CHASHA FARMING
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 7,872
- 9,263
Matunda ya Amarula tumeyala sana utotoni, ni matunda ndani yako kama ilivyo embe sema yana uchachu kwa mbali sana na pia yanalewesha ukila mengi hivyo yulikuwa tunakula kiasi tu. Ukiachana na tunda ila pia kwa ndani kulikuwa na karanga, zile. ndoi haswaa tulikuwa tunapenda ila ni kupasua kwa mawe kama ilivo Macadamia nuts.
Sukumbuki kama mbuzi walikuwa wanakula zile nuts, sina kumbukumbu ni kitambo sana.
Amarural nuts ni the same kama Macadamia nuts ilivyo na ukila Amarural nuts then uje ule macadamai nuts utagundua ni the same thing.Tulipendelea sana nuts kuliko kula tunda la nje ambalo tulikuwa tunahofia kulewa.
Kanda ya ziwa hasa mkoa wa Mara hasa Serengeti hii Amarural ni mingi mno na haina kazi sana sana watu wanaikata tu ila hawajui kama wanakata pesa.
Ukiachana na Amarula kuzalisha ile pombe maarufu, ila pia kwa South Africa ambako kuna miti mingi sana pia wanazalisha Jam ya amarula na zinauzwa kabisa madukani.
Ukiachana sasa na tunda la nje, kumbe kule kule south Raia wana toa zile nuts na wanazikaanga na kupack na kuuza madukani. Zile nuts binafisi sikujua kama zinakaangwa make tulikuwa tunakula mbichi, ila kumbe zinakaangwa kabisa kama korosho au Macadamia nuts.
Tunaangamia sana kwa kukosa maarifa, Mungu aliweka password kwenye vitu vingi sana ili sisi kupitia elimu sasa tu unlock password zile.
Wiki jana nilionja nuts za amarula kutoka kwa mtu alie kuja nazo kiadogo kutoka South Africa ndio hapo nikakumbuka mbali sana na kujilaumu sana pia.
Ile jamii yetu ukienda ukawaambia haya matunda yanayo dondoka yenyewe na kuoza ni pesa hawatakuelewa kabisa, ukiwaambia zile karanga za ndani ni pesa wanaweza kukupiga mawe, sababu ndio kama hio.
Eneway hatujachelewa sana wadau.