Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Samahani kwa kushindwa kueleza kwa kiswahili kizuri. Nilivyosema, kiingereza ni lugha yangu ya kwanza. Shuleni nilijifunza kidogo cha kispanya, kiswahili ndicho cha tatu.Nafikiri kwa kushindwa kutufundisha kizungu kwa kiswahili fasaha, yaweza kumaanisha kuwa amegoogle kupata tofauti ya maneno hayo na asingeweza kupata maana halisi ya maneno hayo na tofauti zake kwa lugha tofauti.
Habari gani jamani. Mimi ni mmarekani aliyeishi Tanzania miaka miwili kuanzia 2014 mpaka 2016. Nimejiunganisha na jamii forums hivi karibuni tu lakini... Samahani nimechelewa. Basi...
Wakati nilikuwa kule, nilisikia sana kosa dogo moja la kiingereza. Niliona kwamba, kati ya kiingereza cha Marekani na kile cha Tanzania, matumizi ya "somehow" na "somewhat" kumbe yamegeuka. Kabla sijatoa mifano, nitafsiri hayo maneno kwa maana zao sahihi:
SOMEHOW: kwa jinsi fulani (tukumbuke kwamba "how" ndiyo "vipi" kwa kiswahili)
SOMEWHAT: kiasi fulani, kidogo
KIINGEREZA CHA TANZANIA (ambacho napendekeza si sahihi):
"It is somehow cold today" (Ni baridi kwa jinsi fulani leo) - lugha mbovu, hatueleweani
"It is somehow a problem" (Ni tatizo kwa jinsi fulani) - lugha mbaya sana, ina maana gani hiyo?
KILICHO SAHIHI ZAIDI (tutumie "somewhat" badala ya "somehow")
"It is somewhat cold today" (Ni baridi kiasi fulani leo) - lugha nzuri
"It is somewhat of a problem" (Ni tatizo dogo) - nzuri tu, tunaeleweana
"Somehow, I was able to get to work on time" (Kwa jinsi fulani, niliweza kufika kazini mapema) - matumizi mazuri ya "somehow"
Je, tumeelewa? Kama kuna maswali nitayajibu.
google sio reliable source.Nenda kwa google. Ingiza "define: somewhat" na "define: somehow". Hivyo utasoma malinki mengi mengi tu ya makamusi kote kote mtandaoni. Yote yanakubaliana kuhusu maana ya hayo maneno mawili. Unafikiri kila kitu kilichopo kwenye intaneti ni uwongo, kisipokuwa kwenye kitabu cha maktaba?
"It is somehow cold today" na "it is somehow a problem" ni sentensi ambazo hazina makosa kama zilivyo, labda kama zimetumika pasipo,kwa muktadha usiofaa.
Nitatoa mfano.
Umeenda sehemu uliyotegemea iwe na joto kwa kufuatilia ratiba za hali ya hewa, ukakuta sehemu haina joto, na inaanza kuwa na baridi ambalo hujalielewa.
Hapo unaweza kusema "It is somehow cold today". Yani kuna jinsi fulani imetokea ikafanya sehemu hii ambayo ilitegemewa kuwa na joto iwe na baridi, sijui ni pepo za kusi, sijui ni maumbile ya kijiografia, lakini kuna namna fulani imefanya pawe baridi,ingawa sijui ni nini kimefanya pawe na baridi.
It is somehow cold today.
"It is somehow a problem".
I like this girl, I respect her. I greet her with all the verve and fanfare of an adoring fan.
Yet to her, it is somehow a problem.
Kwake hata kumsalimia kwa bashasha zote, ni tatizo.
Sijui ana kisirani, sijui hapendi kuongeleshwa, sijui anachukia sura yangu, lakini najua nikimsalimia ananikasirikia.
It is somehow a problem.
Somehow inatumika unapoongelea how.
Somewhat inatumika unapoongelea what
Somewhat inatumika kuongelea extent.
Leo ni baridi, lakini si baridi sana. It is not too hot, actually it is somewhat cold today.
Hapa kazini kuna kitatizo, lakini sitatizo sana.
I couldn't get in, my pass badge is not working, it is somewhat of a problem, but I will call my boss and he will get me in.
soma vitabu wachana na hizo wikipedia.Google inaweza kukuelekezea kwa reliable source, ukijua jinsi kuitumia. Unafikiri site za makamusi yote mtandaoni zinashirikiana kutukosea maana ya haya maneno?
Samahani nilikuwa narejea kwa post Ard67 alivyo mnukuu Tabby kwenye post #32. Wewe umetufundisha kizungu kwa kiswahili safi na tabby ndiye hakufanya vizuri kama wewe ndiyo maana nikasema yawezekana amegoogle!Samahani kwa kushindwa kueleza kwa kiswahili kizuri. Nilivyosema, kiingereza ni lugha yangu ya kwanza. Shuleni nilijifunza kidogo cha kispanya, kiswahili ndicho cha tatu.
