Mauaji Moshi: RC Mghwira asema utaratibu wa kukanyaga mafuta uliandaliwa vizuri ila vibaka walivamia kutokea nje na kusababisha maafa

Mauaji Moshi: RC Mghwira asema utaratibu wa kukanyaga mafuta uliandaliwa vizuri ila vibaka walivamia kutokea nje na kusababisha maafa

Yaani hapo mama kajidhalilisha sana. Nimemshusha hadhi kabisa!
Hivi huo mkutano ulikuwa kwa mualiko au kila mtu alikuwa huru kuhudhuria? Maana katika kundi kubwa hivyo unafikiaje hitimisho la uwepo wa vibaka na kuwa ndio waliosababisha mauwaji? RC anacheza chini ya kiwango.......angekaa kimya tu awaachie polisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tume ya polisi imeleta ripoti kamili ya tukio hili? Au ndiyo tunakubali mambo yaendelee kama hakuna kilichotokea? Kama tutaendelea kuambiwa tukakanyage mafuta najitangaza mimi siyo raia wa nchi hii. Hii nchi na serikali yake msinihesabu kama raia wenu. Nyie endeleeni tu na ujinga mliouamini kuwa utawakomboa.
Kwani kosa la Mchungaji ni lipi? Kiherehere chako ndo kinakupeleka kwa hao Wachungaji feki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amesema " inawezekana ni vibaka".......uwe unaelewa bwashee!
Hebu soma habari nzima pia.....hii sentensi umeiona bwashee?:
"Mkuu wa mkoa amewataka vijana hao wasiofahamika hadi sasa kutubu mbele za Mungu kwani dhambi waliyoitenda ni mbaya sana."
 
Huyu mama nilikuwa namheshimu pakubwa lakini nilipomsikia toka day 1 baada ya tukio hili akiongea kuhusu vibaka mimi nilimshusha sana thamami.Hatoshi na tena hafai kabisa kuwa mkuu wa mkoa.Hata kama ana mahaba kiasi gani ya kiimani hapa amechemka sana.Kumbe ndiyo maana akina Sabaya wanamdharau,wanajua ni mdhaifu mno.Hivi alikuwepo akati wa tukio au vibaka amewaonaje ?
 
Mkuu heshimu katiba wakajoliki wanaka rosari ikwap kibiblia je ikitokea wamejinyongea tumfunge kardinali.je pia waislamu tasbihi zikwap kiquran ? Ya dini tuyaache .mi katoliki naheshimu
Tume ya polisi imeleta ripoti kamili ya tukio hili? Au ndiyo tunakubali mambo yaendelee kama hakuna kilichotokea? Kama tutaendelea kuambiwa tukakanyage mafuta najitangaza mimi siyo raia wa nchi hii. Hii nchi na serikali yake msinihesabu kama raia wenu. Nyie endeleeni tu na ujinga mliouamini kuwa utawakomboa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aibu maneno mepesi pasipo uchunguzi wa kina,mama huyo hasomi biblia ni mweupe.watu wanafanya makafara yao kwa kuangamiza watu wema.walaaniwe hao na watetezi wao
 
Ukipitia maelezo ya victim wa ushenzi huu, utabaini kwamba kuna kundi la watu waovu walio kuwa wamejipanga kuzua taharuki kwenye kongamano la Mwamposa, ili watu wakanyagane, waibiwe vitu vyao na wengine wapoteze maisha - lengo hasa ni kutaka kukasirisha Dola na wananchi ili mwisho wa siku Kanisa la Mwamposa lilazimike kufungwa na yeye kufuguliwa mashtaka.
Kuna health and safety laws and regulations zimewekwa maalumu kwa public places zinazofanya events za mass kubwa kama hizi ikiwemo risk assessment. Suala la kuwepo vibaka kama intruders ni suala la wazi kabisa katika risk assessment kama ingekuwa imefanywa. Jee hizo sheria zilifatwa?
 
Kwahiyo mkuu wa mkoa kashamaliza uchunguzi.
Polisi wangechukua miezi mitatu kukamilisha uchunguzi.
Mwamposa anakuwa huru kwa sababu Mwenyekiti wa kamati ya usalama ya mkoa kashamaliza uchunguzi wake.
Kosa ni la vijana waliokuwa wanataka kuingia uwanjani.
Kesi imeisha lakini inaacha maswali mengi.
Je kuna upendeleo kwa sababu ni Mkristo?
Je hili ni swala la mkuu wa mkoa kulisemea?
Nini uchunguzi wa jeshi la Polisi iwapo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama ya mkoa ameshamaliza uchunguzi na kutupa taarifa?

Mwamposa anabaki kuwa huru viumbe dhaifu vitaendelea kupoteza uhai, tafsiri ya uhai inabaki kuwa mdomoni mwa viongozi.

Poleni wafiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom