Matumizi ya redio kwa ajili ya habari na burudani yameshapitwa na wakati

kwa redio zetu hapa bongo. Unaweza kusema BBC,CNN na nk tokea ujazaliwa zipo na zinazidi kuwepo
 
Hakika redio inabaki kuwa chombo muhimu cha mawasiliano Kwa mwanadamu,ubongo wako mdogo ndio unaweza kuweka bandiko kama hili kwamba dunia haiitaji tena huduma ya redio tena,ili kupata habari Kwa njia ya redio inahitaji redio na nguvu ya kuendesha redio,tofauti na mawasiliano mengine unayofikiri..ni mpuuzi Tu anayeweza kusema redio haina maana tena
Hivi amesema hazina maana kweli?!!! Au mimi ndo sijaelewa?!!!
Mi nimeliona angalizo tu katika masa yake kuwa zinaelekea ukingoni kutokana na ukuaji wa teknolojia.........watu wanahamishia nguvu za kupata habari upande mwingine na hilo litaleta athari (hususani hasara) kwa wanaohusika na uendeshaji wa redio (hususani mabosi) na hiyo ndo tadsiri ya anguko.
 
Mtoa mada ni mwehu. Huwezi kuondoa radio. Hivi vitu vinasupplement each other. Vyote vinahitajika. Tunahitaji radio, tv, magazeti, internet based media. We need it all. Itakapokosekana internet, tv itacover, itakapokosekana radio itacover nk. Ila kwa kuwa mtoa mada is an idiot ndo maana anaandika mashudu kama haya. Sishangai kama sasa atakuwa anaadvocate kufuta vitabu vya hardcopy kwa sababu kuna e-books and that would reflect alivyo mpumbavu.
 
Una hasira sana... Ila yeye kaandika alicho kiona.. ulipaswa kuelezea tu uonavyo kuliko kumpa maneno yote hayo,mara mwehu, idiot!!!! Hatuwezi lingana kimtazamo....
 
Ukishasema zimepitwa na wakati, sio lazima na zitakufa ina maanisha nini?Shida ni kujipigia mahesabu watu wachache wa mijini na huko walikoendelea bado redio ni muhimu kuliko vyanzo anavyodhani ni muhimu,jiulize kuna mitandao hugoma na watu huendelea kupata taarifa kupitia redio
Hivi amesema hazina maana kweli?!!! Au mimi ndo sijaelewa?!!!
Mi nimeliona angalizo tu katika masa yake kuwa zinaelekea ukingoni kutokana na ukuaji wa teknolojia.........watu wanahamishia nguvu za kupata habari upande mwingine na hilo litaleta athari (hususani hasara) kwa wanaohusika na uendeshaji wa redio (hususani mabosi) na hiyo ndo tadsiri ya anguko.
 
Skumbuki ni lini nilitune kusikiliza redio, ndio mana watengeneza TV wameling'amua mapema Sana , TV sa hv ziko na android , bila hvyo na wao wangekuwa na wakat mgumu Sana kutegemea soko la livestream linaloenda kufa kifo cha mende
 
Ujui uandikalo

Af punguza dhalau watu weng sana bado wanatumia radio kupata habari nazan ungefanya uchunguzi kwanza kbla ya kuleta mada yako

Watu weng sana tz bado hupata taarifa kupitia radio kuzid wanaotegemea mitandao ya Simu na kijamii
 
Kwanza kutegemea habari kupitia tv + redio ni kupitwa na wakati kwasasa technology imekuwa pana sana .... mimi mara ya mwisho kununua gazeti , kusikiliza hizo redio zao , na tv ...kwa lengo lakuoata habari ilikuwa 2010 ... from there cjawahi fanya ivo tena .... najua kuna wakolomije watakuja hapa kusema cjawatendea haki wa kijijini lakini huo ndo ukweli maana hata hao wa kijijini hawapati breaking news ... wanpta tarifa zilizopita muda wake ....xo nisawa na nothing

Ndugu zako uko kijijini wote wana smartphone na mitandao ya kijamii ebu jaribu kuandika vtu kwa kuangalia maslai makubwa sio ww na mke wako na watoto
Iyo mitandao iko mingap kuna semehu kibao apa tz Mitandao ya Simu haijafika wala iyo huduma ya internet haipi
 
Matumizi ya redio hayajapitwa na wakati bado,redio zinahitajika sana,Nina smartphone lakini nasikiliza redio na kuna vitu siwezi kuvipata kwenye simu lakini kwenye redio navipata,kuanzia
Burudani
Makala
Taarifa
Elimu

Ni mtandao upi utapata vipindi vya burudani kama Top 20,top 10 au mpambano wa wasanii nk.

Wapi utapata vipindi kama kutembelea wagonjwa hospitalini mitandaoni?

Ni mtandao upi utapata taarifa za habari za kina zinazohusu matatizo ya wakulima vijijini kutoka maeneo tofaut nchini na ukasikia wakitoa maoni yao.

Ni mbunge gani umeshamsikia akisema leo nitakuwa mitandao Fulani nikisikiliza kero za wapiga kura wangu? hayo utapata kwenye redio tu.

