Mauaji ya Karume 1972: Je, muuaji aliwahi kukamatwa na kushitakiwa?

Mauaji ya Karume 1972: Je, muuaji aliwahi kukamatwa na kushitakiwa?

Jamani huo Uzi unaoelezea haya mapinduzi uleteni please
 
Gaidi Mbowe atakuwa alihusika kwnye haya mauaji, achunguzwe vizuri... nipo tayari kutoa ushahidi... hahahaah!
 
Muuaji alikuwa ni shemeji yake,(mdogo wa mkewe) ambaye huyo mkewe alikuwa anatoka ktk ukoo wa waarabu (sultani) ambao waliponduliwa na Karume, umeelewa!? Sasaa...

Kwa mapenzi kwa mkewe au labda ilikuwa ni njia ya kuwapooza mkewe na shemejie,
Baada tu ya mapinduzi alimpandisha shemeji yake vyeo vya kijeshi harakaharaka, ndo maana hata wakati anaenda kumuua karume aliwapita walinzi wote wa raisi huku akiwa na smg ndani ya koti!

Alienda mpaka hazizidi m.5 kabla hajafika alipokaa karume na wenzake, akafyatua risasi kadhaa!

Na yeye aliuawa kwa risasi na walinzi wa raisi pale pale.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kidogo kuna ukweli lkn kuna maeneo umekosea
 
Naomba nihame kidogo
Hiv ni kwann nchi alipewa karume na sio okello na baada ya mapinduzi okello alienda wap na pia je kama kiongozi wa mapinduz SMZ ilimpa reward gan
Na uraia wake ulikua sababu ya yy kukosa nafasi SMZ
labda tuanzie huku kabla ya kufikia tukio hlo la uhaini

Sent using Jamii Forums mobile app
Karume, Babu , Hanga na wengineo ndo waliopanga Mapinduzi. Okello alikua ni askari wa kukodi tu au unaweza kumuita mamluki. Hakuhusika kwenye kupanga hayo mapinduzi na wala hakujua chochote. Kinachofanya watu wamuone ni mhusika ni kule kujitangaza kwenye radio na kuranda randa mitaani kutisha watu baada ya Mapinduzi. Okello alirudishwa kwao Uganda baada ya kuonekana anataka kuwa juu ya wenye mapinduzi yao.
 
It was personal issue na mambo mengine.
Huyu Mahmoud aliuliwa babaake kabisa.
Na mambo kibao mengine ya uonevu yaliendelea huko kisiwani.
Alijitoa muhanga tu.
 
Wapenda umbea tafuteni hii “Karume aliuliwa sababu ya Muungano”.
Karume aliongoza chama cha Afro-Shirazi kupinga muungano wa utawala wa Kiarabu ulioonekana kuwa na lengo la kudumisha utawala wa kisiasa na kiuchumi wa jamii ya Kiarabu.
 
Wapenda umbea tafuteni hii “Karume aliuliwa sababu ya Muungano”.
Karume alichukua hatua yake ya pili muhimu ya kisiasa alipokubali kuunda Muungano na Rais wa Tanganyika Julius Nyerere Aprili. Muungano huo umesababisha nchi mpya iitwayo Tanzania.

Jamuhuri ya Muungano wa Watu wa Tanganyika na Zanzibar

Ilibidi itamkwe hivyo
 
Wapenda umbea tafuteni hii “Karume aliuliwa sababu ya Muungano”.
Karume hakujali mgawanyo wa mamlaka na madaraka kati ya yale ya Muungano na yale ya Zanzibar. Ukiacha mambo ya Nje, Zanzibar iliendelea kudhibiti kivyake madaraka na mambo yote juu ya Uhamiaji, Biashara ya Nje na Mikopo, Utumishi wa Umma, Bandari, Posta na Simu, Jeshi na Usalama wa Taifa ambayo vinginevyo yalipashwa kusimamiwa na Serikali ya Muungano. Na kwa chukizo kwa Nyerere, alitangaza kuwa asingeruhusu uchaguzi kufanyika Visiwani kwa miaka 50; akatangaza ukuu (supremacy) wa Chama cha Afro Shirazi (ASP) kuwa juu ya taasisi zote, ikiwamo Katiba ya Jamhuri ya Muungano na taasisi zake. Kana kwamba alikuwa akiimarisha Taifa huru la Zanzibar nje ya Muungano, Amri yake (Decree) juu ya ukuu wa ASP ilianzisha Idara za Jeshi, Usalama wa Taifa (la Zanzibar), Polisi, Vijana, kina mama wa ASP ili kwamba mambo hayo yashughulikiwe kiserikali chini ya idara husika nje ya Muungano.
 
