Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Ingekua inawezekana mvua ya namna hiyo kunyesha kwenye nyumba za wahalifu na kuwaacha waadilifu ingekua safi sana lkn kwa bahati mbaya haiko hivyo.

Na asingeweza kubaki hata mmoja kwasababu kila mtu ana uhalifu wa aina yake, hata yule unayemfikiria ni mchungaji safi wa kanisani naye anaiba sadaka! ! Haahaa kwa sisi wakristo huwa tunasema tunaishi kwa Neema za Mungu tu.
Btw mtoa mada WISE BOY acha uongo si Tanzania pekee ambapo watu wenye albinism wanauawa fanya uchunguzi tena kabla hujauvua uraia wako. 😂😂😂😂😂

kikubwa wa Tz tuache ushirikina jamani, Ushirikina ni options tu, kama issue ni kutumia ushirikina ili ufanikiwe unaweza ku opt another way na bado ukafanikiwa.
 
Last edited by a moderator:
Wise Boy
Nilipoenda skuli waliniambia when some one is wise, mfuate huyo. Ila miye niukane Utanzania wangu kwa sababu hizo ulizotaja, Mhhh.
Niende wapi, nani anipokee hadi wanajua kuwa huenda ni weye mwenye hiyo kitu ndo maana unataka kuhamia kwao ukawaue walio kwao? Kila nchi ina Albino, huko wakimsikia Mtanzania maini yanawapasuka. Wanajua lile Joka la Makengeza limekuja.
We achatu, yaani, usijaribu kuukana utz. Nchi ya amani, baba anamwuza mwanaye. Kabla ya kuuza anajaribu gadget ka inafanya kazi kwa kumtuma wembe dukani, kwa kumdanganya avute redio karibu,, ikizima tu tayari wateja kibao.
Utaishi wapi Wise Boy??
Dawa ni kuwataja wanga hao na kikosi chao. Wanyongwe, tena wanyongewe Sokoni mchana siku ya soko. Kibri yao itaisha, Tusihame nchi
 
Nimekaangalia kale katoto ka kialbino kanavyolia pale hospitali! Nyee!! achene tu. Halafu kila siku kuna mikesha ya kuombea hii nchi. Tumejikwaa wapi?
 
ikiwa wiki moja tangu rais kikwete atoe msimamo juu ya mauaji ya albino, tukio hilo limetokea tena huko sumbawanga mpanda, kwa mtoto kukatwa kiganja cha mkono. je, rais aliongea kwa nia ya dhati??

