Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Jana 27/11/2012,BBC wameonyesha,kuhusu maalbino tanzania,inasikitisha sana,that dunia ya leo haya mambo yapo-watanzania this really shows how backwards we are-sijui tumemkosea nini mungu tu deserve such barbarism-tears flowed as i was brought back crushing to earth by events in the land of my birth-GOD HELP US

Jambo la kusikitisha na pengine kuleta hasira na chuki kwa viongozi na serikali kwa ujumla ni namna amabavyo serikali imeamua kwa makusudi kutoweka nia ya dhati ya kumaliza/kukomesha madhila yanayowapata hawa wenzetu wenye ulemavu wa ngozi hususan mauaji na kukatwa viungo vya miili yao.

Hili jambo limekuwa likipigiwa kelele mara nyingi na taasisi ambazo sio za kiserikali na mashirika ya nje na hata watu binafsi na wengine kuamua kufanya uchunguzi binafsi na taarifa kutolewa lakini mamlka husika zimeshindwa kuchukua hatua stahili ikiwemo kuwakamata wahusika.

Ifike mahali serikali na watawala waone aibu kwa kuendelea kupokea taarifa za matukio mabaya na ya kutia aibu yanayotokea ndani ya nchi kwa kuhakikisha yanakomeshwa vinginevyo sisi wananchi tutaendelea kuamini kuwa wahusika wa mauaji ya albino ni viongozi walioko ndani ya serikali na kwa msingi huo serikali itkuwa inahusika moja kwa moja kwenye hayo mauaji.

Persecuted Tanzanian albinos push for respect​
[/CENTER][/B]

People with albinism under threat of deadly attacks lead community-education drive to gain acceptance.

People suffering from albinism have long been persecuted in East Africa and Tanzania in particular.

It is estimated that more than 150,000 albinos live there, and at least 70 of them have been murdered in the past six years, often for superstitious reasons.

Al Jazeera's Peter Greste travelled to Dar es Salaam, the capital of Tanzania, for the first part of our "Global Beliefs Versus the Law" series, where an education campaign has begun.

Persecuted Tanzanian albinos push for respect - Africa - Al Jazeera English
 
Ni wazi sasa naweza kusema kwamba mauaji ya albino yanahusiana na harakati za wanasiasa wetu.

Kila tunapokuwa katika harakati za uchaguzi, ndugu zetu wenye hali ya ualbino wanauawa au kukatwa viungo.

Baada ya vurugu za mwanzo kutulia, sasa tena hali hiyo imerudi kwa kasi ikiwa ni kipindi kinachoelekea uchaguzi.

Bahati mbaya kabisa ni kana kwamba serikali inaruhusu maana hakuna hatua yoyote ya nguvu inayochukuliwa, kulingana na ukubwa wa tatizo.

Nguvu kubwa inaelekea kuzima maandamano ya kisiasa kuliko kulinda uhai wa binadamu wenzetu. Rais yuko wapi?, waziri mkuu yuko wapi?

Kwa hakika kabisa viungo vya wenzetu havisaidii katika siasa lakini hawa wenzetu wanaamini hivyo.

Je, nchi hii itafika kokote kweli katika hali ya viongozi wajinga kiasi hiki?
 
Hata km inaweza ikawa si kweli ushahidi wa ki-wakati na kimazingira unatufanya tuamini hivyo.
 
Kumbe kuna connection!!! mbona kuna mwanasiasa aliwalilia albino hadharani, je ilikuwa ni changa la macho! kwanini hakuwaambia wenzake mle mkaoni waache mchezo huo! au wale waliomshinikiza aachie ngazi ndiyo walikuwa wanajihusisha na hiyo biashara! kumbe nao wanaogopana.
 
Ndo maana kesi haziendi maana jamaa hawatakubali kufa peke yao, itabidi wahusika watajwe. Najiuliza, hivi kweli kama kiongozi wa kitaifa angempoteza kijana wake kwa mtindo huu, ingekuwaje?
 
