kutokana na usiri wa baba Yako utakufanya wewe kuona mapungufu au udhaifu fulani kwake, au utakuwa na maswali yasiyo na majibu na inaweza kupelekea kumwona baba Yako mwongo. Lakini endapo angekushirikisha ukweli basi usingemwona mwongo.

Lakini yapo mambo ambayo baba hayaweka Siri mpaka muda mwafaka au mpaka atakapokuamini kwamba Sasa una akili za kiutu uzima au Sasa unaweza kuyabeba. Hata kama utamwonaje hatasema mpaka u meet viwango vyake.

Naamini kwamba kutomwelewa mzazi Kutokana na usiri wake hakumfanyi mzazi kuwa mwongo atabaki kuwa mkweli lakini katika akili ya mtoto ni mwongo. Kweli itabaki kuwa kweli bila kujali mazingira!

2. Katika Andiko letu la pili, mtoto kwa akili zake za kitoto anaweza kumwona baba hana akili au ni mpumbavu. Na kama baba atakuwa mpumbavu machoni pa mtoto basi ni mpumbavu kwa mtoto yule Kutokana na vigezo vya mtoto! Lakini katika uhalisia upumbavu ule wa baba Bado ni hekima iliyozidi sana maarifa au akili ya mtoto yule.

3. HITIMISHO
- Kuna mambo Mungu amekuficha, mwachie Yeye mwenyewe kwa kuwa Bado ameamua kufanya Siri yake. Wewe usi conclude kwamba ni mwongo kwa sababu tu huna majibu. MWAMINI MUNGU KWA SABABU BADO ANASTAHILI SANA KUANINIWA!

- Kuna mambo au tabia za Mungu huzielewi au haziingii akilini mwa akili Yako, kwa maneno mengine anamwona kuwa ni mpumbavu. Kumbuka ni Kutokana na levo ya utendaji kazi ya akili yako. MSOGELEE MUNGU AKUAMINI NA ATAKUSHIRIKISHA SIRI ZAKE NAWE UTAKUBALIANA NAYE VILIVYO!

# Wewe kwa hakika ni mtumishi wake Mungu, na MUNGU AKUBARIKI SANA!
 
Matukio haya yanaonyesha kwamba dini imejaa uongo.

Tuanze na Biblia.
1. Biblia inasema mungu ni alpha na Omega, mwanzo na mwisho, ni yeye aliepo na ataendelea kuwepo. Kwa maana kwamba mungu ndio chanzo cha vitu vyote, hakuna kitu kilianza bila yeye. Mungu ni mjuzi wa kila kitu.

Tukiamini hivyo ni sawa, lakini tukienda mbele zaidi kutafakari, kama mungu anajua vyote, je alijua kama shetani atakuja kumuasi? Kama alijua ni kwa nini bado alimuumba?

2. Kama mungu aliamua tu kumuumba shetani pamoja na kujua kua atakuja kuasi, alikua na maana gani? Biblia inasema yeye ni mkamilifu, hakuna kitu kidhaifu/kibovu kinatoka kwake, sasa unajiuliza shetani alietoka kwake ni mbovu ama mzima ama mkamilifu?

Hapo jibu ni moja tu, mungu hakujua kama shetani atakuja kumuasi hivyo mungu hajui kila kitu.

3. Baada ya shetani kuasi na malaika zake, kwa maelezo ya biblia shetani alitupwa Duniani. Kwa maana kwamba Dunia haikua na kiumbe ila shetani alitupwa huku kukiwa ni empty.

Baadae mungu akamuumba binadamu na kumuweka Duniani. Kwa maana kwamba Adam amekuja Duniani tayari shetani yupo muda mrefu anakula maisha. So Adam kamkuta shetani Duniani.

4. Baada ya Adam kuletwa Duniani, hakuwahi kuambiwa kwamba kuna kiumbe mwingine anaeishi Duniani tofauti na yeye, so hakupewa tahadhari yoyote. Kwa maana nyingine aliachwa kua vulnerable kwa shetani kumshambulia. Swali, kwa nini mungu hakumuonya Adam kuhusu uwepo wa shetani Duniani? Kwa nini alikaa kimia, lengo lake ilikua nini?. Mbaya zaidi mungu hakumuonya shetani asimrubuni adam, so akaacha loop hole ya shetani kujifanyia anayoyataka, baada ya shetani kufanikiwa, lawama ni kwa Adam.

Tu-assume alipewa maelekezo kidogo, lakini alipewa yeye, hakuna maonyo aliyopewa Eva mke wa Adam ambae shetani alimtumia kama kichochoro, je hawa makosa yao ni nini?

Jibu: Mungu aliwaingiza kwenye mtego maksudi, kuanguka kwa adam ilikua ni maksudi ya mungu kutafta justification ya kumlaumu Adam.

5. Kati ya binadamu na malaika mungu anampenda nani zaidi. Biblia inasema shetani alikua malaika mkuu, alipoasi alipata baadhi ya malaika waliomuunga mkono. Maelezo mazuri kabisa.

Biblia inaenda mbali na kusema baada ya shetani na malaika zake kuasi mungu aliwatupa Duniani watatange take. Tunakubali sawa kabisa.

Swali, kati ya binadamu na malaika ni nani anamjua vizuri shetani? Jibu ni malaika kwa sababu wameumbwa pamoja, wameishi pamoja hivyo wanajuana vizuri.

Swali lingine, kwa akili ya kawaida, ni nani alipaswa kuletwa Duniani kupambana na shetani? Jibu, alipaswa iwe ni malaika kwa sababu wanamjua vizuri zaidi shetani kuliko binadamu. Kwa maana kwamba ingekua rahisi sana kwao kumkataa shetani mapema na akakosa wafuasi kwa sababu wanamjua.

Masikitiko ni kwamba, mungu hakutaka kuwaleta viumbe wake anaowapenda Duniani akaamua kuumba viumbe wengine ambao hawajui lolote na kuja kuwapambanisha na shetani ambae ana superiority knowledge kuliko wao.

Ni sawa na wewe una rungu unaenda kupigana na mtu ana mizinga, drones, fighter jets, na kila kitu halafu utegemee utashinda. Hiki ndio mungu alichoamua kuwafanyia binadamu.

B. Nitakuja kuelezea upande wa quran(huku ndio madudu yalikojaa). Mkitaka na vifungu nitaweka.
KUMBUKA
Ni kawaida kwa mtoto akili ikianza kukua anaanza kujiuliza mambo mengi na kufikia conclusion kulingana na uwezo ambao akili yake imefikia!

Lakini haimaanishi kwamba yupo sahihi au hayupo sahihi, au alichokigundua ndio Ukweli Sasa au la.

Na kwa kuwa kweli haibadiliki, akili ya mtoto lazima iambatane na ile kweli.
 
Matukio haya yanaonyesha kwamba dini imejaa uongo.

Tuanze na Biblia.
1. Biblia inasema mungu ni alpha na Omega, mwanzo na mwisho, ni yeye aliepo na ataendelea kuwepo. Kwa maana kwamba mungu ndio chanzo cha vitu vyote, hakuna kitu kilianza bila yeye. Mungu ni mjuzi wa kila kitu.

Tukiamini hivyo ni sawa, lakini tukienda mbele zaidi kutafakari, kama mungu anajua vyote, je alijua kama shetani atakuja kumuasi? Kama alijua ni kwa nini bado alimuumba?

2. Kama mungu aliamua tu kumuumba shetani pamoja na kujua kua atakuja kuasi, alikua na maana gani? Biblia inasema yeye ni mkamilifu, hakuna kitu kidhaifu/kibovu kinatoka kwake, sasa unajiuliza shetani alietoka kwake ni mbovu ama mzima ama mkamilifu?

Hapo jibu ni moja tu, mungu hakujua kama shetani atakuja kumuasi hivyo mungu hajui kila kitu.

3. Baada ya shetani kuasi na malaika zake, kwa maelezo ya biblia shetani alitupwa Duniani. Kwa maana kwamba Dunia haikua na kiumbe ila shetani alitupwa huku kukiwa ni empty.

Baadae mungu akamuumba binadamu na kumuweka Duniani. Kwa maana kwamba Adam amekuja Duniani tayari shetani yupo muda mrefu anakula maisha. So Adam kamkuta shetani Duniani.

4. Baada ya Adam kuletwa Duniani, hakuwahi kuambiwa kwamba kuna kiumbe mwingine anaeishi Duniani tofauti na yeye, so hakupewa tahadhari yoyote. Kwa maana nyingine aliachwa kua vulnerable kwa shetani kumshambulia. Swali, kwa nini mungu hakumuonya Adam kuhusu uwepo wa shetani Duniani? Kwa nini alikaa kimia, lengo lake ilikua nini?. Mbaya zaidi mungu hakumuonya shetani asimrubuni adam, so akaacha loop hole ya shetani kujifanyia anayoyataka, baada ya shetani kufanikiwa, lawama ni kwa Adam.

Tu-assume alipewa maelekezo kidogo, lakini alipewa yeye, hakuna maonyo aliyopewa Eva mke wa Adam ambae shetani alimtumia kama kichochoro, je hawa makosa yao ni nini?

Jibu: Mungu aliwaingiza kwenye mtego maksudi, kuanguka kwa adam ilikua ni maksudi ya mungu kutafta justification ya kumlaumu Adam.

5. Kati ya binadamu na malaika mungu anampenda nani zaidi. Biblia inasema shetani alikua malaika mkuu, alipoasi alipata baadhi ya malaika waliomuunga mkono. Maelezo mazuri kabisa.

Biblia inaenda mbali na kusema baada ya shetani na malaika zake kuasi mungu aliwatupa Duniani watatange take. Tunakubali sawa kabisa.

Swali, kati ya binadamu na malaika ni nani anamjua vizuri shetani? Jibu ni malaika kwa sababu wameumbwa pamoja, wameishi pamoja hivyo wanajuana vizuri.

Swali lingine, kwa akili ya kawaida, ni nani alipaswa kuletwa Duniani kupambana na shetani? Jibu, alipaswa iwe ni malaika kwa sababu wanamjua vizuri zaidi shetani kuliko binadamu. Kwa maana kwamba ingekua rahisi sana kwao kumkataa shetani mapema na akakosa wafuasi kwa sababu wanamjua.

Masikitiko ni kwamba, mungu hakutaka kuwaleta viumbe wake anaowapenda Duniani akaamua kuumba viumbe wengine ambao hawajui lolote na kuja kuwapambanisha na shetani ambae ana superiority knowledge kuliko wao.

Ni sawa na wewe una rungu unaenda kupigana na mtu ana mizinga, drones, fighter jets, na kila kitu halafu utegemee utashinda. Hiki ndio mungu alichoamua kuwafanyia binadamu.

B. Nitakuja kuelezea upande wa quran(huku ndio madudu yalikojaa). Mkitaka na vifungu nitaweka.
Kuhusu Quran mkuu, nadhani unataka JF ichomwe moto 😂😂 maana wavaa kobazi huwa hawataki reasoning
 
Nilivyoona umeweka picha ya NAPE tu nikaishia hapo
 
Ndio maana nikakuambia Wewe bado mchanga.

Ukiwa Darasa la Kwanza ulifundishwa 1-2 jibu ni haiwezekani.
Lakini sasa hivi 1-2 jibu sio haiwezekani Bali ni -1.
Kitu kikikupa mkanganyiko maana yake sio kwamba ni uongo Bali ni Akili yako ni ndogo kukielewa Kwa urahisi.

Kwenye Logic kama ulivyoeleza
True+ True = True
True+ False = False
False + True = False
False + False = False

Sasa yote uliyoyaeleza hakuna uongo wowote hapo.
Ungeomba utatuliwe hiyo kilichokupa mkanganyiko
Misuli imetoshana[emoji725]
 
Mtoa post umeandika kitu cha maana sana tatizo ni kwamba,watu wanaongozwa na mapenzi au hisia (love and emotion) badala ya logic
Mimi ni Mkristo ninayeamini kuwa yupo Mungu ambaye ndiye Alpha na Omega (the existence of the Supreme Being) lakini,ukitumia logic unaona kuna kitu hakiko sawa

NB😀ini haihitaji logic bali inahitaji kuamini (imani ni hakika ya mambo yatarajiwayo) ukitumia logic au akili kwenye dini lazima wewe na dini mtofautiane!
Hapa nimeona kitu ngoja tuone
 
Unfortunately wengi tunaishi kwa masimulizi ya kuambiwa Biblia na Qur'an ni TOFAUTI sana ikiwa akili yako imetulia: So sad....

Naomba nikupe mifano miepesi:

1. Nabii wa Allah Ibrahim kwenye bibilia anatuhumia kwa Uzinzi LAKINI Nabii huyu kwenye Qur'an amesimuliwa akiwa na Uchamungu wa Hali ya juu mpaka anafikia kuitwa Rafiki wa Mola Mlezi

2. Ukisoma Bibilia utamkuta Nabii wa Allah Nuhu akiwa ni shujaa aliyewaokoa watu na Gharika lakini baadaye akawa Mlevi wa kutupwa [Alcoholic] TOFAUTI kabisa na kwenye Qur'an

3. Nabii wa Allah Luti anaonekana akiwaokoa baadhi ya wafuasi wake na gharika ya sodoma na gomora lakini bibilia hiyohiyo inatueleza baadaye akazini na binti zake LAKINI Nabii huyu kwenye Qur'an qnasimuliwa akiwa ni mchamungu na wakupigiwa mfano na ummah wake

5. Nabii wa Allah Daud anasimuliwa kama kamanda aliyeshinda vita [kumshinda goliati] lakini bibilia hiyo hiyo inatuambia baadaye akazini na mke wa kamanda wake na kumua mwenye mke.... Nabii huyu kwenye Qur'an anasimuliwa ni mwema na mwenye kupigiwa mfano na ummah wake..

5. Nabii wa Allah Iysah AMA YESU anavyosimuliwa kwenye bibilia YEYE pamoja na mama yake na WANAVYOSIMULIWA KWENYE QUR'AN ni TOFAUTI..

6. Lakini matukio kama la YUSUF na ndugu zake linavyosimuliwa kwenye bibilia ni kama kuungaunga LAKINI lilivyosimuliwa kwenye QUR'AN ni very clear [rejea SURATUL YUSUF]

Kwa kifupi wengi wa wakiristo hawasomi vitabu vyao hasa Bibilia wanaishi kwa mistari miwili mitatu ya kuambiwa TOFAUTI na imani ya Kiislam iliyojenga kwenye MSINGI wa elimu...

Nimesoma sana bibilia lakini haijawahi kunibariki kama nilivyopata nafasi ya kusoma Qur'an
Yaani wewe nae sijui unaongea nini!Unapataje uthubutu wa kuikosoa biblia wakati mtume wako anakuambia ukitaka kuyajua zaidi mambo ya kina nuhu na lutu uwaulize wasomi wa biblia!Kwa akili yako unaona quran ipo clear sana sio?Nikupe challenge kdg;imani yako inakuambia hakuna binadamu aliyetakasika na dhambi isipokuwa Yesu.Nuhu alikuwa mwanadamu,unaamini hakuwahi kukosea ktk maisha yake?Kama hakuwahi basi alikuwa sawa na MUNGU,na kama alikosea basi biblia imeweka hadharani mapungufu yake ili sisi tulio hai leo tupate funzo.Quran haikueleza hata dhaifu moja la nabii yeyote,unataka useme hawakuwahi kufanya makosa ktk maisha yao?
 
Matukio haya yanaonyesha kwamba dini imejaa uongo.

Tuanze na Biblia.
1. Biblia inasema mungu ni alpha na Omega, mwanzo na mwisho, ni yeye aliepo na ataendelea kuwepo. Kwa maana kwamba mungu ndio chanzo cha vitu vyote, hakuna kitu kilianza bila yeye. Mungu ni mjuzi wa kila kitu.