na ni kwel serikali ina nia ya dhati kutokomeza mauaji hayo? na hao watuhumiwa 13 wa kunyongwa rais amekwisha saini?na kwa nini wasionyeshe kwny tv hao wanaotakiwa kunyongwa?
Hapa lazima tuelewa yafuatayo, hivi unamjua kikwetete? je unamjua rais Kikwete? Unaijua serikali? Kikwete kama Kikwete ni mswahili wa Msoga sawa na wale waswahili wenzake. Mswahili hajawahi kuwa serious anaongea kama cherehani mambo asoyajua na kamwe hawezi kutekeleza na anajua hawezi kutekeleza ila ataongea kwa vile ana mdomo. Kikwete kama rais sote tunajua ni dhaifu hata Mh. Mnyika alitukumbusha pale bungeni. Sifa ya rais dhifu ni kujifanya laisses faire kumbe ni mbinu ya kuficha udhaifu Wauaji wa albino ni matajiri na wanasiasa wakubwa ambao ni marafiki na wafadhili wa ikulu. Mfano mzuri ni wa Gurumo ambaye anafanyia uchafu pale anapopanga Rais Kikwete - Magogoni. Serikali legelege haina muda na watu wake kuhusu hifadhi yao. Serikali hii ya kikwete ni legelege na matokeo yake ni kwamba wengi waliopo serikalini pamoja na Kikwete mwenyewe na kwa maslahi zaidi. Kama masilahi yanapatikana kwa kutumia viungo vya albino basi itabidi wateske tu hakuna ulinzi. Kama kule kanda ya ziwa majangili waliwapora mama watoto wenye albino inteligensia ya kikwete ilikuwa wapi kuchukua taadhari dhidi ya watoto wengine albino? Kwa nini tukubali kwamba tukio la mama wa Sumbawanga kuporwa mtoto ni mpango mzima wa watu walio serikalini? Mbona yule afande siku ile alijitapa wana orodha yote ya albino nchini. Leo atatuambia nini. Vserikali vyote dhaifu vinang'ang'ana vijiinteligensia dhaifu vya kuandama watu dhaifu wanao onekana wakiandamana barabarani kama CUF na CDM. Kamwe hawana inteligenisia sophisticated ya ku-deal na wababe wasaka albino au wale magaidi wa Amboni. Yule kamanda wa operesheni alituambia tukio la Amboni nila kihalifu sio la kigaidi. Amiri jeshi wake mwishoni mwa mwezi anatuambia kuna elements za ugaidi. Hiyo ndio serikali yetu. Rais, mkuu wa nchi, m/kiti wa chama tawala na amiri jeshi mkuu anajitutumua kutishia nyau wazee wa albino, bila mafanikio. Bila kumung'unya maneno huyu bwana anstahili kujiuzulu. Kazi imemshinda hawezi kutoa matamko hata wiki haijapita tunashuhudia mtoto anakatwa kiganja, jiuzulu amiri jeshi mkuu ili kujenga heshima yako.
 
Nimeamua Kwa Moyo Wa Dhati Kabisa Kuukana Uraia Wa Tanzania,sitaki Kuwa Mtanzania Na Siitambui Tanzania,ila Nafahamu Kuwa Jakaya Mrisho Kikwete Ni Rais Wa Tanzania, siwezi Kuendelea Kuwa Mtanzania, naogapa Ghadhabu Ya Mungu ambayo muda si mrefu itashuka juu ya taifa hili la kishirikina na Kuangamiza Maelfu Ya Watu,

hakika Mungu amechoka na upuuzi wa hili taifa wa kuua ndugu zake kikatili na kubeba viungo kwa imani za kishirikina,kila siku nalia, nimelia hadi Nimechoka, ndugu Zetu Wanaishi Kama Wanyama Mwitu Ndani Ya Taifa Lao, ili Nikwepe Hasira Za Mungu Juu Ya Hili Taifa Ni Bora Nikaukana Utanzania Mapema Sana, watu Wanadhani Ni Mchezo Lakini ipo siku isiyo na jina

ambapo Tanzania itakuja kupata pigo kubwa sana, ushenzi wa taifa hili hauvumiliki hata chembe, dunia nzima ni Tanzania Pekee inayoua albino kwa imani za kichawi, wakati mataifa yote yanaamini uchawi na hayaui albino, ole Wako Tanzania Maana Siku Zako Zinahesabika Utalia na kusaga meno,kuanzia Leo Sikutambui Tanzania,kaa Na Laana Yako Mimi Simo Najitoa.

Mkuu, maneno makali sana, ni kama ujumbe wa kinabii. Lkn hata ikiukana Utanzania wako zitabaki kuwa siasa, kama asili yako, kama wazazi ni Watanzania, kitovu chako kiko Tanzania na utabaki Mtanzania.
 
ikiwa wiki moja tangu rais kikwete atoe msimamo juu ya mauaji ya albino, tukio hilo limetokea tena huko sumbawanga mpanda, kwa mtoto kukatwa kiganja cha mkono. je, rais aliongea kwa nia ya dhati??

na ni kwel serikali ina nia ya dhati kutokomeza mauaji hayo? na hao watuhumiwa 13 wa kunyongwa rais amekwisha saini?na kwa nini wasionyeshe kwny tv hao wanaotakiwa kunyongwa?

