Tatizo kubwa la vilaza ni ujinga wa kiakili unaoathiri uwezo wao wa kufikiri vyema na hata kuweza kufanya tathmini halisi juu ya jinsi ukweli wa mambo ulivyo. Ujinga si kilema lakini ukiendekezwa hugeuka kuwa upumbavu, na upumbavu ukiendekezwa hugeuka kuwa uzuzu, yaani zumbukuku mzungu wa reli.
Wajinga wengi hupenda "short cut" ili kuficha mapungufu yao, na ili wapate mafanikio. Wasomi kwa kutambua hilo, wakitambua wana madaraka na mamlaka makubwa juu yao huwapachika vyeo vya kisomi ili kwa ujinga wao wajione kuwa nao ni wasomi, kupitia kwayo wavimbe kichwa na kufanikisha malengo ya wasomi halisi.
Mtu asiye kuwa na elimu nzuri ama akiwa mwenye elimu ya chini kwa kawaida huwa na "inferiority complex" pale anapokabiliana na msomi kihoja ama kimaono. Msomi kwa kawaida huwa ana "possess analytical skills" na wakati mwingine kulazimika ku "express critical thinking" katika mijadala yenye tija.
Ikifika hapo mtu mjinga anatumia "pre-emptive measures" kwa nguvu zake zote kumtoa msomi kwenye reli. Silaha kubwa ya mjinga dhidi ya msomi ni matumizi ya lugha zisizokuwa na staha, mf. matusi, ushirikina, masengenyo, ufitini, kuteka, kuuwa, matendo ya udhalimu na ufedhuli, na mambo mengine kama hayo.
Dhahabu hata ukiichafua kwa oil chafu ama kinyesi haipotezi thamani yake halisi. Silaha ya msomi siku zote ni wasifu wake ambao huonekana katika elimu, ujuzi, mafunzo ya vitendo, na uzoefu wake.
Chuki ya kilaza kwa msomi, haimsaidii kitu chochote, zaidi ya kumfanya a "graduate from ignorance level , then to stupidity level, and eventually to the idiocy level".