Wapenda umbea tafuteni hii “Karume aliuliwa sababu ya Muungano”.
Kufika mwaka 1971, Vyeo kama “Rais wa Zanzibar” (chenye kutambuliwa na Katiba ya Muungano), Mawaziri na Manaibu Mawaziri, vilibadilishwa kuitwa “Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi” (badala ya Rais), Mawaziri na Manaibu Mawaziri wakaitwa Wenyeviti na Manaibu Wenyeviti wa Idara; yote haya ilikuwa ni chenga kimamlaka kufanya Katiba ya Muungano isiwe na pa kushika kiutawala Visiwani.

Kufikia hapo, ASP kilikuwa ndiyo Serikali na Serikali ilikuwa ndio ASP wakati ikifahamika kwamba, Vyama vya Siasa (ASP na TANU) havikuwa jambo la Muungano. Ikumbukwe kwamba, wakati huo Zanzibar haikuwa na Katiba ambapo ilitawaliwa kwa Amri (Decrees) za Rais zisizohojika.
 
Wapenda umbea tafuteni hii “Karume aliuliwa sababu ya Muungano”.
Na vivyo hivyo, Jamhuri ya Muungano ilitawaliwa na kuongozwa kwa Katiba ya Mpito (Interim Constitution) ambayo ilimpa madaraka Rais wa Jamhuri ya Muungano, kuifanyia marekebisho kadri alivyoona inafaa katika kipindi cha mpito cha mwaka mmoja kuelekea Katiba ya kudumu, isipokuwa kwa mambo kumi na moja ya Muungano (kutopunguza au kuongeza) yenye kulindwa na Mkataba wa Muungano (Articles of Union), uliotiwa sahihi na waasisi wake, Aprili 22, 1964.

Kitendo cha Karume kuendelea kudhibiti baadhi ya mambo ya Muungano Visiwani, kilitafsiriwa kuwa cha mabavu na “usaliti” kwa Muungano.

"Yuda unamsaliti mwana wa Adamu kwa kumbusu?"
 
Wapenda umbea tafuteni hii “Karume aliuliwa sababu ya Muungano”.
Baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana mwaka 1964 katika kipindi hiki cha mpito kwa nchi hizi kuanzisha Benki Kuu na sarafu yake, mgogoro mkubwa ulizuka kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar juu ya mambo matatu: la kwanza, ni kama Zanzibar iendelee kuhudhuria au la, vikao vya EACB kama nchi; pili, kama Zanzibar bado ilistahili gawiwo la faida kutokana na uwekezaji wake baada ya EACB kuvunjwa.

Hoja iliibuliwa pia juu ya nafasi na hadhi ya Zanzibar (kama nchi ndani ya Muungano) kuhusiana na mambo ya fedha chini ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliyokusudiwa; na mwisho, hadhi ya “Benki Kuu ya Taifa la Zanzibar” (BoZ) iliyotarajiwa kuundwa, ndani ya Muungano.

Maokoto_
 
Wapenda umbea tafuteni hii “Karume aliuliwa sababu ya Muungano”.
Tangu kufikiwa kwa Muungano, Aprili 26, 1964; na kufuatia kuvunjika kwa EACB, Zanzibar ilikuwa na shauku hai ya kuanzisha Benki Kuu (BoZ) yake. Wizara ya Fedha Zanzibar, chini ya Waziri makini Abdulaziz Twala, ilianza mchakato huo kwa kupeleka vijana nchini Ujerumani Mashariki kwa mafunzo ya Fedha na Usimamizi wa Fedha, Ukaguzi na shughuli za Benki.

Na katika kuhakikisha kwamba akiba yake ya fedha za kigeni haikodolewi macho wala kuguswa na Serikali ya Muungano au Benki za Kiingereza, Zanzibar ilihamisha haraka jumla ya pauni za Uingereza 700,000 kutoka Benki ya Uingereza ya Grindlays, kwenda “Norodony Moscow Bank”, Tawi la London, Uingereza; kitendo ambacho kililaaniwa vikali na Serikali ya Muungano.

Maokoto again_
 
Wapenda umbea tafuteni hii “Karume aliuliwa sababu ya Muungano”.
Ukwasi wa Zanzibar, ikilinganishwa na Tanganyika, ulikuwa wa kiwango cha juu wakati wa Karume kutokana na bei nzuri ya karafuu katika soko la dunia, ambapo ilipanda kutoka dola za Kimarekani 550 hadi dola 1,500 kwa tani, kiasi kwamba kufikia mwaka 1971, Zanzibar ilikuwa na akiba ya fedha za kigeni ya pauni za Uingereza (£) 14,000,000, ikilinganishwa na 6,500,000 za Tanzania Bara.