Ni wazi sasa naweza kusema kwamba mauaji ya albino yanahusiana na harakati za wanasiasa wetu.

Kila tunapokuwa ktk harakati za uchaguzi, ndugu zetu wenye hali ya ualbino wanauawa au kukatwa viungo. Baada ya vurugu za mwanzo kutulia, sasa tena hali hiyo imerudi kwa kasi ikiwa ni kipindi kinachoelekea uchaguzi. Bahati mbaya kabisa ni kana kwamba serikali inaruhusu maana hakuna hatua yoyote ya nguvu inayochukuliwa, kulingana na ukubwa wa tatizo.

nguvu kubwa inaelekea kuzima maandamano ya kisiasa kuliko kulinda uhai wa binadamu wenzetu. Rais yuko wapi?, waziri mkuu yuko wapi? ...

Kwa hakika kabisa viungo vya wenzetu havisaidii ktk siasa lakini hawa wenzetu wanaamini hivyo. Je, nchi hii itafika kokote kweli ktk hali ya viongozi wajinga kiasi hiki??
kwakuwa mama yetu wazir wa ardhi prof. anna tibaijuka amekwisha onyesha nia ya kuwasaidia albino kwa kuwajengea uzio mkubwa kwa usalama wao, naomba urais 2015 tumchague yeye prof. anna tibaijuka
 
Kikwete aliingia kwa matanguli unadhani wafuasi wake wengine wataacha mpaka pale albino wa mwisho atakapoisha ndio MACCM yatakapofurahia na kuanza ua vijana wamemaliza wazee,wanawake sasa maalbino
 
Ni wazi sasa naweza kusema kwamba mauaji ya albino yanahusiana na harakati za wanasiasa wetu.

Kila tunapokuwa ktk harakati za uchaguzi, ndugu zetu wenye hali ya ualbino wanauawa au kukatwa viungo. Baada ya vurugu za mwanzo kutulia, sasa tena hali hiyo imerudi kwa kasi ikiwa ni kipindi kinachoelekea uchaguzi. Bahati mbaya kabisa ni kana kwamba serikali inaruhusu maana hakuna hatua yoyote ya nguvu inayochukuliwa, kulingana na ukubwa wa tatizo.

nguvu kubwa inaelekea kuzima maandamano ya kisiasa kuliko kulinda uhai wa binadamu wenzetu. Rais yuko wapi?, waziri mkuu yuko wapi? ...

Kwa hakika kabisa viungo vya wenzetu havisaidii ktk siasa lakini hawa wenzetu wanaamini hivyo. Je, nchi hii itafika kokote kweli ktk hali ya viongozi wajinga kiasi hiki??
Mkuu siyo siri, kuna wanasiasa walio ingia madarakani toka 2005 na wanafikiri kupata madaraka hayo ni kwa sababu ya nguvu za giza.
Nimefanya udadisi kidogo tu mikoa fulani na nilipokutana na wakuu fulani kiserikali walinipa kavu kavu.
Wakaniambia na wao wenyewe wamefanya uchunguzi wa kina mikoani mwao na kugundua kuwa uuaji wa albino unatokana na "order" za watu fulani toka huko huko kwenu Darisalama na Zanzibar!!!!

Hii ilinitia simanzi sana kuwa kwa kweli kutokoma kwa mauaji ya albini pamoja na kuchuna ngozi watu , inatokana na "order" za watu wanao amini mafanikio yao yana tokana na nguvu za giza.
 
Kuna wale akina Lembeli wa kahama waliwahi kuleteana Bundi kwenye kikao!! Watu wa namna hii hawawezi kumuacha Albino!! Msisahau Albino wanapotea sana maeneo hayo!! Hawa CCM hawaaaa...!!
 
kumbe ndio maana tulilishwa maneno siku za nyuma kuwa albino hafi bali hupotea tuuuu kumbe mchezo ulianza zamani mhhhhhh......
hawa wa sasa ni kwa ajili ya bunge la katiba ili watu fulani toka maeneo hayo tbr wawe weupeee tuwaone ni wasafi duuu ......kimazingira
 
Mchange atasema ni CHADEMA hao Mbowe anaua albino subirini.
 
