Matumizi ya akili bandia (AI) yahofiwa kushusha ubora elimu

Matumizi ya akili bandia (AI) yahofiwa kushusha ubora elimu

AI ni nzuri kwa anayetaka elimika
Ni mbaya kwa anayetaka faulu maana ataitumia kujibu mitihani na si kuelewa
 
Kongamano la 8 la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu limeanza leo jijini Dar es Salaam ambapo wito ukitolewa kwa wanataaluma kuongeza umakini kukabiliana na changamoto za teknolojia mpya.

Kupitia kongamano hilo lililoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), mada mbalimbali zimejadiliwa ikiwemo maandalizi ya taifa kuingia kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda mojawapo ikiwa ujio wa teknolojia na athari zake chanya na hasi kwenye elimu.

Akichangia mada hiyo leo Juni 14, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma (Udom), Profesa Lughano Kusiluka ameeleza kuwa mapinduzi hayo yamekuja na changamoto ambazo zinaweza kuathiri mifumo mbalimbali ikiwemo elimu.

Amesema ili kuepuka athari hasi ni muhimu kwa wanataaluma kwenda na kasi ya teknolojia hizo ili kubaini udanganyifu unapojitokeza.

Akitolea mfano wa programu rununu ya Chat GPT amesema inatumika vibaya na wanafunzi hivyo ni muhimu kuwa walimu kuwa makini kufanya ufuatiliaji.

“Sasa hivi kuna hii Chat GPT ni teknolojia nzuri lakini matumizi yake yanaweza kuleta shida kwenye elimu yetu, huku vyuoni sasa hivi tuna shida mwanafunzi anaweza kukuletea tasnifu imeandikwa vizuri na akapata 'A' ukiifanyia tathmini utagundua wala hakustahili kupata hiyo alama.

“Hii inatufanya vyuo vikuu na sisi tuone haja ya kuwekeza ili kuzibaini tasnifu zinazofanywa kwa njia hii, tuongeze umakini kwenye tathmini. Teknolojia hizi zipo na hatuna namna ya kuzikwepa lakini tuhakikishe hazitumiki kushusha kiwango cha elimu yetu,” amesema Profesa Kusiluka.

Akizungumzia hilo Mkurugenzi wa zamani wa Costech Dk Hassan Mshinda amesema teknolojia hiyo ni tatizo kwenye elimu kwani inawawezesha wanafunzi kufanya udanganyifu.

“Mtu anaweza kuandika tasnifu nzuri kabisa ya kurasa tano ndani ya dakika tano. Hata hivyo hatuwezi kupingana na maendeleo haya lazima tuendane na kasi hiyo. Changamoto ni kwamba kama tutaenda taratibu kila siku tutakuwa nyuma lazima kazi kubwa ifanyike kuendana na mabadiliko na maendeleo haya teknolojia,” amesema.
Mimi naona hizi AI software ni kama ilivyo Google na search engine nyingine. Pia bado haina tofauti mfano mtu akamuomba mwingine amfanyie kazi yake na yeye ku- submit. Tofauti ni kwamba ile ni software na huku aliyefanya ni binadamu. Kwa kifupi AI teknolojia haiepukiki maana ndiyo tuliyomo sasa, cha msingi ili kuiangalia originality ya kazi ya mtu ni kwanza kutumia AI detectors ambazo zitabaini ni human au AI generated content. Pili ni kumtaka huyo aliyefanya hiyo kazi kuitetea kazi yake kulingana na hoja ailizowasilisha.
 
Hii fourth revolution ndo inaenda kuleta chapa ya mnyama ambapo unique ID zitatumika kuwatambua watu wote duniani ambazo zitakuwa connected na huduma mbalimbali. Kwa maana nyingine binadamu anaenda kufanywa mateka na waabudu shetani ili watimize malengo yao ya giza.​
Nadharia njama za Mathanzua zimekuteka....acha hofu mkuu
 
Nadharia njama za Mathanzua zimekuteka....acha hofu mkuu
Alichosema ni 100% correct,wala sio conspiracy theory,acheni ujinga.Wenzenu wamewapumbaza ili msiwastukie na kuchukua hatua wawamalize,wake up.Na msipoamka watawamaliza.Wako almost mwishoni kabisa in their depopulation plan,and next year 2024 will be crucial.Wata-create a fake holographic imagery mimicking an Alien invasion while using the confusion ensuing in killing billions of people.

