Bueno
JF-Expert Member
- Sep 9, 2022
- 4,114
- 6,449
Ni pale aliporejea Zanzibar baada ya kutia sahihi Muswada huo, Karume alipofafanuliwa na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Wolfgang Dourado, kwamba kile alichotia sahihi ni Hati ya kujinyonga yeye na Zanzibar, kwa kukubali kuingizwa kwenye Muungano jambo kama hilo muhimu kwa uchumi wa Zanzibar; lakini wapi, alikuwa amechelewa.Wapenda umbea tafuteni hii “Karume aliuliwa sababu ya Muungano”.
Kama kawaida, hilo halikumnyima usingizi Karume; aliendelea na Mpango wake wa kuanzisha BoZ na mambo mengine ya fedha, kwa kuteua Tume kuanzisha mchakato huo kwa chukizo la Serikali ya Muungano iliyodai (Karume) alikuwa akivunja Katiba kwa jeuri na kiburi.
Aliyekuwa Waziri wa Fedha wa Muungano wa wakati huo, Amir Habib Jamal, katika barua yake ya 18 Machi, 1966 kwa Waziri Twala, aliweka wazi msimamo wa Kikatiba dhidi ya “jeuri” ya Karume kwa kusema, “Gavana wa BoT atakuwa ndiye mwakilishi pekee wa Tanzania na Zanzibar kwenye vikao vya EACB; mgawo wote wa mali na au faida utakaofanywa na EACB kwa ajili ya Tanzania na Zanzibar, utalipwa na kuchukuliwa na Serikali ya Muungano”.
Na kuhusu BoZ, Jamal alisema, “Benki hiyo inaweza kuanzishwa kama Benki nyingine ya kawaida chini ya Sheria za Zanzibar kufanya shughuli zisizokuwa za Benki Kuu”.
Zanzibar yasalimu amri
Ubishi wa Zanzibar ulifikia kikomo mwaka 1966 baada ya kuanzishwa kwa BoT, pale Sheria ya Benki na Sheria ya Udhibiti wa fedha za Kigeni (the Banking Ordinance” na “The Exchange Control Ordinance” – Cap 139), zilipofanyiwa marekebisho kuweza kutumika pia Zanzibar.
Jamal, kwa kuhuzunishwa na msimamo mkali wa Zanzibar na Karume, wa kuendeleza mchakato wa kuanzisha BoZ kwa Amri ya Rais Karume, chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma (Zanzibar Public Enterprises Decree, 1966), katika barua yake Kumb: TYC.46/08 ya 23 Machi 1966, kwa Serikali ya Zanzibar alisema, hatua hiyo ni ya “kuvuka mipaka na isiyokuwa na nguvu ya Kisheria kwa kuzingatia Katiba ya Muda/Mpito ya Muungano”.
Kwa kusalimu amri na shinikizo, ilibidi Benki ya Zanzibar ianzishwe kama Kampuni binafsi, na kuitwa “Benki ya Watu wa Zanzibar (The People’s Bank of Zanzibar – PBZ) yenye Wanahisa wawili, mmoja wa wawili hao akiwa Karume mwenyewe.