Tukiamini hivyo ni sawa, lakini tukienda mbele zaidi kutafakari, kama mungu anajua vyote, je alijua kama shetani atakuja kumuasi? Kama alijua ni kwa nini bado alimuumba?

2. Kama mungu aliamua tu kumuumba shetani pamoja na kujua kua atakuja kuasi, alikua na maana gani? Biblia inasema yeye ni mkamilifu, hakuna kitu kidhaifu/kibovu kinatoka kwake, sasa unajiuliza shetani alietoka kwake ni mbovu ama mzima ama mkamilifu?

Hapo jibu ni moja tu, mungu hakujua kama shetani atakuja kumuasi hivyo mungu hajui kila kitu.

3. Baada ya shetani kuasi na malaika zake, kwa maelezo ya biblia shetani alitupwa Duniani. Kwa maana kwamba Dunia haikua na kiumbe ila shetani alitupwa huku kukiwa ni empty.

Baadae mungu akamuumba binadamu na kumuweka Duniani. Kwa maana kwamba Adam amekuja Duniani tayari shetani yupo muda mrefu anakula maisha. So Adam kamkuta shetani Duniani.

4. Baada ya Adam kuletwa Duniani, hakuwahi kuambiwa kwamba kuna kiumbe mwingine anaeishi Duniani tofauti na yeye, so hakupewa tahadhari yoyote. Kwa maana nyingine aliachwa kua vulnerable kwa shetani kumshambulia. Swali, kwa nini mungu hakumuonya Adam kuhusu uwepo wa shetani Duniani? Kwa nini alikaa kimia, lengo lake ilikua nini?. Mbaya zaidi mungu hakumuonya shetani asimrubuni adam, so akaacha loop hole ya shetani kujifanyia anayoyataka, baada ya shetani kufanikiwa, lawama ni kwa Adam.

Tu-assume alipewa maelekezo kidogo, lakini alipewa yeye, hakuna maonyo aliyopewa Eva mke wa Adam ambae shetani alimtumia kama kichochoro, je hawa makosa yao ni nini?

Jibu: Mungu aliwaingiza kwenye mtego maksudi, kuanguka kwa adam ilikua ni maksudi ya mungu kutafta justification ya kumlaumu Adam.

5. Kati ya binadamu na malaika mungu anampenda nani zaidi. Biblia inasema shetani alikua malaika mkuu, alipoasi alipata baadhi ya malaika waliomuunga mkono. Maelezo mazuri kabisa.

Biblia inaenda mbali na kusema baada ya shetani na malaika zake kuasi mungu aliwatupa Duniani watatange take. Tunakubali sawa kabisa.

Swali, kati ya binadamu na malaika ni nani anamjua vizuri shetani? Jibu ni malaika kwa sababu wameumbwa pamoja, wameishi pamoja hivyo wanajuana vizuri.

Swali lingine, kwa akili ya kawaida, ni nani alipaswa kuletwa Duniani kupambana na shetani? Jibu, alipaswa iwe ni malaika kwa sababu wanamjua vizuri zaidi shetani kuliko binadamu. Kwa maana kwamba ingekua rahisi sana kwao kumkataa shetani mapema na akakosa wafuasi kwa sababu wanamjua.

Masikitiko ni kwamba, mungu hakutaka kuwaleta viumbe wake anaowapenda Duniani akaamua kuumba viumbe wengine ambao hawajui lolote na kuja kuwapambanisha na shetani ambae ana superiority knowledge kuliko wao.

Ni sawa na wewe una rungu unaenda kupigana na mtu ana mizinga, drones, fighter jets, na kila kitu halafu utegemee utashinda. Hiki ndio mungu alichoamua kuwafanyia binadamu.

B. Nitakuja kuelezea upande wa quran(huku ndio madudu yalikojaa). Mkitaka na vifungu nitaweka.
Matukio haya yanaonyesha kwamba dini imejaa uongo.

Nimesoma kwa masikitiko makubwa hoja DHAIFU alizojaribu kuibua mleta mada kujaribu kushawishi kuwa hakuna Mungu. Kama ukisoma kwa umakini kidogo tu utabaini kwamba mleta mada ana ufinyu wa uelewa na kwamba kwa kiasi kikubwa hoja zake zimejengwa kwa kile alichokisikia na sio kile anachokielewa kwa kufanya tafakari binafsi.

Hoja ya awali kabisa ni pale anapodai kwamba dini ni uongo, halafu anajaribu kuelezea maandiko (hakutoa nukuu ama rejea yoyote) kama yalivyo kwenye Biblia Takatifu kutetea pingamizi lake dhidi ya Ukristo. Ni vema kukujulisha kuwa hakuna mahali maandiko yamedai kuwa Ukristo ni dini!! YHWH hakuwahi kuanzisha dini, bali wanadamu walijaribu kujitengenezea mfumo wa dini kama njia ya kutafuta uhusiano na Mungu. Kwa kufanya hivyo wako waliokutana na YHWH aliye Mungu wa kweli na kuijua kweli hivyo kuishi sawa sawa na maagizo yake. Lakini pia wako wengine ambao waliangukia kwenye himaya za miungu (ndizo roho zidanganyazo) wakapewa mfumo wa kipepo kusudi waiabudu miungu hiyo ya uongo ambayo kiasili si Mungu.

