Kwenye biashara, uaminifu umekuwa shida Kwa Watanzania wengi Mkuu.
Kuna wakati nilipata tender ya kusambaza dagaa wa Mwanza kwenye mgodi Fulani. Kutokana na u-busy niliamua kumtumia ndugu mmoja kule Bunda akawa ananiagizia kwenye magari ya mizigo then nikawa napokea. Mara ya mwisho akaja akanitapeli milioni 5.5 na mzigo sikuupata hadi leo.
Kwahiyo suala la uaminifu huwa ni gumu sana miongoni mwetu.
Kwa kuwa umesema wewe ni Mwalimu ina maana wiki ijayo mtafunga shule, tumia sehemu ya Likizo hiyo kwenda Mwanza na Kahama kama ulivyosema.
Tafuta Masoko ya bidhaa zako za Migebuka, then utakuwa unawatumia mzigo then wao watakuwa wanakuingizia fedha zako kwenye akaunti baada ya kupokea mzigo ama vyovyote mtakavyo kubaliana.
Kwenye hili unaweza kudraft Mkataba mdogo kwaajili ya kuwa-guide.
Nikutakie mapambano mema kwenye suala la kukuza kipato 💪