Mauaji Mara, Maandamano ya pande zote yavumiliwe

Mauaji Mara, Maandamano ya pande zote yavumiliwe

Anaemtetea jambazi ndio jambazi mwenyewe.

Kama huyu hapa?

IMG_20220928_193111_561.jpg
 
Mchawi jambazi mganga hawq awatakiwi kabisa kuishi hawa ndio chanzo cha matatizo yote kwenye Jamii. Zikiwemo vurugu zote chanzo ni hawq wapumbavu watatu.
 
Je kuna maandamano huko Mara? Kama ni kweli basi shida iko

Kabisa mkuu I am suspecting something fishing here.
Mbona majambazi yanauliwa Mara nyingi sehemu mbalimbali hapa Tanzania lakini sijawahi kuona wananchi wakiandamana kupongeza.
Hao polisi wanaficha kitu haiwezekania mamlaka za Juu zichunguze suala hili Kwa kina.
Bado Yale yaliyofanywa na Zombe hayajasahaulika
 
Tofautisha "mchawi, jambazi, mganga" na "mshukiwa mchawi, jambazi, mganga" kama ulivyoorodhesha.

Kwenye fungu la pili hata wewe unaweza kuwamo.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Ikithibitika chakula chako ni chuma Ili iwe fundisho.
Kama jambazi anaenda fungwa haimfundishi aliye nje atafanya uhalifu then ataenda jela atatoka.
hizo nchi zinazowaua wahalifu ni baada ya kustudy kwamba sheria haina uwezo wa kumfunza mwanadamu wapo watu wamezaliwa always ni criminal hata uwape shilingi bilioni moja Katu awaaji ujambazi, hawa dawa ni kuwatenga na jamii na sio kumuweka jela anakula bure kodi zetu.
 
Mara yameonekana maandamano ya kuwapongeza polisi kuuwa wanaosemekana majambazi.

Kwamba maandamano hayo yamekuwa ya amani yakipokelewa na RPC wa huko, ni jambo la kupongezwa kwani haki ya kikatiba imetamalaki.

Hata hivyo kuna tashwishi za kutosha kuwa maandamano haya yameasisiwa na kuratibiwa na polisi wa huko kwa lengo la kuficha maovu yao au kujaribu kujisafisha.

View attachment 2371340

Tuhuma hizi katika hali yoyote ile si za kupuuzwa.

Ikumbukwe kazi ya polisi ni kukamata watuhumiwa na kuwafikisha kunakohusika. Katu si kuwauwa kinyama kama inavyosemekana ilitendeka.

Wakati kunaitishwa uchunguzi kwenye kadhia tata hii, ni vyema polisi wakatarajia kuyapokea maandamano mengine ya amani pia, yenye kuwafikishia ujumbe wa malalamiko.

Ni muhimu wakaliona hilo kuwa ni jambo la kheri kwani wao "kama ma taxi dereva sisi sote ni abiria wao."

Ni vyema wakafahamu wengine tulikaa kwa kutulia wengine walipoandamana kuwaunga wao mkono. Hivyo iwe wakati wao nao wa kukaa kwa kutulia ili kuyapokea malalamiko yetu.

Tunaamini kwa mujibu wa sheria, mkuki hauwezi kuwa mtamu kwa nguruwe tu.

Shime waungwana.
Kuna time Huwa nawaza viongozi tuliowapa uongozi wanatuona kama sie ni watoto wadogo tutambaao...
 
Ikithibitika chakula chako ni chuma Ili iwe fundisho.
Kama jambazi anaenda fungwa haimfundishi aliye nje atafanya uhalifu then ataenda jela atatoka.
hizo nchi zinazowaua wahalifu ni baada ya kustudy kwamba sheria haina uwezo wa kumfunza mwanadamu wapo watu wamezaliwa always ni criminal hata uwape shilingi bilioni moja Katu awaaji ujambazi, hawa dawa ni kuwatenga na jamii na sio kumuweka jela anakula bure kodi zetu.

Ikithibitika. Nani anathibitisha? Goodluck, Mahita, Jumanne, yule mwenzao au wewe?
 
Kuna time Huwa nawaza viongozi tuliowapa uongozi wanatuona kama sie ni watoto wadogo tutambaao...

Inawezekana ni sisi ndiyo tunaowakubalia kuwa sie tu watoto wadogo ...

Si unaliona genge la kina Kalunya, RNA & Co Ltd?
 
Inawezekana ni sisi ndiyo tunaowakubalia kuwa sie tu watoto wadogo ...
Si Kweli, minyororo itakatikatika soon, mateka watakuwa huru kwenda ktk njia Yao.

Tusichoke, tusiogope. Ameeen
 
Kuna ndugu yeyote ametoa tamko kwamba ndugu yako kauwawa na sio jambazi?
Kama hakuna basi polisi imefanya kazi nzuri. Jambazi hana huruma
 
Kuna ndugu yeyote ametoa tamko kwamba ndugu yako kauwawa na sio jambazi?
Kama hakuna basi polisi imefanya kazi nzuri. Jambazi hana huruma

Tarime ndugu wametoa matamko kama ilivyokuwa mtwara, Ifakara na sehemu nyingi tu.

Kwa nadharia uliyoweka hapo basi ni sahihi kuwa polisi Ina jambo zito la kujibu.

Tofauti ya mtuhumiwa wa ujambazi na jambazi ni muhimu kuzingatiwa achilia mbali sheria.
 
Sawa wameua majambazi, lakini je kazi ya polisi ni kuua au kukamata na kupeleka mbele ya Mahakama Ambao ndio wakata mashauri?
 
Kuna ujambazi wa kalamu mnene na mingi saana, lakini masikio yetu hayasikii chochote kutoka kwa Hao Hao wanaokimbilia kunyoosha silaha kwa "majambazi" wachovu tuu.
 
Back
Top Bottom