Kumbe kule kusema dini ni uongo yaweza kuwa kweli kabisa kutegemea na aina ya mfumo wa kidini aliokutana nao mwandishi. Kumbuka dini si mfumo wa Mungu kwa ajili ya mwanadamu bali ni mfumo wa mwanadamu ili kumtafuta Mungu. Ukiongelea maandiko, Mungu ni mwanzilishi wa IMANI, sio dini:

Waebrania 12 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
² tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ......

Kwa hiyo hoja zako zijengwe kwa kuzingatia imani sio dini, kwani dini ina taratibu nyingi za kibinadamu ambazo sio maagizo ya Mungu.

Sasa tuzitazame hoja zilizowekwa jukwaani:

Tuanze na Biblia.
1. Biblia inasema mungu ni alpha na Omega, mwanzo na mwisho, ni yeye aliepo na ataendelea kuwepo. Kwa maana kwamba mungu ndio chanzo cha vitu vyote, hakuna kitu kilianza bila yeye. Mungu ni mjuzi wa kila kitu.

Tukiamini hivyo ni sawa, lakini tukienda mbele zaidi kutafakari, kama mungu anajua vyote, je alijua kama shetani atakuja kumuasi? Kama alijua ni kwa nini bado alimuumba?

2. Kama mungu aliamua tu kumuumba shetani pamoja na kujua kua atakuja kuasi, alikua na maana gani? Biblia inasema yeye ni mkamilifu, hakuna kitu kidhaifu/kibovu kinatoka kwake, sasa unajiuliza shetani alietoka kwake ni mbovu ama mzima ama mkamilifu?

Hapo jibu ni moja tu, mungu hakujua kama shetani atakuja kumuasi hivyo mungu hajui kila kitu.

Ni kweli maandiko yanasema Mungu ni ALPHA na OMEGA, yaani mwanzo na mwisho wa kila kitu:

Ufunuo wa Yohana 1 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁸ Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.

Kwa hiyo vitu vyote vimo kwenye mamlaka yake, naye ajua mwanzo na mwisho wa kila kitu. Kuhusu hoja yako kwamba kwa nini basi alimuumba shetani kama alijua kwamba ataasi. Pasipokuwa na msingi wa maandiko kupitia tafakari huwezi kamwe kuyaelewa maandiko wala kusudi la Mungu katika uumbaji wake.

Katika sifa kuu alizonazo Mwenyezi Mungu ni kwamba Yeye si kigeugeu, habadili kusudi lake. Ndipo akasema hulituma neno lake nalo halirejei mpaka limetimiza mapenzi yake:

Isaya 55 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁸ Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.
⁹ Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.

Mwanadamu hawezi kuwa na mawazo kama Mungu, hata kufikiri kwetu hakuwezi kutupa majibu yoyote kumhusu Mwenyezi Mungu. Mungu ni Roho, kutafakari kwetu ni kwa jinsi ya mwili, ndio maana ukitaka kumjua Mungu imekupasa kutafakari kwa kuongozwa na Roho wa Mungu. Huyo ndiye hutuonyesha Baba, sio kutumia logic mfu kwa jinsi ya mwili kama ulivyofanya humu.

¹⁰ Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;
¹¹ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.

Mungu akilituma neno lake (ndio mawazo yake) halirudi hivi hivi bali ni lazima litekeleze kile alicholikusudia. Ndio maana MUNGU NI MWAMINIFU. Tunaamini pale anaposema anatusamehe dhambi zetu na kutuepusha na adhabu ya milele. Mungu wetu si kigeugeu. Sasa hii ni hoja ya msingi katika kujibu swali lako.

Mungu alijua yote hata kabla ya uumbaji, kwamba shetani ataasi, mwanadamu ataasi na dunia itakwisha vipi. Lakini kama tulivyoona, Yeye ni mwaminifu kwa neno lake. Pale aliposema niumbe viumbe wa kiroho alitazama tangu kuumbwa kwao mpaka mwisho wao kabla hajawaumba. Lakini kwa kuwa Yeye ni mwaminifu hakutaka tena kubadili nia eti kwa vile ameona shetani ataasi basi aahirishe uumbaji, hii ingeondoa sifa yake muhimu ya kuwa AMINI na hivyo hata sisi tusingemwamini kwamba anavyosema atatupatia uzima wa milele ni kweli atafanya, kwani anaweza kubadili mawazo kama alivyobadili kwenye uumbaji.
Tazama fungu hili ujifunze ni kwa vipi Mungu alijua yote kabla ya kuumba:

Isaya 46 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁹ kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi;
¹⁰nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.

Mungu hutangaza mwisho kabla ya mwanzo, hutazama jinsi kiumbe kitakavyoanza mpaka pale kitakapoishia. Tena akisema neno lake ni LAZIMA LITIMIE. Kwa hiyo Mungu alijua yote, jinsi gani shetani atakavyoasi, atakavyoshawishi baadhi ya malaika, atakavyowashawishi na binadamu nk. Lakini kwa kuwa wazo lake la msingi tayari lilikuwa ni kuumba viumbe wenye sifa alizokusudia, hakutaka kughairi, kwani Yeye ni AMINI. Hebu tazama hapa kuumbwa kwa mwanadamu jinsi Mungu alivyojua tangu mwanzo:

Zaburi 139 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁴ Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,
¹⁵ Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi;
¹⁶ Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.

