Maisha ya watu 5 wakiwamo wasiokuwa na hatia yamepotea jana, wengine wakijeruhiwa.
Haya yakitokea katika kinachosemekana kuwa ni mwendelezo wa matukio ya dhuluma tokea kwa watu wenye dhamana ya kutoa ulinzi kwa watu.
Aliyesemekana kuwa ni gaidi anasemekana hakuwa gaidi bali alikuwa ni raia wa kawaida. Hata katika tukio lenyewe hakuonekana kujificha wala kuwa tatizo na watu.
Bwana yule alionekana kukereka na jambo, alitembea wazi wazi akionekana kulalama. Yawezekana hakuwa gaidi wala jambazi. Labda kama alikuwa ni mwenda wazimu.
Taarifa zinazoeleza uwepo wa tashwishi ya dhuluma toka kwa waliokuwa wamemkamata si za kupuuzwa.
Hata hivyo, ni nani mwenye kumfunga paka kengele? Polisi hawa wanaweza kujichunguza wenyewe? Kwa fursa ipi ya kuaminika waliyoiwekeza kwa raia?
Kwani ilikuwaje kwenye:
1. Tukio la wafanya biashara wa madini wa Ifakara?
2. Matukio lukuki ya dhuluma kwenye vituo vya polisi?
3. Matukio lukuki ya akina Sabaya?
4. Matukio lukuki ya watu wasiojulikana?
5. Matukio ya lukuki ya watu wanaopigwa, kuteswa, kufa na hata kupotea mikononi mwa polisi?
Walaaniwe wahusika wote kwenye tukio la jana.
Wawajibishwe wahusija wote kwenye tukio la jana.
Kwamba tumefika hapa kwa sababu ya ukikwaji wa haki, haikubaliki.