Soul21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 210
- 351
Kuna kauli moja inasema hivi,
Sasa wewe mpendwa uliyepata pesa ambazo hata watoto pia ukifa leo hawawezi kurithi kwa sababu huzalishi bali unanua bidhaa zinazotengenezwa na wasomi unaowatukana, Je Huo ni woga au ujinga.
Mtu mmoja alisema hivi, Kucheka au dharau ya mjinga kwa msomi haipunguzi thamani ya kitabu, bali inaonyesha ukubwa wa giza lililomo kichwani mwake.
Wasomi ndio wanajenga na kununua bidhaa kutoka kwenu hivyo tuendelee kujenga jamii ya kuheshiamiana kwa sababu tunategemea kwa vitu vingi.
Nchi zilizoendelea hawabezani ila wanatambua nafasi ya kila mtu katika kujenga taifa.
Ndugu wasomi, pia wekezeni nguvu katika kutumia maarifa ndani ya jamii zetu ili kutatua changamoto mbalimbali zaidi na tusiwe mzigo au chanzo cha maovu katika jamii.
Tutumie elimu zetu kuishi maisha yaliyokamili huku ukitambua pesa ni matokea ya utu na jitihada zako.
Na maneno ya watu walioshindwa kifikra na kupata mafanikio haraka yasikupanikishe.
Tambua mafanikio ya haraka hujenga kiherehere ila ya polepole hujenga utu.
Tuijenge Tanzania kwa heshima kubwa.
Wajinga hawachukii elimu yenyewe, bali humchukia mtu anayewafanya waone jinsi walivyo na upungufu wa maarifa.
Hivi karibuni kuwekuwa na hali ya watu waliofanikiwa kwenye biashara za kuuza vitu si kuzalisha vitu kuwakejeli wasomi na wataalamu walioajiriwa kwenye idara mbalimbali hapa nchi kama vile Elimu, afya, ulinzi na usalama.
Naomba kuwauliza kitu kimoja, unaweza kuona MO au BAKHERSA AU GSM akikosoa na kutukana wasomi? Hapana kwa sababu ndio walioshikilia utajiri wao katika uzalishaji.Ni kwa sababu wamejiona wamefanikiwa sana na kupata pesa kuliko daktari anayeshinda hospitalini kuokoa maisha ya watu.