Hebu nikuulize, je, awamu zilizopita nchi ipi ilineemeka na mikopo/misaada kutoka nje kati ya zanzibar na Tanzania bara??
Zanzibar ilipata share yake, pamoja na facts kwamba nusu ya Wazanzibar wameruhusiwa kununua ardhi kuishi kama Watanganyika kamili. Wanaweza kugombea nafasi yoyote bara kuanzia mtaa kijiji, kata, wilaya mkoa, ubunge, uwaziri nk. Hakuna ubaguzi huku.
Angalia sasa huyu SSH anatupeleke wapi?
Angalia issue za umeme, maji,mfumuko wa bei , pembejeo kwa wakulima, tozo, mikopo, Ngorongoro, Bagamoyo, Ndugai, Mbowe anavyowashughulikia wenye mawazo mbadala.
Linganisha na Hussein Mwinyi, kaunganisha nchi, wapinzani kawaleta serikalini, mafisadi anashugulikia nao kama JPM, anajua anataka nini?
Huku bara tumerudisha mafisadi wahuni serikalini, tunayumbayumba kama mlevi wa Gongo. Muungano ni sababu mojawapo yeye kuwa pale, anaturudisha nyuma sana.