DALALI MKUU
JF-Expert Member
- May 7, 2022
- 2,011
- 4,705
Nakula maweni hapo, jioni maeneo ya stand mpya ndio nakaa, siwezi fata chakula cha buku jero mwanga au jiji wakati nakaa zulumbona hapo Kigoma wali ni 1,500 wewewaelfu mbili unanunua wapi maana hapo mwanga ndio vyakula ghali ila huko ujiji,mlole,katubuka n.k had msosi wa buku upo. kitimoto buku sita tu pale manguruweni
Milo miwili kibibliaVijana wengi mnapoteza sana pesa kwa kununua vyakula migahawani. Ukijipikia utasevu pesa nyingi sana. Halafu kula ni mara 2 tu kwa siku. Kula mara 3 ni matumizi mabaya ya pesa na kiafya sio sawa.
Wewe ni mlalahoi tu. Hujafikia kuwa mlalahai.
Kaza buti.
Misaada kila siku laki😀Wewe umeshatoboa jamaa, kaza hapohapo
Ni kweli MkuuAisee kumbe unatoka saa 9 muda wa kupika unao kabisa! Unaonaje ukipika zako wali jioni unaobaki unanywea chai kama Grahams alivyosema
Wewe uwe unanunua tu chakula cha mchana.
Kwa bajeti hii, kutoboa utasikia tu.Kwenda kazini natumia nauli ya 2000, kwenda 1000 kurudi 1000, asubuhi haiwezi kuzidi 1000 chai na harakati zingine, mchana hapa napiga sahani ya wali na nyama/dagaa/migebuka daily, ni 2000 nashushia na juice ya buku, kwa hiyo mchana jumla ni 3000, usiku ratiba yake ni kama mchana tu, 3000 lazima nitumie, kwa hiyo kwa siku nzima natumia 8000/= vocha natumia 5000 kwa week japo week haifiki mwisho, kwa hiyo kwa siku lazima nitumie 10,000/=
Hapo sina familia, kwa mwezi natumia 300,000/= ...nyumba nakaa ya 80,000/= hapo sijapiga mahesabu ya zaka na sadaka na michango mingine ya kanisa na jumuiya, kwa hiyo kwa mwezi natumia 450K hata nijibane kivipi, kila mwezi kwenye account nabakiza kiasi cha laki moja kama akiba so tokea nimepata hiki kibarua nina akiba ya 1.5m kipato changu kwa mwezi ni laki tano tu,
Sina cha kujivunia sana kwa sababu sina plot ninayomiliki, wala asset yoyote ile, nachukia sana kwenda church Jumapili nakutana na watu wengi wakiendesha magari n.k najiona kama myonge sana lakini najipa matumaini tu kwamba ipo siku moja, Age bado sijafika 30, nina 26.
Wewe mdau matumizi yako kwa siku ni yapi? Shusha Nondo zako tupate kujifunza na sisi.
Nifanyaje hapo mkuu kwa maono yako? Nipunguze nini? Niongeze nini?Kwa bajeti hii, kutoboa utasikia tu.
Shukrani sana mkuu, nipo kigoma kituo cha kazi kipo ujiji, hakuna mtumishi yoyote anakaa ujiji, ujiji ndio wenyeji wapo huku ujiji sidhani kama kuna eneo lolote Tanzania linalofikia ujiji kwa kuamini na kupractise ushirikina, kila siku uwezi pita njia panda usikute vyungu, sanda n.k napenda sana kukaa eneo la kazi sema mazingira ndio yanaforce iwe hivyo, hapo kwenye nyumba ndio inabidi sasa nitafute ya chini zaidi.Angalia matumizi yako
1. Nauli
2000x 30 = 60k
Unatumia kiasi kikubwa sana kwenye nauli fanya hamia sehemu ya jirani na kazini kwako
Kama sasa hv unalipa chumba 80k ni heri uongeze 20k iwe 100k uwe karibu na kazini kwako hapo utasave 40k
2. Matumizi ya bando lako ni makubwa mno
Unatumia 5k kwa wiki je inakuingizia kipato? Jibu
Hamna hebu punguza na ujiunge na bando la wiki la 3k
Hapo utasave 8-10k kwa mwezi
3. Matumizi yako ya kula ni makubwa mno yaani unakula kibosi wakati huna hela
Punguza fanya
Asubuhi iwe 1k
Mchana 2k
Jioni 2k
Hapo utasave 3k kwa siku na kwa mwezi utasave 90k
Hivyo basi ukijumlisha hapo
Unaweza ona kwamba unaweza kusave mpaka kiasi cha zaidi ya
90+ 40 +10 ambayo ni 140k ya ziada kwa mwezi
Mwisho sheria ya mapato ili uweze kupiga hatua ni kuhakikisha unaishi kwenye nyumba au chumba cha chiji ya 10% ya kipato chako
Yaani wewe una mshahara wa 550k unatakiwa uishi kwenye chumba cha 55k
Sio unaishi kisupastaa ili washikaji na mademu wako wakusifie una gheto zuri wakati moyoni huna amani au unapigq mizinga nyumbani na kwa washkaji
Ndio maana watumishi wanaongoza kuishi maisha ya madeni kwasababu ya kutaka kuishi nje ya mahesabu yao
Rules of success
First save save save
Then jiongeze kuzalisha ulichokisave
Mazingira mzeeNi kweli Mkuu
Tena kwa muda huo wa kutoka saa 9 anaweza kufanya shughuli zake binafsi na kuongeza Kipato.
Mimi Kuna wakati huwa nawaonea Gere Walimu hasa kwenye muda wa kuwa idle.
Ningekuwa naupata Mimi huo muda, wangenambia nina hela za Majini.
Ni vile tunatofautiana namna ya kuona fursa na changamoto ya mazingira maana Walimu wengi hufanya kazi maeneo ya Vijijini zaidi🙌
Umejitahidi sana, ila unaweza kujitahidi zaidi. Rejea bajeti yako ya matumizi angalau iwe laki 3 kwa mwezitokea nimepata hiki kibarua nina akiba ya 1.5m kipato changu kwa mwezi ni laki tano tu,
Umri bado unaruhusu kabisa kwa Bongo, ila sio UlayaAge bado sijafika 30, nina 26.
Wewe mdau matumizi yako kwa siku ni yapi? Shusha Nondo zako tupate kujifunza na sisi.
Vipi akiba ipo? Au unachokipata unaspend yoote?Elfu 50mafuta ya gari kwa wiki,,kula 15k kwa siku,asubuhi napika chai mchana elfu 6,usiku 6.hiyo 3 maji juice...nyumba 350k,Airtime na internet Kama buku kumi kwa mwezi Kuna free WiFi,Sina demu,Sina mke mistress or girlfriend,,nimejiajiri ..kwa siku napata karibu 50k au zaidi,nime stuck kwenye maisha haya,najua siwezi kutoboa,I got to do something about it,,nihame nchi?naenda wapi??
Akiba wapi ukipata shida ya million kichwa kinauma,Vipi akiba ipo? Au unachokipata unaspend yoote?
Ann umemuuliza kama yupo kigoma?😁Upo kigoma?
Kwa ulaya ninakua nimechelewa? Au nimewai?Umejitahidi sana, ila unaweza kujitahidi zaidi. Rejea bajeti yako ya matumizi angalau iwe laki 3 kwa mwezi
Umri bado unaruhusu kabisa kwa Bongo, ila sio Ulaya
Zaidi ya 30,000 kwa siku