Prakatatumba abaabaabaa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2022
- 1,842
- 6,087
Kwenda kazini natumia nauli ya 2000, kwenda 1000 kurudi 1000, asubuhi haiwezi kuzidi 1000 chai na harakati zingine, mchana hapa napiga sahani ya wali na nyama/dagaa/migebuka daily, ni 2000 nashushia na juice ya buku, kwa hiyo mchana jumla ni 3000, usiku ratiba yake ni kama mchana tu, 3000 lazima nitumie, kwa hiyo kwa siku nzima natumia 8000/= vocha natumia 5000 kwa week japo week haifiki mwisho, kwa hiyo kwa siku lazima nitumie 10,000/=
Hapo sina familia, kwa mwezi natumia 300,000/= ...nyumba nakaa ya 80,000/= hapo sijapiga mahesabu ya zaka na sadaka na michango mingine ya kanisa na jumuiya, kwa hiyo kwa mwezi natumia 450K hata nijibane kivipi, kila mwezi kwenye account nabakiza kiasi cha laki moja kama akiba so tokea nimepata hiki kibarua nina akiba ya 1.5m kipato changu kwa mwezi ni laki tano tu,
Sina cha kujivunia sana kwa sababu sina plot ninayomiliki, wala asset yoyote ile, nachukia sana kwenda church Jumapili nakutana na watu wengi wakiendesha magari n.k najiona kama myonge sana lakini najipa matumaini tu kwamba ipo siku moja, Age bado sijafika 30, nina 26.
Wewe mdau matumizi yako kwa siku ni yapi? Shusha Nondo zako tupate kujifunza na sisi.