Mkuu siyo siri, kuna wanasiasa walio ingia madarakani toka 2005 na wanafikiri kupata madaraka hayo ni kwa sababu ya nguvu za giza.
Nimefanya udadisi kidogo tu mikoa fulani na nilipokutana na wakuu fulani kiserikali walinipa kavu kavu.
Wakaniambia na wao wenyewe wamefanya uchunguzi wa kina mikoani mwao na kugundua kuwa uuaji wa albino unatokana na "order" za watu fulani toka huko huko kwenu Darisalama na Zanzibar!!!!

Hii ilinitia simanzi sana kuwa kwa kweli kutokoma kwa mauaji ya albini pamoja na kuchuna ngozi watu , inatokana na "order" za watu wanao amini mafanikio yao yana tokana na nguvu za giza.

Hata mimi nilihakikishiwa ni wanasiasa na kwa ujumla wanafahamika, tatizo ni upuuzi tulioanzisha nchi hii kwamba mwanasiasa wa chama tawala sasa hawezi kufikishwa kwenye vyombo vya sheria wanalindana. Kama wangekuwa ni CHADEMA, Hakika wangekwisha fikishwa mahakamani.

CCM wamekuwa ni uhuni na ndo maana nawafananisha na wauza madawa wa kolombia. Hakuna mzima wote ni watu wa kufanya mambo ya hovyo tuuuu
 
Wanatuharibia sifa ya Tz tunaonekana watu wa ajabu sana
 
kwakuwa mama yetu wazir wa ardhi prof. anna tibaijuka amekwisha onyesha nia ya kuwasaidia albino kwa kuwajengea uzio mkubwa kwa usalama wao, naomba urais 2015 tumchague yeye prof. anna tibaijuka

Naye haonekani kama ni profesa. Kila wakati mawazo yake ni ya kizembe kabisa! Nchi gani duniani ambayo inaamua kufungia watu. Mbona Rais hajafungiwa ikulu kuliko kumulinda kila siku. Mama huyu naye konokono tu!
 
Wana Jf;

Tunaungana na makundi mbali mbali pamoja na ndugu zetu Albino waliotoa kilio na kupaaza sauti zao ktk kipindi MUHIMU sana cha Malimbano ya Hoja ya ITV yaliyopita wiki hii, ambao yalifana washiriki wengine kudondosha machozi hasa pale aliposimama Mariam Stanford ambaye wauzaji hao wanaolindwa na serikali mbali na kuendeleza uovu WAO kwa takriban miaka 30 sasa bila hata muuaji MMOJA kapewa adhabu inayoendana na robo ya madhara wanayosababisha kwa familia, Jamii na utulivu wa taifa nzima. Mariam alirudia na kurudia tena akisema, "...haya ni matendo ambayo serikali inayajua, wanasiasa wanaoyafanya serikali inawajua, viongozi wanawajua, ni matendo ya wanasiasa, ..serikali inawajua...aliyenikata mikono yote miwili namjua, tumeishi naye kijijini, namjua...niliitwa kwenda kutoa ushahidi, niliongea kila kitu, nilimtaja...ila Serikali ikamwachia huru...serikali ikasema eti ushahidi wangu sio sahihi...sioni vizuri, nina upungufu wa kuona, ..sasa yupo kijijini anatembea kifua wazi anatamba bila woga wowote....nasema Serikali ilaaniwe, ilaaniwe, ilaaniwe milele, milele..." Mariam alimalizia kwa uchungu! Machozi yaliwadondoka wachangiaji wengi...

