Mauaji Moshi: RC Mghwira asema utaratibu wa kukanyaga mafuta uliandaliwa vizuri ila vibaka walivamia kutokea nje na kusababisha maafa

Mauaji Moshi: RC Mghwira asema utaratibu wa kukanyaga mafuta uliandaliwa vizuri ila vibaka walivamia kutokea nje na kusababisha maafa

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro amesema paliwekwa mabeseni ya mafuta katika mageti yote ila cha ajabu katika geti moja palitokea kundi la vijana kutoka nje ya uwanja na kulazimisha kuingia ndani kwa nguvu ndipo watu wakaanza kukanyagana.

Akizungumza katika ibada ya kuwaaga marehemu mama Mghwira amesema vijana hao hawaeleweki walikuwa wanaingia uwanjani kufanya nini kwani ibada ilishamalizika, yawezekana walikuwa vibaka.

Mkuu wa mkoa amewataka vijana hao wasiofahamika hadi sasa kutubu mbele za Mungu kwani dhambi waliyoitenda ni mbaya sana.

Mama Mghwira amesema Huduma za kiimani zitaendelea kama kawaida na kwamba mikutano ya Injili kuanzia sasa itaratibiwa kwa makini na ameomba kukutana na viongozi wote wa dini mkoani humo.

Mama Mghwira amesema aliongea na Rais Magufuli leo asubuhi na kwamba Rais alimtaka kutositisha shughuli za kidini bali waweke utaratibu mzuri wa kuzimonitor.

Source: TBC
 
Tume ya polisi imeleta ripoti kamili ya tukio hili? Au ndiyo tunakubali mambo yaendelee kama hakuna kilichotokea? Kama tutaendelea kuambiwa tukakanyage mafuta najitangaza mimi siyo raia wa nchi hii. Hii nchi na serikali yake msinihesabu kama raia wenu. Nyie endeleeni tu na ujinga mliouamini kuwa utawakomboa.
 
Hivi huo mkutano ulikuwa kwa mualiko au kila mtu alikuwa huru kuhudhuria? Maana katika kundi kubwa hivyo unafikiaje hitimisho la uwepo wa vibaka na kuwa ndio waliosababisha mauwaji? RC anacheza chini ya kiwango.......angekaa kimya tu awaachie polisi.
 
Mdogo wangu yanaitwa maelezo toka juu.
 
Hivi huo mkutano ulikuwa kwa mualiko au kila mtu alikuwa huru kuhudhuria? Maana katika kundi kubwa hivyo unafikiaje hitimisho la uwepo wa vibaka na kuwa ndio waliosababisha mauwaji? RC anacheza chini ya kiwango.......angekaa kimya tu awaachie polisi.
Amesema " inawezekana ni vibaka".......uwe unaelewa bwashee!
 
Back
Top Bottom