Umeona? Kumbe Mungu alizijua siku za mwanadamu, maisha yake, kila mmoja wetu kabla hata hajatungwa tumboni mwa mama yake bado. Kuna baadhi hapa hupenda kupotosha kuwa kumbe maisha yetu yameandikwa ama kupangwa na Mungu, kwa nini basi atuadhibu kwa kuishi vile alivyotupangia? Kwamba wengine wamepangiwa kuwa wazinzi, wengine walevi, watukanaji, wafiraji nk? Ukweli ni kuwa HAKUNA andiko hata moja lisemalo hayo. Mungu ameshatazama maisha ya viumbe wake wote jinsi watakavyoishi mpaka kufa kwao, sio kwamba ameshawapangia, bali anajua tayari nani atamtii na nani atamuasi. Hayo yapo tayari kwenye kumbukumbu zake hata kabla hatujazaliwa, lakini Yeye huvifanya vyote katika ukamilifu.

3. Baada ya shetani kuasi na malaika zake, kwa maelezo ya biblia shetani alitupwa Duniani. Kwa maana kwamba Dunia haikua na kiumbe ila shetani alitupwa huku kukiwa ni empty.

Baadae mungu akamuumba binadamu na kumuweka Duniani. Kwa maana kwamba Adam amekuja Duniani tayari shetani yupo muda mrefu anakula maisha. So Adam kamkuta shetani Duniani.

4. Baada ya Adam kuletwa Duniani, hakuwahi kuambiwa kwamba kuna kiumbe mwingine anaeishi Duniani tofauti na yeye, so hakupewa tahadhari yoyote. Kwa maana nyingine aliachwa kua vulnerable kwa shetani kumshambulia. Swali, kwa nini mungu hakumuonya Adam kuhusu uwepo wa shetani Duniani? Kwa nini alikaa kimia, lengo lake ilikua nini?. Mbaya zaidi mungu hakumuonya shetani asimrubuni adam, so akaacha loop hole ya shetani kujifanyia anayoyataka, baada ya shetani kufanikiwa, lawama ni kwa Adam.

Tu-assume alipewa maelekezo kidogo, lakini alipewa yeye, hakuna maonyo aliyopewa Eva mke wa Adam ambae shetani alimtumia kama kichochoro, je hawa makosa yao ni nini?

Jibu: Mungu aliwaingiza kwenye mtego maksudi, kuanguka kwa adam ilikua ni maksudi ya mungu kutafta justification ya kumlaumu Adam.

Kwanza kabisa ni UONGO MKUU kudai kuwa Mungu alimuumba mwanadamu kama jeshi lake la kupambana na shetani. Hili halikuwa kusudi la Mungu. Baada ya kuumba viumbe visivyoonekana kwanza, Mungu alikusudia kuumba viumbe vinavyoonekana pia, ndipo mwanadamu akaumbwa kwa mfumo tofauti na malaika. Malaika hawana mwili lakini binadamu ana mwili wa nyama. Tofauti hii ni muhimu mno kwani mwili ndio unaompatia mwanadamu uwezo wa kuishi duniani, lakini pale unapoondoka hurudi kuwa kiumbe cha kiroho kwani roho haifi. Mwanadamu anaporudi katika roho hupewa mwili maalum ambao sio tena kama huu ulioharibika kwa dhambi hivyo kuzeeka na kufa. Mwili mpya ni sawa kabisa na ule alioumbwa nao Adam kabla ya kuasi.

Sasa tujiulize, je Mungu hakuwapa maelekezo ya kutosha Adam na Hawa?

Mwanzo 1 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²⁶ Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
²⁷ Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
²⁸ Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
²⁹ Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;
³⁰ na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.
³¹ Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.

Mungu alitoa maagizo yake kwa kiumbe wake. Kuna neno moja usilofahamu kuhusu Mungu, ni kwamba kwa sababu ya utakatifu wake kila kiumbe chake kinaanza na huo utakatifu wakati wa kuumbwa kwake. Mungu ni nuru, hawezi kutoa maelekezo ya giza kwa viumbe wake, hivyo aliwaeleza jinsi ya kuishi bustanini kwa ajili ya mema tu. Katazo alilotoa ndilo lilikuwa msingi wa dhambi, kwamba wasile tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Kama nilivyosema mwanzoni, Mungu hakumuumba mwanadamu ili amsaidie kumpiga shetani, bali aishi kwa kufuata maelekezo yake, ndio kumwabudu. Hapa sijaelewa wewe ungependa kwa hekima zako wapewe maelekezo gani hasa?

Mwanzo 2 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁶ Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
¹⁷ walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Umeona? Mungu alijua mbinu atakayotumia shetani naye kuhusu matunda ya huo mti, ndipo akamuonya mbele kwamba USILE. Kwamba alikula hilo ni kosa la mwanadamu, sio kwa kuwa hakuonywa, bali alichagua kumuasi muumba. Pia shetani alimdanganya, si kwa sababu mwanadamu hakujua kama kuna shetani:

Mwanzo 3 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu.....

Kumbe roho ya shetani ilikuwa ikitenda kazi kupitia nyoka ambaye alikuwa humo bustanini. Kitendo cha Hawa kupiga stori na nyoka ni ishara tosha kuwa walifahamu fika uwepo wa shetani mle bustanini, bali muhimu ni kwamba walipaswa kuisikiliza sauti ya Mungu (wasile tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya) basi. Kwa nini basi Hawa akachagua kuisikiliza sauti ya nyoka ambaye naye ni kiumbe tu? Kwa nini kumlaumu Mungu kwa kutokutii kwao?