Nasi tunasema tena Leo hii na siku zote,...Serikali hii dhaifu, kwa dhuluma hizi, udhaifu huu na kulinda wauwaji wa albino wakati serikali inaandaa ulinzi mkali wa gharama kwa ajili ya wanyama-pori, tembo, nyati, NYOKA, mbwa mwitu, kenge nk kwa kutumia helkopta na vikosi vya majeshi ktk kampeni Tokomeza na nyinginezo wakati ndugu, watoto, dada, kaka, wazazi wetu walio albino wanauawa na kukatwa viungo machoni mwa watawala, polisi na wakuu wa nchi waligeuza nyuso zao pembeni kwa miaka 30 bila kutenda lolote linaloendana na uovu huo...."Serikali ilaaniwe, ilaaniwe, ilaaniwe milele, milele"

Kadhalika, pia kwa Serikali hii hii kwa kuungana na CCM kuvuruga Rasimu ya umma iliyobeba HAKI, maoni na dhamira wa WANANCHI kupata Katiba yao Mpya ambayo ingelinda na kutoa adhabu Kali kwa wauwaji hawa na waovu wengine wakiwemo wanasiasa hao hao wanaoivuruga Rasimu, tunatamka NENO lile lile..."Serikali ilaaniwe, ilaaniwe, ilaaniwe milele, milele"

Watoto, na wajukuu wetu watacheza ngoma na kushangilia juu ya makaburi ya viongozi hawa wa UTAWALA wa CCM na makundi yanayowaunga mkono ili mradi wapate kushibishwa. Hakika siku zitakuja pale ambapo magereza YETU yaliyojaa vijana wetu wengi maskini wa kesi za kuku, na udokozi kwa ajili ya kujipatia tu mlo wa siku, magereza HAYO yatajaa watoto wa Vogogo watawala hawa wanaodhulumu uhai wa watu, wali ASILI, uuzaji wa Unga na rasilimali za nchi...na NDIPO itakuwa shangilio juu ya makaburi ya wazazi WAO....siku hii itakuja muda sio mrefu!

Naomba kuwasilisha!
 
Ana haki ya kikatiba ya kukata rufaa..alafu acha kuhusisha mapungufu ya watu na vyama..inawezekana huyo aliyefanya huo unyama ni mfuasi wa chadema au cuf,inawezekana hao waliodhulumu haki yake mahakaman ni wafuasi wa ukawa,,hapa hoja ni kuwa haki haikutendeka hivyo hana budi kwenda ngazi inayofuata kutafuta haki yake...!
 
Acha porojo na kujing'ata ng'ata, CCM ndiyo mhimili wa yote...uovu wote uu juu yao, ingekuwa CMD, au Cuf au yeyote nje ya CCM wangeshamnasa na hata kumng'oa meno na kucha, lakini ili mradi ni wauaji wenzao...HAKUNA nyani wa wakumfukuza nyani mwenzake aache kula mahindi shambani, asiulizwe mbona nawe unafanya vile na vile? Na kwa taarifa yako hawezi kuiondoa hali hii mbali na mfumo mbovu wa CCM na dhamira yao kuhakikisha wanaangamiza malengo yaliyo wazi ktk Rasimu ya II, ktk kulinda HAKI, uhai wa raia na dhuluma kama wanavyofanya free kwa sasa...! Kamwe ili kujilinda, watafanya wawezavyo kuizuia au kuvuruga Rasimu, na ndicho wanachofanya sasa...unatetea uovu huu bila soni yoyote Usoni?...mmekopeshwa akili au?....useless mind.
 
Ana haki ya kikatiba ya kukata rufaa..alafu acha kuhusisha mapungufu ya watu na vyama..inawezekana huyo aliyefanya huo unyama ni mfuasi wa chadema au cuf,inawezekana hao waliodhulumu haki yake mahakaman ni wafuasi wa ukawa,,hapa hoja ni kuwa haki haikutendeka hivyo hana budi kwenda ngazi inayofuata kutafuta haki yake...!

Mbona kuna mdada aliyekatwa mkono alisema aliyemkata mkono anamfahamu na alishikiliwa akaja kuachiwa na yeye kuambiwa hakuona vizuri tena aliyemkata mkono aligombea ubunge Mwanza na akashindwa
 
Back
Top Bottom