"View" lugha mbayaview Watakuwa wengi kuliko wachangiaji
Wee jamaa yaani kama mzungu kweli,kumbe mdogo ake Afande Sele Dumila.Napendelea kutokusema jina la mtaa lenyewe, lakini ukinitambulisha kwake rafiki yako, nitapenda kuongea naye.
Hapo sijakuelewa... najua mchanga ni kile unachokikuta baharini. Unauliza kama nimewahi kula tumbo?
Nafikiri tumetoka mbali na somo la kiingereza. Tafadhali turudi, jamani.
"Acaunt" lugha mbayaHaya mmarekani !!
Asante kwa kujitambulisha hivyo kwa uzi wa kwanza kwenye hii acaunt mpya
Mwalimu unapoteza....KILICHO SAHIHI ZAIDI (tutumie "somewhat" badala ya "somehow")
"It is somewhat cold today" (Ni baridi kiasi fulani leo) - lugha nzuri
"It is somewhat of a problem" (Ni tatizo dogo) - nzuri tu, tunaeleweana
"Somehow, I was able to get to work on time" (Kwa jinsi fulani, niliweza kufika kazini mapema) - matumizi mazuri ya "somehow"
Je, tumeelewa? Kama kuna maswali nitayajibu.
Mimi nmegundua sio mtalaam ila huenda nimzungumzajiMwlsamwel
Umeandika kutumia "It is somehow cold today." na "It is somehow a problem." ni makosa.
"It is somehow cold today" na "It is somehow a problem" ni sentensi ambazo hazina makosa kama zilivyo, labda kama zimetumika pasipotakiwa, au kwa muktadha usiofaa.
Nitatoa mfano.
Umeenda sehemu uliyotegemea iwe na joto kwa kufuatilia ratiba za hali ya hewa, ukakuta sehemu haina joto, na inaanza kuwa na baridi ambalo hujalielewa.
Hapo unaweza kusema "It is somehow cold today". Yani kuna jinsi fulani imetokea ikafanya sehemu hii ambayo ilitegemewa kuwa na joto iwe na baridi, sijui ni pepo za kusi, sijui ni maumbile ya kijiografia, lakini kuna namna fulani imefanya pawe baridi,ingawa sijui ni nini kimefanya pawe na baridi.
It is somehow cold today.
"It is somehow a problem".
I like this girl, I respect her. I greet her with all the verve and fanfare of an adoring fan.
Yet to her, it is somehow a problem.
Kwake hata kumsalimia kwa bashasha zote, ni tatizo.
Sijui ana kisirani, sijui hapendi kuongeleshwa, sijui anachukia sura yangu, lakini najua nikimsalimia ananikasirikia.
It is somehow a problem.
Somehow inatumika unapoongelea how.
Somewhat inatumika unapoongelea what
Somewhat inatumika kuongelea extent.
Leo ni baridi, lakini si baridi sana. It is not too hot, actually it is somewhat cold today.
Hapa kazini kuna kitatizo, lakini sitatizo sana.
I couldn't get in, my pass badge is not working, it is somewhat of a problem, but I will call my boss and he will get me in.
Hahaha....Mkuu.Ninatokea jimbo la Missouri (linatamshwa kama neno la kiswahili: "Mizuri"), lakini siku hizi niko mbali kikazi.
Kwa mtu aliyekulia anaongea Kiswahili, na hana kipaji na ufuatiliaji kuhusu lugha, kujifunza Kiingereza fasaha baadaye kunaweza kuwa kugumu, kwa sababu ni kama kujifunza lugha yenye makosamakosa mengi.Mimi nmegundua sio mtalaam ila huenda nimzungumzaji
Hebu soma hapa kwanza. Halafu tutaendelea kujadili.Kipi kinachokupoteza? "of"?
Hapa nakubali. Kiswahili kimenyooka sana, na sheria zake za sarufi, mwandiko, na mtamsho ni nzuri kabisa. Kuna mambo machache sana nje ya hizo sheria. Ndiyo sababu ninapenda sana kujifunza kiswahili kuliko kispanya au kijerumani!Kwa mtu aliyekulia anaongea Kiswahili, na hana kipaji na ufuatiliaji kuhusu lugha, kujifunza Kiingereza fasaha baadaye kunaweza kuwa kugumu, kwa sababu ni kama kujifunza lugha yenye makosamakosa mengi.
Kiswahili kimenyooka sana, kina sheria za sarufi na matamshi ambazo zinapinda sehemu chache sana.
Kiingereza sheria zake za sarufi na matamshi ni kama nusu ya lugha inafuata sheria, na nusu nyingine imepinda.
Kwa hiyo, kwetu tuliozoea lugha iliyonyooka, kujifunza lugha iliyopindapinda ukubwani inakuwa vigumu sana.