Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Kuna kesi za mauaji kama haya zaidi ya 76 nchi nzima, zilizokwishatokewa hukumu ni 5 tu na kati ya hizo tano watuhumiwa wengine wameachiwa huru kwa rushwa.

Lkn pia muuaji unamfunga ili iwehe? Huko si kubadilisha tu style ya maisha?

Katika hali kama hii unategemea wananchi wasichukue sheria mkononi?

Serikali legelege haioneshi nia ya dhati kukabiliana na hili jambo.

Mkuu ukiona hivyo ushahidi hamna.serikali ni sikivu sana.
 
Mkuu usinitafutie balaa please! Mie nimetoa mfano tuu
lakini hata hivyo hayo uyasemayo ni kweli kwa asilimia kubwa sana. sehemu kubwa ya hawa viongozi wetu ni washirikina. na wala sio hao wa mikoa husika tu ila ni karibia nchi nzima. nchi hii inaendeshwa kishirikina wala sishangai kuchelewa kwenye maendeleo.
imagine tumepata uhuru miaka zaidi ya 53 iliyopita na leo hii bado ni nchi masikini kabisa duniani. tena hakuna hata vita na tuna kila aina ya rasilimali.
 
Ni jambo la kuudhi tena la kukatimisha tamaa kuona kuwa hadi hivi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kufuatia wimbi la mauaji ya ndugu zetu wenye matatizo ya rangi ya ngozi ambao wanajulikana kama Maalbino. Taifa ambalo limeweza kupelekeka wanajeshi zaidi ya 700 kwenda kumng'oa Bakari wa Comoro limeshindwa kufuatilia wauaji wa maalbino ambao wanafanya hivyo with impunity. Hivi kwanini Rais Kikwete anaamini kuwa kwa "kukemea" mauaji hayo yatakoma? Viongozi wa dini wanayakemea na wa serikali wanatoa maonyo ati wauaji hao "wakome mara moja" tabia hiyo! Nikiwa mmoja wa watu waliopitia elimu ya tabia naamini kuwa tunachoshuhudia ni kuibuka kwa serial killing katika Tanzania ambapo walengwa ni maalbino. Ni sawasawa kabisa na mauaji ya mfululizo yanayofanywa dhidi ya makahaba, vikongwe n.k ambayo wengi tunaamini ni "ushirikina" kitu ambacho kinatupa udhuru wa kushindwa kufuatilia. Naamini mauaji ya maalbino yanatokana na reward ya mauaji yenyewe kwa wauajji na watu hao hawatakoma hadi watiwe pingu. Kama tumeshindwa kuzuia wizi wa fedha za umma, ina maana kina manumba na RO wameshindwa hata kulinda usalama wa maalbino wa Tanzania?
Kitu ambacho kilikuwa wazi sana ila sijasikia mtanzania aiyeng`amua ni pale Police walipojiwekea malengo ya kihuni kuwa watamtafuta akiwa ahai au amekufa..yule mkuu wa mkoa mwenye aliyeshindwa arusha bingwa wa kuropoka na kutumia madaraka vibaya Mulongo AKAJISIFU KUWA SERIKALI INA MKONO MREFU NA WATAMTAFUTA AKIWA HAI AU AMEKUFA.Maana yake nini...?wamekausha kifo,na wanaojificha kuwa watapata mwili.Na wezi wakawapata nafasi kuwa shida si kumuua ila kumpata.Huwa Watz hawana muda wa kufikiri kuanzia wanachoongea hadi wanachotenda au hata hatari iliyopo.Sikuwahi msikia mti akiwatahadharisha kutomuua..na very soon ikawa km nilivyoona. kapatikana Kauwawa kwani walichotaka majangili wa albino hakikuwa haramu ktk macho ya MACCM.Na huu uzembe utauona hata hapa JF kuna mods wajinga ila hawapo honets enough kukubali kuwa hawajui.Mada nyingine hawawezi zimeza ila zina maana sana ktk usitawi na usalama wa nchi.
 
Nilikuwa nikitazama kipindi cha Agenda 2015 kinachorushwa na Star TV, kilichonisikitsha ni maelezo yaliyotolewa na mwenyekiti wa chama cha albino mkoani mwanza Bwana Alfred Kapole ambae ni albino pia.