Tumuombe Mungu sana, ili mpango wao huo muovu kabisa kuwahi kushuhudiwa katika historia ya wanadamu usifanikiwe.
 
Elimu za samaki ana matamvua mangapi ? Huwezi kulinganisha na Chat Gpt. Mfumo wetu wa elimu ni wa kiwango cha chini sana. Teknolojia itaamua maisha yetu na siyo siasa. Revolution of science and technology.
 
Alichosema ni 100% correct,wala sio conspiracy theory,acheni ujinga.Wenzenu wamewapumbaza ili msiwastukie na kuchukua hatua wawamalize,wake up.Na msipoamka watawamaliza.Wako almost mwishoni kabisa in their depopulation plan,and next year 2024 will be crucial.Wata-create a fake holographic imagery mimicking an Alien invasion while using the confusion ensuing in killing billions of people.

Tumuombe Mungu sana, ili mpango wao huo muovu kabisa kuwahi kushuhudiwa katika historia ya wanadamu usifanikiwe.
Watu kama hawa hawataki kujihangaisha kudadisi mambo ya kinabii yalivyo, ni hadi ajikute ndani ya nyavu ndo anakuja kushtuka kuna watu waliwahi kudokeza mahali.

Hiyo vision ya kama viumbe wakishuka duniani kutokea angani niliiona, na hilo tukio kufuatiwa na hali mbaya sana ya machafuko, nakubaliana na wewe tumwombe sana Mungu Mwenyezi aweze kuingilia kati.​
 
Watu kama hawa hawataki kujihangaisha kudadisi mambo ya kinabii yalivyo, ni hadi ajikute ndani ya nyavu ndo anakuja kushtuka kuna watu waliwahi kudokeza mahali.

Hiyo vision ya kama viumbe wakishuka duniani kutokea angani niliiona, na hilo tukio kufuatiwa na hali mbaya sana ya machafuko, nakubaliana na wewe tumwombe sana Mungu Mwenyezi aweze kuingilia kati.​
Acha hofu wewe..... teknolojia haikwepeki zama hizi
 
The truth is AI is inevitable !! At least one should learn on how to use AI applications in a posive way coupled with having an idea and understanding of what you are doing !!!
 
Waambieni hao vilaza kuwa Technolojia ya sasa haizuiliki, Huko duniani waliko staharabika ambao ndio mliwacopy elimu wameamua kuukubali ukweli kuhusu technolojia.

Ukishindwa kupambana na jambo basi ungana nalo, hapo suluhisho ni serikali na hao vilaza wetu kuamua kutunga mifumo mipya ya kielimu tofauti na hii ya sasa ya kukalilishana upumbavu.

Kwa sasa tulitakiwa kuwekeza nguvu kwa wanafunzi waelewe masomo ya sayansi haswa mambo ya Computer na ubunifu wa technolojia zinazorahisisha maisha,

Sapoti kwa wabunifu huko mitaan+mashuleni, fanyeni research juu ya umuhimu wa mabadiriko ya kitechnolojia na athari kijamii, kiuchumi, kimaadili, maana haya mambo hayazuiliki ni lazima yatokee hata tupinge vipi,

kwa akili za wanadamu zilipofikia kwa kutaka kuutumia Uwezo wao wa akili kuvumbua mambo ambayo wanaona ni sahihi na yatareplace mbadala wa utegemezi+uwezo wa mwanadamu badala yake kuundwa kwa vifaa vitakavyofanya mambo ambayo mwanadamu angeyafanya au zaidi ya uwezo wa mwanadamu.

Tuelimike Technolojia ya AI ni nzuri kama tutaukubali ukweli, lkn tukiendelea kuona hili jambo ktk Muono negative basi lazima tupigike tu na hivi tunaongozwa na vilaza ambao wanajiamini na hizo akili za kukalili, basi tujiandae.
Tanzania ama afrika kuna msomi wa kuona wengine vilaza.
Sijaona hao wanajiita wasomi wanavyolisaidia taifa, ili vilaza wajovunie wasomi wao, naona tunafanana tu.
 
Waabudu shetani nimewakamata kunako, tulieni sindano iwaingie.
Yaani kuabudu shetani kukoje, maana mada haina uhusiano mambo ya Kiimani, hebu jaribuni kutenganisha Mambo basi, kwenye hizi mada kuna watu tunajifunza na kuondoka na kitu.
 
Back
Top Bottom