Kwamba Hawa hakupewa maelekezo yoyote!!! Hii nayo ni kutokuelewa maandiko. Hawa alichukuliwa kutoka Adam, wala Mungu hakuumba roho mpya ndani ya Hawa. Hivyo sauti ya Mungu ilikuwa kwenye roho ya Hawa kama ilivyokuwa kwa Adam. Hii ikifundishe jambo moja, sisi tuaminio tunaposema kuwa huzungumza na Mungu ni kwamba ametupa uwezo wa kuisikia sauti yake katika ROHO, sio physically tu. Tunazungumzia naye kabisa katika roho, na hili haliwezekani kulithibitisha kwa wasiotaka kuingia katika roho, watabaki vipofu na viziwi wa kiroho kama walivyozaliwa na mama zao. Wewe pia ni kipofu na kiziwi wa roho.

Hivyo kile alichokijua Adam ndicho hicho hicho alichokijua Hawa:

Mwanzo 5 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;
² mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.

Kumbe Adam (roho yake) ilikuwa pamoja na Hawa siku ya kuumbwa kwao, isipokuwa mwili wa Hawa ulikuwa haujaumbwa bado kutoka Adam. Nadhani umeelewa vema sasa.

5. Kati ya binadamu na malaika mungu anampenda nani zaidi. Biblia inasema shetani alikua malaika mkuu, alipoasi alipata baadhi ya malaika waliomuunga mkono. Maelezo mazuri kabisa.

Biblia inaenda mbali na kusema baada ya shetani na malaika zake kuasi mungu aliwatupa Duniani watatange take. Tunakubali sawa kabisa.

Swali, kati ya binadamu na malaika ni nani anamjua vizuri shetani? Jibu ni malaika kwa sababu wameumbwa pamoja, wameishi pamoja hivyo wanajuana vizuri.

Swali lingine, kwa akili ya kawaida, ni nani alipaswa kuletwa Duniani kupambana na shetani? Jibu, alipaswa iwe ni malaika kwa sababu wanamjua vizuri zaidi shetani kuliko binadamu. Kwa maana kwamba ingekua rahisi sana kwao kumkataa shetani mapema na akakosa wafuasi kwa sababu wanamjua.

Masikitiko ni kwamba, mungu hakutaka kuwaleta viumbe wake anaowapenda Duniani akaamua kuumba viumbe wengine ambao hawajui lolote na kuja kuwapambanisha na shetani ambae ana superiority knowledge kuliko wao.

Ni sawa na wewe una rungu unaenda kupigana na mtu ana mizinga, drones, fighter jets, na kila kitu halafu utegemee utashinda. Hiki ndio mungu alichoamua kuwafanyia binadamu.

Swali kwamba Mungu ampenda nani kati ya binadamu na malaika jibu ni kwamba anawapenda VIUMBE WAKE WOTE!! Ndio maana baada ya uumbaji aliona kila kitu tazama ni CHEMA SANA. Hakukuwa na chema kupita kingine, huo ni mtazamo wako wa kibinadamu.

Kwamba Mungu alimtupa shetani na malaika zake watangetange duniani, fahamu kuwa kutangatanga kwao hakukutokana na kuadhibiwa hivyo, bali kulitokana na kutokuwa na nafasi mbinguni. Kumbuka malaika waliumbwa kwa ajili ya kuishi mbinguni (viumbe wa kiroho kwenye ulimwengu wa roho). Sasa walipofukuzwa huko kwenye domain yao, ulitarajia wangeweza vipi kuishi kwenye dunia ya wenye mwili? Ndio maana shetani alivaa MWILI WA NYOKA bustanini ili kuteta na Eva. Shetani hana makao duniani, hakuumbwa kwa ajili ya kuishi huku, dunia ni kwa ajili ya wenye mwili tu, lakini pia hana makao mbinguni kwa sababu alifukuzwa huko. Ndipo akaangukia kwenye mbingu ya pili na kufanya utawala wake unaoiathiri dunia yetu. Hushuka huku duniani na kutangatanga akili tafuta mtu dhaifu katika Bwana kama wewe na kumfanya kuwa mbaya zaidi.

Kwamba ni nani anayemjua vizuri shetani kati ya mwanadamu na malaika? Jibu ni Mungu, malaika na wanadamu ni viumbe tu, wala hayuko amjuae vema mwenzake, ndio maana hatuna mamlaka ya kuhukumu kwa sababu hatuna tulijualo zaidi ya kile tukionacho. Kumbuka mwanadamu hakuletwa duniani ili apambane na shetani, hili halipo kabisa na ulifute kuanzia sasa.

Kusema kuwa malaika ndio wangeshushwa kupambana na shetani pia ni uzushi mkubwa. Malaika hawakuumbwa kuishi duniani (hawana miili), bali shetani ametupwa toka mahali pake, ndio maana maandiko yanasema anatangatanga duniani, hana makao maalumu mpaka apate mwili wa wana wa uasi kama ilivyo kwako hivi sana, anavyojaribu kukutumia lakini neno la Kristo litamchakaza kwani giza halitoweza kuishinda nuru, haleluya!!

