Matumizi yangu ya mwezi

Ila wadada wa kazi za nyumbani mnawaoneaga sana asee.
Unakuta mtu yuko ofisini,kukiwa na kazi ambayo posho ni 50k kwa siku analalamika ni ndogo ila anaona inatosha kabisa kumlipa mtu mwingine kwa mwezi.
Aliyeshiba, hamjui mwenye njaa.
 
Kimsingi ndio maana tunaitwa nchi maskini...hapo ni mshahara wa mtumishi wa serikali aliyekazini miaka 10 na hajakopa kabisaa katika utumishi wake....Patia picha hapo mtu atajengaje bila kuwa Mwizi?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa mshahara anaopta alitakiwa ibaki zaidi ya 30%.
 
Nakubaliana na wewe Mkuu

Kwa hizo gharama za maisha, vyema ajikite kufanya ujasiriamali kidogo ili kujiongezea kipato

Kipato chake hakitoshi, kulingana na idadi ya wategemezi alionao
Atafanyaje ujasiliamali huku hana kipato cha kuanza huo ujasiliamali .
 
Aahh ahh nipm nikufundishe namna ya kupunguza bill ya maji hadi elfu 10 kwa mwezi
Nakucheck ila sio ya kutumia mbinu ya wizi maana washenzi ukiichezea mita tu wanashtuka na lazima waje kuifyatua
 
We takataka masikini tuu......ulimbukeni umekujaa, hvi kwa nn masikini limbukeni huwa mnawaita wadada wasaidizi wa kazi nyumbani beki tatu.....
 
Ada sio mbaya ila msosi ni kweli wanabajeti kubwa sana.
 
Sasa mimi hii laki na 30 yangu kwa mwezi naigawa vipi
 
Jaribu kutafuta source of income nje ya mshahara,alafu mkeo hakusaidii kwani baadhi ya majukumu
 
Aisee kuna gharama nimeziona hapo hadi nimeshangaa...
Elfu 15 anapewa mke kila siku,inaonesha ni mama wa nyumbani na bado unaishi na binti wa kazi....
Itoshe kusema wewe ni mtu wa kipato cha kati lakini unaishi Maisha ya kitajiri kabla hujawa tajiri....
Huna investment Nyingine yoyote maana mapato yako yanatokana na Ajira...
Anza kujiongeza kutafuta chanzo kingine cha mapato hasa biashara..
Watoto wako hawatarithi hiyo ajira yako bro....
Mke awe msaada kwako,tafuta pesa fungua biashara asimamie mke wako,mke asiwe mzigo....

Hapo umetuficha lazima unadaiwa madeni wewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…