Kuna kipindi kinaendelea sasa kinajadiri mauaji ya Albino yanayoendelea Tanzania. Wanajadiri kupitia kipindi kinachoitwa The Stream, ni kipindi ambacho watu kutoka maeneo mbalimbali kupitia Skype ujadiri kwa pamoja. Kuna Albino kadhaa wa Tanzania wameunganishwa.
Mhusika mmoja wapo anasema Mwaka 2009 Pinda alilia na akapiga marufuku uganga wa Tunguri, lakini baada ya Waganga wa kienyeji kuwatishia wanasiasa kuwa kama wataendelea kuwafungia basi hawatatoa huduma kwao katika uchaguzi unaofuata (2010). Baada ya mkwara huo, Pinda na serikali yake wakawaruhusu tena wapiga tunguri, na mauaji yakaendelea kama kawaida kwenye uchaguzi. Pia jamaa wanasema kuwa asilimia 60 ya Watanzania uenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta huduma.
Al Jazeera inatazamwa na dunia nzima, hii ni aibu. Inaonesha, wakati wenzetu wanatumia akili nyingi kuvumbua mashini za kuchimba madini kirahisi na kupata madini mengi, sisi tunakimbiza Albino tukidhani wao ndio wanaoleta kwa wingi.
Kumbe kilio kilikuwa cha kifurahia ukatili husika!