Na mwisho,kusikiliza redio ni nafuu zaidi(low cost)kuliko kutumia mitandao,kila siku lazima uweke bando wakati mwenye radio hana gharama zaidi ya umeme au betri alizoweka na pia rahisi kuendesha radio(energy)kuliko simu.Ukiwa nje ya miji ndio utajua kwamba simu ikizima na kama hakuna umeme utalazimika kusubiri mpaka urudi hata kama ni siku nzima wakati huo utakuwa huna habari yoyote wakati mwenye redio ana uwezo wa kununua betri muda wowote na akapata habari.

Kaulize wamachinga redio za mkononi au kubwa kidogo zinatoka kila siku ina maana mahitaji ni makubwa.

Hata kwenye hizo Smartphone kuna redio walijua umuhimu wake,watu wengi wanasikiliza redio,usidanganyike.

Kusikiliza redio kuna ladha yake tofauti kabisa na mitandao,hata kama umechoka ni rahisi kuzima simu au kuiacha pembeni lakini ukaendelea kusiliza redio bila karaha.
 
Mwishoni mwa miaka ya 1930s ndio redio zilianza kutumika na ilikuwa teknolojia maarufu sana wakati huo.

Wanasiasa kama Hitler na wengineo wakaitumia kueneza propaganda.

Kwa sasa redio hazina jipya, zimeshapoteza wafuasi. Hakuna mtu atakayefanya uwekezaji mpya kwasababu taarifa na burudani zinapatikana mitandaoni.

Nyingi zimejigeuza kuwa makampuni ya michezo ya kubahatisha hapa tz
Yaani utakuta redio Ina promote betting. Yaani nachokaga kabisa. Ni bora hata wasituwekee kwenye madaladala. Maana made a daladala wangejua promo wanayowafanyia wamiliki wa redio ni kama burebure
 
Nimesafiri zaidi ya vijiji mia moja vya hapa nchini na asilimia kubwa mitandao na simu janja zipo. Wasiokuwa na simu janja wataendelea kusikiliza redio mpaka pale watakapozipata.

Hata hivyo redio zitakazoendelea kudumu ni zile za serikali maana wao wanategemea ruzuku.
Wewe umeamua kuweka ligi, lakini kwa nchi maskini matumizi ya redio yatachukua muda mrefu sana
 
Hakika redio inabaki kuwa chombo muhimu cha mawasiliano Kwa mwanadamu,ubongo wako mdogo ndio unaweza kuweka bandiko kama hili kwamba dunia haiitaji tena huduma ya redio tena,ili kupata habari Kwa njia ya redio inahitaji redio na nguvu ya kuendesha redio,tofauti na mawasiliano mengine unayofikiri..ni mpuuzi Tu anayeweza kusema redio haina maana tena
Kwanza alievumbua ana akili kubwa sana
 
Matumizi ya redio hayajapitwa na wakati bado,redio zinahitajika sana,Nina smartphone lakini nasikiliza redio na kuna vitu siwezi kuvipata kwenye simu lakini kwenye redio navipata,kuanzia
Burudani
Makala
Taarifa
Elimu

Ni mtandao upi utapata vipindi vya burudani kama Top 20,top 10 au mpambano wa wasanii nk.

Wapi utapata vipindi kama kutembelea wagonjwa hospitalini mitandaoni?

Ni mtandao upi utapata taarifa za habari za kina zinazohusu matatizo ya wakulima vijijini kutoka maeneo tofaut nchini na ukasikia wakitoa maoni yao.

Ni mbunge gani umeshamsikia akisema leo nitakuwa mitandao Fulani nikisikiliza kero za wapiga kura wangu? hayo utapata kwenye redio tu.

Na mwisho,kusikiliza redio ni nafuu zaidi(low cost)kuliko kutumia mitandao,kila siku lazima uweke bando wakati mwenye radio hana gharama zaidi ya umeme au betri alizoweka na pia rahisi kuendesha radio(energy)kuliko simu.Ukiwa nje ya miji ndio utajua kwamba simu ikizima na kama hakuna umeme utalazimika kusubiri mpaka urudi hata kama ni siku nzima wakati huo utakuwa huna habari yoyote wakati mwenye redio ana uwezo wa kununua betri muda wowote na akapata habari.

Kaulize wamachinga redio za mkononi au kubwa kidogo zinatoka kila siku ina maana mahitaji ni makubwa.

Hata kwenye hizo Smartphone kuna redio walijua umuhimu wake,watu wengi wanasikiliza redio,usidanganyike.

Kusikiliza redio kuna ladha yake tofauti kabisa na mitandao,hata kama umechoka ni rahisi kuzima simu au kuiacha pembeni lakini ukaendelea kusiliza redio bila karaha.
Naunga mkono hoja zako kwa 100%
Umemjibu mtoa maada kwa facts. Good.
 
Naona umeleta matusi na kuropoka lakini unatakiwa kufahamu kwamba teknolojia hiyo haina faida kwa sasa. Lazima ife natural death kwasababu hakuna fedha za kujiendesha.
Msamehe bure tu mkuu, inawezekana ni mmliki wa Fm radio mojawapo.
 
Ila ckuiz kusikiliza radio Ni jau Sana,unakuta asilimia 90 ya maongezi ya watangazaji yamejikita kwenye kuhamasisha michezo ya kamari mixer udaku udaku tu.

Hakuna lolote la maana linaloendelea kwenye radio nyingi ckuiz maana hata habari zenyewe Ni za kuokoteza tu.
 
Back
Top Bottom