Matumizi yako kwa siku ni sh. ngapi? Je, niko vizuri au mimi ni mwananchi mnyonge?

Matumizi yako kwa siku ni sh. ngapi? Je, niko vizuri au mimi ni mwananchi mnyonge?

Hata siku ukilipwa milioni, kwa mwezi utatumia laki 8.

Mshahara hujawahi kutosha, jinsi unavyopata ndivyo jinsi unazidi spend, utaanza kula lunch ya 10000 kwa siku, nyumba 200000 kwa mwezi n.k..

Ile mindset mwezi ujao napokea, mwezi ujao napokea.. mwezi, mwaka,miaka mi 5, miaka 10 una familia, hapo matumizi yanaongezeka mara 5 yake, kama ni mnywa pombe ndio basi tena.

Ujumbe: mshahara hujawahi kutosha, mshahara unalemaza akili kama si mtu makini.

Suluhisho: Mradi nje ya kazi muhimu, fanya savings sana, epuka starehe.
 
Kwenda kazini natumia nauli ya 2000, kwenda 1000 kurudi 1000, asubuhi haiwezi kuzidi 1000 chai na harakati zingine, mchana hapa napiga sahani ya wali na nyama/dagaa/migebuka daily, ni 2000 nashushia na juice ya buku, kwa hiyo mchana jumla ni 3000, usiku ratiba yake ni kama mchana tu, 3000 lazima nitumie, kwa hiyo kwa siku nzima natumia 8000/= vocha natumia 5000 kwa week japo week haifiki mwisho, kwa hiyo kwa siku lazima nitumie 10,000/=
Hapo sina familia, kwa mwezi natumia 300,000/= ...nyumba nakaa ya 80,000/= hapo sijapiga mahesabu ya zaka na sadaka na michango mingine ya kanisa na jumuiya, kwa hiyo kwa mwezi natumia 450K hata nijibane kivipi, kila mwezi kwenye account nabakiza kiasi cha laki moja kama akiba so tokea nimepata hiki kibarua nina akiba ya 1.5m kipato changu kwa mwezi ni laki tano tu,

Sina cha kujivunia sana kwa sababu sina plot ninayomiliki, wala asset yoyote ile, nachukia sana kwenda church jumapili nakutana na watu wengi wakiendesha magari n.k najiona kama myonge sana lakini najipa matumaini tu kwamba hipo siku moja.

Wewe mdau matumizi yako kwa siku ni yapi? Shusha Nondo zako tupate kujifunza na sisi.
Matumizi ya kawaida ni 10000 kila siku

Bundle najiunga la mwezi 30000

Kodi nalipa 70000

Umeme na taka jumla hufikia 17000

Huduma za king'amuzi 60,000

Matumizi mengineyo (watoto wa kike bata etc.) kila week ni 50000- 100,000 itategemeana.

😭😭
Naishi mwenyewe. Natamani sana kuwa mbana matumizi ila kila siku zinavyozidi kwenda naona nazidi kuwa mtu wa hovyo.
 
Hata siku ukilipwa milioni, kwa mwezi utatumia laki 8.

Mshahara hujawahi kutosha, jinsi unavyopata ndivyo jinsi unazidi spend, utaanza kula lunch ya 10000 kwa siku, nyumba 200000 kwa mwezi n.k..

Ile mindset mwezi ujao napokea, mwezi ujao napokea.. mwezi, mwaka,miaka mi 5, miaka 10 una familia, hapo matumizi yanaongezeka mara 5 yake, kama ni mnywa pombe ndio basi tena.

Ujumbe: mshahara hujawahi kutosha, mshahara unalemaza akili.
Nzuri sana hii.
 
Matumizi yangu kwa siku ni kama ifuatvyo;
1. Mafuta ya gari 30,000
2. Chakula cha nyumbani 30,000
3. Simu data 5000, Voice 1000
4. Chai na chakula cha mchana nikiwa kazini 15,000
5. Misaada kwa ndugu, jamaa na michepuko 100,000
6. Bia jioni 20,000 pamoja
7. Zawadi za watoto 10,000

Akiba kwa mwezi 4-6m.

Mtanzania wa Kiwango cha kati cha chini ( Lower middle income)
 
Matumizi ya kawaida ni 10000 kila siku

Bundle najiunga la mwezi 30000

Kodi nalipa 70000

Umeme na taka jumla hufikia 17000

Huduma za king'amuzi 60,000

Matumizi mengineyo (watoto wa kike bata etc.) kila week ni 50000- 100,000 itategemeana.

😭😭
Naishi mwenyewe. Natamani sana kuwa mbana matumizi ila kila siku zinavyozidi kwenda naoma nazidi kuwa mtu wa hovyo.
Tutatoboa kweli mzee?
 
Kwa sisi wenye extended family, kwa kweli hatujawahi kuifahamu bajeti ya kila siku.

Sisi kwetu uzima ndiyo kila kitu. Na siku ikipita salama, basi tunamshukuru Mwenyezi Mungu, huku tukiendelea kuilaani kimya kimya ccm na watu wake kwa kutafuna wenyewe tu keki ya Taifa.
 
Matumizi yangu kwa siku ni kama ifuatvyo;
1. Mafuta ya gari 30,000
2. Chakula cha nyumbani 30,000
3. Simu data 5000, Voice 1000
4. Chai na chakula cha mchana nikiwa kazini 15,000
5. Misaada kwa ndugu, jamaa na michepuko 100,000
6. Bia jioni 20,000 pamoja
7. Zawadi za watoto 10,000

Akiba kwa mwezi 4-6m.

Mtanzania wa Kiwango cha kati cha chini ( Lower middle income)
Wewe umeshatoboa jamaa, kaza hapohapo
 
Hongera Mkuu kuweza kujifanyia tathmini ya Kipato chako.

Vipato vingi Kwa Vijana wengi huwa vina range humo humo

Ili kubana Matumizi nashauri ungekuwa unapika japo chakula cha usiku ambacho ungekitumia kunywea Chai asubuhi hasa kama utapika Wali.

Kingine nashauri ungepunguza kiasi cha Sadaka. Maandiko yanasema toa kadri Mungu alivyokujalia.

Sisi Kanisani kwetu, tunakuwa na Sadaka zaidi ya 5 Kila Jumapili

Kama utatoa shilingi 2,000 Kila Sadaka ina maana itakata shilingi 10,000 Kwa Jumapili Moja na shilingi 40,000 Kwa Mwezi.

Nimeona hapo juu umesema una akiba ya 1.3M, ni vyema ufanye tathmini ili uanze kufanya biashara japo hata ya Banda la Chips ili kuongeza kipato.

Wahenga walisema "Mgagaa na upwa hali wali Mkavu''

"Ndondondo si chululu"

Pia Vijana wanasema "Mbuyu ulianza kama Mchicha "

Keep hustling 💪
 
Safi sana, ngoja nichukue hii japo nilitaka nifike milion 10 nifungue, duka la simu na vifaa vyake.
 
Back
Top Bottom