Hao ni wahanga tu,mabosi wao wanazunguka na V8 na hakuna wakuwagusa.
 
ikiwa wiki moja tangu rais kikwete atoe msimamo juu ya mauaji ya albino, tukio hilo limetokea tena huko sumbawanga mpanda, kwa mtoto kukatwa kiganja cha mkono. je, rais aliongea kwa nia ya dhati??

na ni kwel serikali ina nia ya dhati kutokomeza mauaji hayo? na hao watuhumiwa 13 wa kunyongwa rais amekwisha saini?na kwa nini wasionyeshe kwny tv hao wanaotakiwa kunyongwa?
Hao Malbino wamepigana Ikulu Mbele ya Kikwete juzi
 
Unakimbia kwenda wapi.. Baki utetee ndugu zako..kukimbia hakusaidii
 
hakuna jamii ambayo imekosa majanga.kila jamii ina laana yake.ulaya na america wanasumbuliwa na ushoga,

jamii ya waarabu huko middle east inasumbuliwa na jinamizi la kuchinjana wenyewe kwa wenyewe kwa imani kali za kidini.

jamii ya watu wa south america wanasumbuliwa na umasikini,uhalifu na matumizi ya kiwango cha juu cha madawa ya kulevya.

jamii ya watu wa far east kama wachina wanasumbuliwa na sheria kali za ukomunist,hakuna uhuru wa kujieleza nk.

hiyo ni kwa uchache tu.sasa sijui mwenzetu unachukua uraia wa nchi gani ambako hakuna majanga?.
 
Dunia yaleo unaweza kukimbia mkojo ukakutana na kinyesi(m*v)
 
jamani mengine raisi tunamsingizia tu!!!
Yeye anapenda wauwawe???
Yeye ndo anawatumaga???
yeye ni Mungu akae masaa24 kulinda kila albino????
Au mnataka awakusanye maalbino wote awapeleke ikulu kuishi nao???
Yeye ndo mganga mtuma watu viungo???
Yani kuna watu mko kukosoa tu kila wengine wafanyalo
Hao waganga wanaishi nao vijijini mwao wauwaji wanaishi nao pia
Mimi siwezi toka dar nikakate kiungo albino mwanza au bukoba na sijui nampatia wapi
 
Nahisi hili swala la mauaji ya albino lina uhusiano na moja kwa moja na uchaguzi
 
Nimecheka sanaa baada ya kusoma hii post mwisho nimejikuta nalia kwakuwa siku moja nitakuwa rais wa Tanzania nimeona mzigo mkubwa nitakao kuwa nao kuwafanya wananchi kujivunia utanzania wao..

Mwishiwa usinisahau katika ufalme wako Japo kwa ukuu wa wilaya....
 
by Copenhagen DN;
Tatizo la sisi wabongo tukishakula kande na kuvimbiwa tunaingia jamvin na jaaazba. Dogoo wote tunaguswa na mauaji ya ndugu zetu mazeruzeru lakin kuukana uraia huo ni uahini muulize nyani ngabu faiza foxxy na akina chris lukos wanavyohaha. Achaa wewee mara moja!!


cc
Chris Lukosi
faiza Foxy
Nyani Ngabu
njooni mje mmuone jamaa yenu anavyowasema kinafiq!
 
Last edited by a moderator:
Tena hiyo adhabu ikishuka we ndo utakung'utwa kisawia huko ulikokimbilia Maana hata ukikana kwa mdomo damu ni ya Tz,napata wakati mgumu kuhusianisha ID yako,Maana yake baada ya kutafsiriwa kwa kiswahili na maamuzi yako mafupi ya kukimbia tatizo badala ya kulitatua,Sie wengi hatupendi pia na tunaugulia huku tukitamani wauaji wasakwe popote walipo eboo 😡
 
Back
Top Bottom