Alfred Kapole ameelezea jinsi alivyoandaa mtego ili kuwakamata watu wanaojihusisha na mauwaji ya Albino. Anasema aliamua kunyoa nywele zake na kuzitangazia soko, katika mtego huo alimshirikisha kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza kwa kipindi hicho Afande Zerote Stephen.

Mteja wa kununua Nywele za Alfred alipatikana. Siku ilifika na Alfred alimuuzia nywele jamaa, mara tu baada ya kuuziwa nywele zile, polisi walifika na kumhoji mtuhumiwa kuwa wanamhisi ana vitu vya magendo, mtuhumiwa alikana kuwa na vitu vya magendo na badala yake alisema ana Nywele za Alfred Kapole, mtuhumiwa alizitoa Nywele zile na kwa kuwa eneo lile kulikuwa na watu wengi pia walishuhudia kitendo hicho. mtuhumiwa alichukuliwa polisi.

Ilifika siku ya kwenda mahakamani Bwana Alfred alikwenda kutoa ushahidi, lakini Hakimu aliamuru Nywele zile za ushahidi zipelekwe kwa mkemia mkuu wa serikali. Nywele zilipelekwa kwa mkemia, lakini cha ajabu majibu yalirudi yakionesha nywele zile sio za binadamu ni za mdoli (TOY). Rushwa inalitafuna taifa.

Alfred anadai majibu hayo hayakumsikitisha yeye peke yake bali hata kamanda Zerote Stephen alisikitika sana

Swali hapa wadau ni vipi tutaipigana vita hii ya mauwaji ya albino? maana naona Pinda nae tangu alie machozi bungeni hataki tena kuzungumzia hii ishu. Mkuu wa kaya yuko kimya lakini ndugu zetu wanauwawa tena kwa mateso jamani

Pongezi zangu kwa muongoza kipindi wa Star TV Dotto Bulendu, ameonesha kuguswa sana na jambo hili na ameliongelea kwa uchungu mkubwa. Inasikitisha wabunge kuwa wanaomba bunge lisitishe shughuli zake wazungumzie suala la dharula kama kupigwa waandamanaji wa CUF lakini hawajawahi kuomba kuzungumzia mauwaji ya Albino.

Naomba tuungane Watanzania tupige kelele mpaka mkuu wa kaya aelekeze nguvu nyingi kadri iwezekanavyo katika kupambana na swala hili
 
Watanzania swala la mauaji ya albino yametawala kila kona na kauli mbiu STOP KILLING ALBINO lakin serikali inahamasisha wananchi kushiriki kutoa taarifa ya mauaji hayo. Ngoja nijaribu kutoa nafas kwa wana JF kupata mawazo yenu, maana haya mauaji ya albino yanakidhiri kipind cha uchaguz au panapo karibia kwa kuteuliwa kwa WAKUU WA MIKOA, WILAYA, MAJAJI,WAKURUGENZI na nyasifa za juu kibao!! Swali . JE KUNA HUSIANA NINI KATI YA NYISIFA ZA JUU ZA SERIKALI NA VIUNGO VYA ALBINO??????? maana hata kama ndio ushikirina viungo vyao unafikiria niatumika wapi?????? ni ufinyu wang wa mawazo but
 
Angalia mkuu wasije wakakuletea madhara maana ni nyoka wenye makengeza
 
CCM ni wauwaji...kuna ushahidi usio na shaka kwamba mtoto aliyeuawa juzi ni viongozi wa CCM wasaka urais kundi la mwigulu ndi waliohusika.....Kuna ushahidi wa wazi...narudia...wakati ukifika tutayaweka wazi
 
CCM ni wauwaji...kuna ushahidi usio na shaka kwamba mtoto aliyeuawa juzi ni viongozi wa CCM wasaka urais kundi la mwigulu ndi waliohusika.....Kuna ushahidi wa wazi...narudia...wakati ukifika tutayaweka wazi

Huu ndio wakati muafaka wa kushusha huo ushahidi.
 
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye (pichani), amesema serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kudhibiti na kupambana na vitendo vya mauaji vinavyofanywa dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) na hivyo kusababisha kukithiri.

