Mara yameonekana maandamano ya kuwapongeza polisi kuuwa wanaosemekana majambazi.
Kwamba maandamano hayo yamekuwa ya amani yakipokelewa na RPC wa huko, ni jambo la kupongezwa kwani haki ya kikatiba imetamalaki.
Hata hivyo kuna tashwishi za kutosha kuwa maandamano haya yameasisiwa na kuratibiwa na polisi wa huko kwa lengo la kuficha maovu yao au kujaribu kujisafisha.
Your browser is not able to display this video.
Tuhuma hizi katika hali yoyote ile si za kupuuzwa.
Ikumbukwe kazi ya polisi ni kukamata watuhumiwa na kuwafikisha kunakohusika. Katu si kuwauwa kinyama kama inavyosemekana ilitendeka.
Wakati kunaitishwa uchunguzi kwenye kadhia tata hii, ni vyema polisi wakatarajia kuyapokea maandamano mengine ya amani pia, yenye kuwafikishia ujumbe wa malalamiko.
Ni muhimu wakaliona hilo kuwa ni jambo la kheri kwani wao "kama ma taxi dereva sisi sote ni abiria wao."
Ni vyema wakafahamu wengine tulikaa kwa kutulia wengine walipoandamana kuwaunga wao mkono. Hivyo iwe wakati wao nao wa kukaa kwa kutulia ili kuyapokea malalamiko yetu.
Tunaamini kwa mujibu wa sheria, mkuki hauwezi kuwa mtamu kwa nguruwe tu.
Hapana, maandamano yanayohalalisha uvunjifu wa sheria na taratibu ni ya wajinga, yasiyofaa kuvumiliwa, hayo maigizo ya kipuuzi yatawajengea polisi kujiamini na kuendeleza tabia zao za kufanya kazi kienyeji kinyume cha sheria, na iko siku hao wajinga walioandamana yatawakuta.

Chief sheria haina uwezo wa kuishape Jamii Ingekuwa hivyo uhalifu usingekuwepo. Hata jambazi anajua risasi ndio hukumu yake ya haki.
Hakuna njia nyingine ya kuishape Jamii nje ya bunduki. Bunduki ndio silaha pekee ya kuwalazimisha watu wastaarabike
Hao wao wanapomalizwa kwa risasi uingiwa hofu na uacha uhalifu. Waganga wa kienyeji ndio chimbuko kuu la ujambazi tukiwashughulikia ipasavyo waganga wa kienyeji ujambazi utapotea kabisa, majambazi wote upewa kichwa na waganga wa kienyeji kwa kuwapa matumaini feki kwamba wanao uwezo wa kuwalinda wasikamatwe.
Mchawi jambazi mganga hawq awatakiwi kabisa kuishi hawa ndio chanzo cha matatizo yote kwenye Jamii. Zikiwemo vurugu zote chanzo ni hawq wapumbavu watatu.
Mchawi jambazi mganga hawq awatakiwi kabisa kuishi hawa ndio chanzo cha matatizo yote kwenye Jamii. Zikiwemo vurugu zote chanzo ni hawq wapumbavu watatu.