Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mikoa salama ya kuishi albino ni Arusha na Kilimanjaro ni kweli kabisa huko mara ,rukwa,musoma n.k uchawi umetawala sana
 
Hivi kama baba wa Albino ambaye anatakiwa amlinde mwanae anafanya hivyo serikali imwamini nani. Labda kila Albina awe na mlinzi kama raisi kila mahali anapokwenda awe analindwa na boardguard. Hii vita ni ngumu sana inahitaji nguvu za kiroho zaidi kuliko njia nyingine ili watu wabadili tabia.
 
Si kuna waliohukumiwa kunyongwa hivi karibuni. Pamoja na baba mzazi wa Albino
 
Mauaji ya albino yameanzia katika utawala wako, hadi sasa wameshauawa zaidi ya 70 na makumi wana vilema vya maisha, nimesisimka sana kusoma post ya wiseboy mwana JF mwenzangu,huyu kijana kwangu mimi tangu nimeanza kusoma post zake ni great thinker,anasema ameukana utanzania maana anahofia hasira za Mungu,kwa uelewa wangu mdogo na elimu yangu ndogo huyu hajaukana utanzania bali ameonyesha hisia zake na jinsi gani Tanzania inaongelewa kimataifa japokuwa wengi wetu tuna kasumba ya kukashfu kila post bila kuitafakari kwa kina,rais kikwete muda wako wa kukaa ikulu umeisha,hivi ndivyo unavyotuacha? rais kikwete TISS wana kazi gani nzito hadi wasahau kulinda uhai wa albino? rais kikwete,kama ingetokea mawaziri watano watoto wao ni albino na wakauawa,huu mtandao wa mauaji ya albino ungeendelea kuwepo? rais kikwete unajisikiaje unapokuwa nje ya nchi umekaa na marais wenzako jinsi gani wanavyoifikiria Tanzania? rais kikwete nakuomba usome kumbukumbu la torati 28:15-59.rais kikwete jitokeze uongee kitu,taifa limechoka.
 
na katika kipindi chako wewe jk pia tumeshuhudia mboga ikununuliwa kwa milion kumi
nyoka wenye makengeza wakijigamba hadharani
wadada wenye "ukuu wa wilaya" wakipewa nafasi zao stahiki
konda wa daladala akipewa wilaya kienyeji
ashki majinun zikipatikana mjengoni
wasanii wakikaribishwa ofsin kwako kupongezwa..ila vijana wazalendo wakitoka geita hadi kwako kwa mguu wakifunguliwa mashtaka
mwenzio kuagiza wapigwe tu mana hamna namna
twiga kula pipa hadi uarabuni

aisee serikali yako haitakaa itokee tena hapa ulimwenguni hadi jesus ataporudi
 
Jk sio kiumbe wa kawaida kwanza hana hasira ya maendeleo, haguswi na matatizo yetu, hana hamasa ya kuonesha umahiri wake ktk uongozi, hakosoi viongozi wake hata wanapoonekana dhahir wamekosea labda kwa shinikizo kubwa n.k uongozi wake umekuwa ni dhaifu zaid kutokea tz na Mungu saidia asitokee kiongozi kama huyu. Pongezi kwako Ndg W. Mkapa
 
Mtoa mada ni kweli ndugu zetu albino wanauwaawa sana CKu moyo wangu unaniuma cna pa kulalamikia sababu serikar ambayo ndio kimbilio wamechemsha rasmi kinacho endelea ni maigizo tu utasikia albino wamepigana karibu na ikulu ni sanaa tu.Ki ukweli br Tz sasa ivi matatizo tupu mauaji ya kikatili kupindukia yamezidi @ cku ukosi kuckia/kuona mtu or watu wameuwawa uwaji wa kikatili kupindukia hata ambao sio albino mpaka inafikia mtu anakatwakatwa alafu anachemshwa yule co albino at tz kila kona ni mauaji ya kikatili ya kupindukia Rais uko wapi?, unafanya nini?
 
Last edited by a moderator:
asipojitokeza kuongea lolote juu ya mauaji haya sijui watanzania tunaenda wapi,majuzi rafiki yangu alikuwa Namibia wakati akijitambulisha kwa ktk semina yao yule kiongozi wa mkutano akasema" huyu jamaa anatoka kwa wale wauaji wa albino"anasema alijisikia vibaya hadi akatoka nje ya kikao.
 
Habarizenu,
Nimefikiri sana swala hili,ni kwamba halina majibu au wanaogopwa waganga ,au wanao watuma kufanya hayo mauaji mana,bado sijasikia bado kama wahusika wakuu wakiwa wameshikwa,zaidi ya kushikwa kwa wale wanaotumwa kuuwa,napenda nchi yangu ingeweka mkazo hili jambo,haija pita wiki tanga Mh.Raisi kufanya kikao na walengwa,lakin tena Sumbawanga mtoto amekatwa kiganja cha mkono,hii ni uchungu na uzuni kwa wenye ulemavu wa ngozi kuishi maisha ya sinto fahamu katika nchi yao wao wenyewe.
 
mbona alishalizungumzia hili katika hotuba yake ya mwezi uliopita au ulitaka nini specificaly mkuu. labda atoe amri watuhumiwa kunyongwa hadharani. labda utafurahi.
 