Mwanadamu alipewa mwili maalum wa kuweza kuishi kwa raha na amani bila jasho hapa duniani, tena bila kuhofia shetani wala viumbe wengine ndio maana akapewa kuwatawala wote. Lakini pale alipoyakana mamlaka yake kwa kumsikiliza nyoka alupoteza mwili huu wa utukufu ulioneba mamlaka yote duniani na kuuvaa mwili wa kufa. Hivyo tangu kuumbwa kwake mwanadamu ana nguvu na mamlaka kumshinda shetani na malaika zake. Ndivyo inavyokuwa kwa wale waaminio kweli kweli, wanapokea tena mamlaka katika Yesu Kristo kuweza kuzisambaratisha ngome za shetani.

Habari za mizinga sijui fighters ni ufinyu wa elimu ya kiroho, hebu ona hapa:

Waefeso 6 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹¹
Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
¹² Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
¹³ Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
¹⁴ Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
¹⁵ na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
¹⁶ zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
¹⁷ Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
¹⁸ kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;

AMINA
 
Matukio haya yanaonyesha kwamba dini imejaa uongo.

Tuanze na Biblia.
1. Biblia inasema mungu ni alpha na Omega, mwanzo na mwisho, ni yeye aliepo na ataendelea kuwepo. Kwa maana kwamba mungu ndio chanzo cha vitu vyote, hakuna kitu kilianza bila yeye. Mungu ni mjuzi wa kila kitu.

Tukiamini hivyo ni sawa, lakini tukienda mbele zaidi kutafakari, kama mungu anajua vyote, je alijua kama shetani atakuja kumuasi? Kama alijua ni kwa nini bado alimuumba?

2. Kama mungu aliamua tu kumuumba shetani pamoja na kujua kua atakuja kuasi, alikua na maana gani? Biblia inasema yeye ni mkamilifu, hakuna kitu kidhaifu/kibovu kinatoka kwake, sasa unajiuliza shetani alietoka kwake ni mbovu ama mzima ama mkamilifu?

Hapo jibu ni moja tu, mungu hakujua kama shetani atakuja kumuasi hivyo mungu hajui kila kitu.

3. Baada ya shetani kuasi na malaika zake, kwa maelezo ya biblia shetani alitupwa Duniani. Kwa maana kwamba Dunia haikua na kiumbe ila shetani alitupwa huku kukiwa ni empty.

Baadae mungu akamuumba binadamu na kumuweka Duniani. Kwa maana kwamba Adam amekuja Duniani tayari shetani yupo muda mrefu anakula maisha. So Adam kamkuta shetani Duniani.

4. Baada ya Adam kuletwa Duniani, hakuwahi kuambiwa kwamba kuna kiumbe mwingine anaeishi Duniani tofauti na yeye, so hakupewa tahadhari yoyote. Kwa maana nyingine aliachwa kua vulnerable kwa shetani kumshambulia. Swali, kwa nini mungu hakumuonya Adam kuhusu uwepo wa shetani Duniani? Kwa nini alikaa kimia, lengo lake ilikua nini?. Mbaya zaidi mungu hakumuonya shetani asimrubuni adam, so akaacha loop hole ya shetani kujifanyia anayoyataka, baada ya shetani kufanikiwa, lawama ni kwa Adam.

Tu-assume alipewa maelekezo kidogo, lakini alipewa yeye, hakuna maonyo aliyopewa Eva mke wa Adam ambae shetani alimtumia kama kichochoro, je hawa makosa yao ni nini?

Jibu: Mungu aliwaingiza kwenye mtego maksudi, kuanguka kwa adam ilikua ni maksudi ya mungu kutafta justification ya kumlaumu Adam.

5. Kati ya binadamu na malaika mungu anampenda nani zaidi. Biblia inasema shetani alikua malaika mkuu, alipoasi alipata baadhi ya malaika waliomuunga mkono. Maelezo mazuri kabisa.

Biblia inaenda mbali na kusema baada ya shetani na malaika zake kuasi mungu aliwatupa Duniani watatange take. Tunakubali sawa kabisa.

Swali, kati ya binadamu na malaika ni nani anamjua vizuri shetani? Jibu ni malaika kwa sababu wameumbwa pamoja, wameishi pamoja hivyo wanajuana vizuri.

Swali lingine, kwa akili ya kawaida, ni nani alipaswa kuletwa Duniani kupambana na shetani? Jibu, alipaswa iwe ni malaika kwa sababu wanamjua vizuri zaidi shetani kuliko binadamu. Kwa maana kwamba ingekua rahisi sana kwao kumkataa shetani mapema na akakosa wafuasi kwa sababu wanamjua.

Masikitiko ni kwamba, mungu hakutaka kuwaleta viumbe wake anaowapenda Duniani akaamua kuumba viumbe wengine ambao hawajui lolote na kuja kuwapambanisha na shetani ambae ana superiority knowledge kuliko wao.

Ni sawa na wewe una rungu unaenda kupigana na mtu ana mizinga, drones, fighter jets, na kila kitu halafu utegemee utashinda. Hiki ndio mungu alichoamua kuwafanyia binadamu.

B. Nitakuja kuelezea upande wa quran(huku ndio madudu yalikojaa). Mkitaka na vifungu nitaweka.
Q urani nasubiri
 
Ungeanza kuandika wa Quran, Biblia wengi tunaifahamu sababu inapatikana kiurahisi na imeandikwa kwa Kiswahili ambayo ni kugha inayofahamika, ila Quran ikeandikwa kwa Kiarabu na kuielewa ni ngumu
Qurani zipo za kiswahili play store ..ukisoma kama moyowako mwepesi kupokea unaweza kusilimu
 
Back
Top Bottom