Akizungumza jijini Mwanza juzi wakati wa uzinduzi wa albamu ya watoto ya Kanisa la EAGT Lumala mpya, Sumaye alisema vitendo vya baadhi ya watu kuwanyakua watoto wenye ulemavu wa ngozi na kuwaua, vinasikitisha, kwani vinakiuka haki za binadamu.

Alisema serikali kutochukua hatua mwafaka dhidi ya vitendo hivyo, kunalisababishia taifa aibu, hasa pale inapoonekana baadhi ya wahusika kutumia viungo vya albino kutafuta madaraka au utajiri.

Hivyo, aliishauri serikali na vyombo vya usalama kuchukua hatua zaidi ili kukabiliana na vitendo hivyo.

"Haiwezi kuingia akilini eti viungo vya binadamu, hasa albino vinasaidia kupata umaarufu wa uongozi ama madaraka. Kama ni hivyo, kwanini usitumie kiungo chako ili ufaidike na utajiri huo," alisema Sumaye.

Alisema fedha zinazotolewa na baadhi ya watu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu zinatokana na ubadhirifu wa mali za umma na kuwatahadharisha viongozi wanaosimamia michakato ya uchaguzi kutenda haki kwa wagombea na wapigakura ili kuepukana na machafuko kama yanavyotokea kwa baadhi ya nchi barani Afrika

Awali, Mchungaji wa Kanisa hilo, Daniel Kulola, alisema wamekuwa wakiwalea watoto katika matunzo ya kumtukuza Mungu ili kupeukana na matendo maovu.

Chanzo:Nipashe
 
Yericko Nyerere acha bangi za asubuhi asubuhi, sasa hilo gobole la kwenye makumbusho ya Mkwawa kule Kalenga lina tatizo gani Kinana akishika? Mbona kila mtu akienda pale makumbusho analishika?
 
Last edited by a moderator:
Yericko Nyerere acha bangi za asubuhi asubuhi, sasa hilo gobole la kwenye makumbusho ya Mkwawa kule Kalenga lina tatizo gani Kinana akishika? Mbona kila mtu akienda pale makumbusho analishika?

Lete picha yako ukiwa umelishika hilo gobole
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: mpk
Ha ha ha nawaona magamba yanavyorukaruka kutafuta pa kutokea Yericko Nyerere.. Ila kwa huyo Kinana hapo alikuwa anajaribisha kuona kama inaweza kumfaa kwenye ile biashara yake ya pembe za ndovu..
 
Last edited by a moderator:
Mtaalamu wa majungu na hadithi za uchonganishi!
I hope you put your head to better use!!!
Mkuu toka posti yako ya kiuzushi wiki iliyopiya juu ya mapigano ya Amboni, ambapo ulisema ni polisi na polisii wanarushiana risasi, mi nilikutoa maanani.Wewe ni jungu kubwa na mkuu wa majungu humu JF.

Kwani mkuu hebu nijuze.. Polisi walikuwa wanarushiana risasi na nani.. wanajeshi..? Maana naona picha imefia kati wala haijajulikana mwisho iliishia wapi..!
 
Albino wote wanauwawa wahusika wanakuwa wanatumwa na viongozi wakubwa wa ccm hilo wazi .kuhusu uhusiano wa silaha zinazoibiwa kwenye vituo vya polisi zinawezekana zikawa hujuma za Chagonja na Kinana kumwaribia IGP Mangu
 
Yericko ni mtuhumiwa namba moja kwenye haya mauaji halafu mpaka leo hajaweza kujibu tuhuma zake zinazomkabili,

Lazaboni aliwahi kuweka uzi ambao unaelezea vizuri sana anavyohusika na hili sakata.
 
Albino wote wanauwawa wahusika wanakuwa wanatumwa na viongozi wakubwa wa ccm hilo wazi .kuhusu uhusiano wa silaha zinazoibiwa kwenye vituo vya polisi zinawezekana zikawa hujuma za Chagonja na Kinana kumwaribia IGP Mangu

Mkuu...kwa hili la juzi geita ni kundi la wana CCM wasaka urais...wamemuua yule mtoto...Ushahidi upo...Tutauweka wazi...wao wanadhani tunatania
 
Back
Top Bottom