Habarizenu,
Nimefikiri sana swala hili,ni kwamba halina majibu au wanaogopwa waganga ,au wanao watuma kufanya hayo mauaji mana,bado sijasikia bado kama wahusika wakuu wakiwa wameshikwa,zaidi ya kushikwa kwa wale wanaotumwa kuuwa,napenda nchi yangu ingeweka mkazo hili jambo,haija pita wiki tanga Mh.Raisi kufanya kikao na walengwa,lakin tena Sumbawanga mtoto amekatwa kiganja cha mkono,hii ni uchungu na uzuni kwa wenye ulemavu wa ngozi kuishi maisha ya sinto fahamu katika nchi yao wao wenyewe.
Tukio lolote la kishirikina linahusisha nguvu za giza. Tuanzie hapa.
Kukabiliana nalo mhusika anahitaji nguvu ya ziada mbali na akili na zana alizotengeneza. Nguvu hii isitoke upande wa giza kwani haitatatua tatizo. Mchawi mwenyewe akikamatwa kwelikweli anayefanya haya atasema nimeelekezwa na mkuu wa giza. Sasa mapambano haya ni dhidi ya YULE anaewapa hawa wachawi UCHAWI wa kufanya wafanyayo. Inahitajika nguvu ya Mungu kuingilia kati.

USHAURI WANGU KWA KIKOSI KAZI CHOCHOTE KInachowasaka hawa majangiri. Maharifa yote yaliotumika mpaka sasa wachache sn waliokamatwa ni waliotenda bila wahusika wakuu na wateja wa wahusika wakuu. Mnawasaka bila mafanikio wao wanajificha na kuwazubaisha kwa kutumia nguvu za giza. Kuwapata tumieni NGUVU ZA GOD ni nuru. NI hivi watafuteni wanamaombi wanaomwomba Mungu katika roho na kweli; WAAMBIENI MNAHITAJI MSAADA WA MUNGU KUPAMBANA NA TATIZO BILA KUWAFICHA. SIO LAZIMA IWE PUBLIC iwekeni kimkakati. Mtaombewa pia mtafunikwa na damu ya yesu kristo. Hapo wachawi na nguvu zao hazita fua dafu japo watakuekeeni mikwala. MSINIULIZE wanamaombi wanapatikana wapi Intelligensia yenu mkitumia mnawapata. Katika makanisa ya kiroho zipo vitengo maalumu vya MAOMBI na ni bule sio kwa pesa. Mkidaiwa pesa jueni hao sio.
Kuweni kama MAKOMANDO WA VITA. KOMANDO akiona plan A inakataa anageukia plan B na kusikiliza maoni ya wanaemwelewa ADUI.
Serekali haina dini. Lakini nyie KIKOSI KAZI katika kukabili janga hili pangeni mambo yenu maofisini baada ya hapo pita najua wengine mtazarau;
HAYA utamfuata mchawi hivi hivi kwa akili zako wakati ukinyanyuka keshakuona kwenye tunguli zake. Anakutia upofu kesi inaishia hewani. Hata hao wateja wao wakuu wanawaficha kwa hizo nguvu za giza. ILA kwa Mungu hakuna linaloshindikana.
HAO waganga wanaowatuma ndio wachawi wenyewe. Mwingine anajifanya kulaani hilo tukio la kuua albino mchana Lakini usiku wanavyofanya mambo yao WANAAGIZWA NA MAGWIJI kutekeleza nao wanatenda. PRICIPLE ZAO NDIO ZILIVYO TENA HAWARUHUSIWI KUTAJANA.
 
Haya mambo ya uchawi actually ni occultism. Hatujui wazee wetu walikuwa wanafanya nini zamani lakini tukisoma grimoire tunaweza kupata idea kuhusu magic. It all has an occult purpose. Ni mambo yale yale yanayozungumziwa na occultists kama lobsang rampa. Huu uwindaji wa albino ni uchawi ambao umepoteza dira na mwelekeo. It just has to be sanitised. Mchawi anacho kitabu chake cha kazi kinaitwa grimoire. Sananda anasema hii grimoire is hdndwritten by the witch. Hakisomi tu bali anakiandika kwa mkono wake.
 
Binadamu amefikia kiwango cha juu cha ukatili dhidi ya ubinadamu.utuwa binadamu umekuwa chini ya pesa.tumrudieni mungu.
 
mbona alishalizungumzia hili katika hotuba yake ya mwezi uliopita au ulitaka nini specificaly mkuu. labda atoe amri watuhumiwa kunyongwa hadharani. labda utafurahi.

Kulizungumzia Ktk Hotuba Zake Hajaanza Leo Mkuu,kinachotakiwa Ni Kauli Nzito Ya Mkuu Wa Nchi Kuwa Kamwe Haitakaa itokee tena Albino Kuuawa,na Serikali Yake Imejipanga Kwa Hilo,albino Wote Tanzania Ktk Kila Wilaya Mbona Inawezekana Kabisa Wangelindwa Na Kamati Ya Ulinzi Ya Wilaya Tu Na Si Taifa Hata Hilo Limeshindikana?
 
Back
Top Bottom