Kwa tanzania hii diaspora hana tofauti na muahini.Tena kwa kazi ya wanawake wawili Diaspora.
Wakati huku tunawaminya Diaspora eti kuwapa hadhi maalum tu. Sijui tunashindwa nini kuwatambua rasmi fully kama raia na hata kutambua uraia pacha.
Yaani kitendo tu cha wewe kuishi nje ya nchi hata kama kila unachofanya huko ni halali, serikali automatically inakosa imani na wewe na kukuona wewe ni potential enemy kwa ustawi wa taifa hili lenye lahana.
Yaani kibaka anayeishi pale kwenye viunga vya Manzese anaonekana ni mzalendo kuliko wewe mtanzania unayeishi ughaibuni unafanya shughuli zako halali na unatuma na remittance hapa nyumbani...😅😅
Kasumba hii ndio imepelekea mpaka kupata passport au visa imekuwa ni suala zito na gumu sana kulinganisha na nchi zingine zilizotuzunguka.
Watu wengi huwa wanamsifia Samia kuwa eti ni mwanadiplomasia mzuri, anajua umuhimu wa interactions kwa watu wa mataifa tofauti tofauti kwenye kuboost uchumi, lakini nashangaa mpaka leo hii mifumo ya mtu kupata visa,passport bado ni ile ile..
Pia nilitegemea yeye baada ya kukabidhiwa Kijiti kwa upeo wake mkubwa na exposure aliyonayo basi ataona umuhimu wa kuwathamini diaspora lakini mambo bado ni yale yale tu....
Binafsi naamini nchii hii bado haijakomboka hasa kifikra hili kuendana na dunia.