SI KWELI Matumzi ya Wali mweupe yana hatari zaidi kuliko Soda kwenye kusababisha kisukari

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Chapisho la uongo
Nakazia hoja. Chapisho hilo lipo na ndo hili tunajadili hapa lakini yaliyomo kwenye chapisho husika sio ya ukweli halisi i.e. yana mapungufu makubwa:
1.Mwandishi anadai Kisukari kinaambukizwa(Maambukizi i.e. infectious au contagious) kitu ambacho sio kweli hata kidogo.
2. Mwandishi hajasema hatari iliyopo ni kwa wale ambao tayari wana Tatizo la kisukari(Diabetic) au vinginevyo. Wale ambao tayari wana Tatizo la kisukari; Ni kweli ulaji wa vyakula hivyo kwao ni changamoto lakini kwa yule asiye na changamoto ya kisukari hakuna shida yoyote. Zingatia hili: Kisukari ni changamoto ya uwepo wa kiwango kilichozidi cha Glucose(aina ya sukari) kwenye damu ambapo tezi iitwayo Pancrease inashindwa kuzalisha Insulin ya kutosha kuichakata glucose iliyozidi ktk.damu
3. Mwandishi ameshindwa kuelezea uhusiano wa Kongosho(Pancrease) au kiwango cha uzalishwaji wa Insulin mwilini na uwepo wa tatizo la kisukari.
Ni hayo tu.
 

Suala sio wanga au sukari, suala ni rate ya kunyonywa kwenye damu na kuspack kongosho kumwaga insulin ili iweze kuconvert hiyo sukari kwenda kwenda kutoa nguvu.
Sukari ya soda ni conc. na inaingia moja kwa moja kwenye damu, insulin ina raise kwa wingi na haraka.
Mtu hali wali directly, wengine mboga za majani, etc..fibres etc vyote hivyo vinapelekea slow but steady process hata hiyo insulin inakua na adabu.
Asia ndo nchi zinazoongoza kwa kula wali: Japani, China etc but wana rate ndogo ya unene etc why sababu ya utamaduni wa ulaji wao: wali kiaso, fibres za kutosha, mboga za kutosha..
Soda ni noma tusifanye mchezo
 
Waache kutupangia maisha kenge hao kutiahana tu 😂😂🙌 na wanaokunywa spirit je wasemwaje
 

Je! Utajuaje sukari imezidi?.
Mwathirika: 1. Anakuwa na Kiu isiyoisha
2. Anakojoa mara kwa mara ndani ya muda mfupi.
3. Anaweza kujipima mwenyewe kwa kukojoa nje mahali pa wazi ( e.g. nyuma ya nyumba yake, bustanini kwake etc) halafu baada ya muda mfupi kupita e.g. dk10-15+ aende kuangalia kama sisimizi (ants) au nyuki wachache wamekusanyika hapo alipokojolea. Kumbuka sisimizi na nyuki wanapenda sana sukari. Mkojo wenye sukari ndo unawavutia wadudu hao na huo ndo utakuwa utambulisho kwako kwamba una sukari ktk. mkojo wako. Ni ishara ya uwepo wa Tatizo la Kisukari kwako.
 
Waache kutupangia maisha kenge hao kutiahana tu 😂😂🙌 na wanaokunywa spirit je wasemwaje
Hao sio kenge na wala hawajakupangia maisha hata kidogo. Nia na lengo lao ni wanatutanabahisha i.e. wanacreate awareness kwetu. Kukubaliana nao au kutupilia mbali walichokisema inabaki ni uamuzi wako 100%.
 
Watu hawana elimu ya Lishe.

Wao wanakwambia tu acha kula wali.

Kwanini haujiulizi enzi za zamani walikula wali na miwanga kibao lakini hawakuwa na ugonjwa wa sukari.

Usasa na ujuaji mwingi ndiyo umetufikisha hapa.

Mwili unahitaji makundi yote ya chakula.

Utakuta mtu anafakamia chakula kuliko mwili unavyohitaji halafu mazoezi hana ,ndani AC ,gari AC ,ofisini AC ,muda wote yupo kwenye gari na kukaa tu.
 
Kuna mataifa kama Australia, mwongozo wa Afya ni kuwa usile wali mweupe wala ugali wa mahindi meupe kwa sababu sukari yake inakuwa absorbed kwa haraka na kusababisha spike ya sukari, ambayo inasababisha excessive production ya Insulin, ambayo ni major culprit kwenye matatizo ya heart attack na stroke. Carbohydrates ambazo ni salama ni zile coloured, kama ugali wa ulezi, mahindi ya rangi, ngano isiyokobolewa, na mchele usiosafishwa.
 
Watu hawana elimu ya Lishe.
Yep. Lakini wanazungumza na kutoa ushauri kwenye masuala ya kiLishe.
Wao wanakwambia tu acha kula wali.
Kwa kweli huo ni Ubeberu kwani mtu anapaswa aelekezwe sio aamriwe kama jeshini.
Kwanini haujiulizi enzi za zamani walikula wali na miwanga kibao lakini hawakuwa na ugonjwa wa sukari.
Sio wali tuu mkuu; rejea ulaji wa mihogo (tena mibichi), Ugali wa Dona au sembe, mahindi ya kuchoma etc; etc.
Usasa na ujuaji mwingi ndiyo umetufikisha hapa.
Exactly Yes. Mtu akielekezwa madhara yanayoweza kutokea kutokana na mtindo wa maisha ya Ukisasa anakukejeli eti unamwonea gere.
Mwili unahitaji makundi yote ya chakula.
Na ndivyo tulivyofundishwa na kuaminishwa tangu enzi hizo huko shuleni kuanzia shule ya Msingi na kuendelea -na ndo Ukweli wenyewe.
Utakuta mtu anafakamia chakula kuliko mwili unavyohitaji halafu mazoezi hana ,ndani AC ,gari AC ,ofisini AC ,muda wote yupo kwenye gari na kukaa tu.
Sasa katika mtindo huo wa maisha, mtu atakosaje magonjwa yasiyoambukiza e.g. Kisukari, Saratani, Presha, Matatizo ya moyo, Figo, Bila kusahau Viriba tumbo, n.k.?
 
jamaa ana potosha fulani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…