Akiba hiyo nono, mbali na kutokana na bei nzuri ya Karafuu, ilitokana pia na Serikali ya Zanzibar kuwapunja wakulima bei ya mazao yao kwa kuwalipa asilimia 10 tu ya bei, na sehemu kubwa ya mauzo kubakia Serikalini.

Kwa mfano, wakati karafuu iliuzwa kwa bei kati ya sawa na shilingi 14/= [Indonesia] na shilingi 21/= [India] kwa ratili, mkulima alilipwa na Serikali ya Zanzibar bei ya Shs. 1.50 tu kwa ratili; wakati huo, kwa Tanzania Bara na nchini Kenya, bei kwa mkulima ilikuwa kati ya shilingi 8/= na 10/= kwa ratili.

Wazanzibari walioumizwa zaidi ni Wapemba wa Visiwa vya Pemba ambao ndio walikuwa wazalishaji wakubwa wa karafuu Visiwani.

Maokoto_
 
Wapenda umbea tafuteni hii “Karume aliuliwa sababu ya Muungano”.
Ukakasi juu ya ushiriki au la, wa Zanzibar katika EACB, umiliki wa hisa, gawiwo la faida za EACB na kuhusu uanzishaji wa BoZ kufuatia Muungano na Tanganyika, ulimalizwa na Katibu wa EACB, H.R. Hirst, katika ufafanuzi wake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha wa Serikali ya Muungano wa wakati huo, D. Namfua, akisema, “Katiba ya Mpito ya Jamhuri ya Muungano, haikuhamishia mambo ya Fedha na Sarafu ya nchi hizi kwa Serikali ya Muungano na hivyo uanachama wa Zanzibar wa EACB haukuathirika”, akimaanisha kuwa, mambo ya Fedha na Sarafu hayakuwa ya Muungano hivi kwamba kila nchi ilikuwa na uhuru wa kuwa na Benki Kuu na sarafu yake.

Tanzania Bara na Uingereza, kupitia Mjumbe wake katika EACB, J. B. Loyness, zilitaka ima faima, Zanzibar iondolewe kwenye EACB kuanzia kikao cha Septemba 8, 1964; lakini Hirst, mapema Januari 1965 baadaye, akawashushua kwa kumwandikia Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Fedha, Edwin Mtei, kumtaka nchi yake kuheshimu nafasi ya Zanzibar.

Maokoto_
 
Mkuu kitabu safi hiki,kilipelekea kupata hii ID name yangu licha ya kuwa nimeshafika sehemu tajwa ya ID ila mchango wake kwenye Uhuru wa Zanzibar uliniongezea maarifa!
Kuna Documentary aliandaa Mwandishi Na Mwanahistory Mohamed Said kuhusu Kipumbwi
 
Wapenda umbea tafuteni hii “Karume aliuliwa sababu ya Muungano”.
Ule ukweli kwamba mambo ya Fedha, Sarafu na uhalali wa Zanzibar kuanzisha BoZ hayakuwa mambo ya Muungano wakati huo, uliipa matumaini na haki isiyohojika kuweza kunufaika na kile ilichowekeza kwenye EACB kabla na baada ya Muungano, jambo ambalo halikupokelewa vyema na Serikali ya Muungano.

Bila Zanzibar kufahamu, Mwalimu Nyerere aliwaita kwa siri wanasheria wake, wakiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Roland Brown, na kuwaelekeza “wafanye kitu” juu ya Zanzibar isiendelee kutamba kwa fedha zake.

Roland Brown ndiye huyo huyo aliyeelekezwa na Mwalimu kabla ya hapo mwezi Aprili 1964, kuandaa kwa njia ya dharura, Hati ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar “bila mtu mwingine yeyote kujua”, baada ya juhudi za Mwalimu za kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki (EAF) kushindwa na kugeukia Muungano finyu kati ya Tanganyika na Zanzibar badala yake.

Taarifa za wakati huo zinaonesha kwamba, katika mazingira hasi na hatarishi kwake, Karume alishinikizwa kutia sahihi Hati hiyo ambayo baadhi ya mambo yaliyomo aliyakana baadaye kwamba alidanganywa au kuchengwa kutokana na yeye kutojua lugha ya Kiingereza ndani ya Hati hiyo, ikizingatiwa pia kwamba alinyimwa ushauri wa kisheria, baada ya kulazimishwa kumpa likizo ya lazima ya siku saba, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Wolfgang Dourado hadi mchakato wa Muungano ukamilike.

Haraka haraka ukaandaliwa Muswada wa Marekebisho ya Katiba (The Interim Constitution Ammendment Bill; baadaye kupitishwa kuwa Sheria Na. 21 ya 1965) kufanya sarafu, Fedha za Kigeni na udhibiti wake kuwa mambo ya Muungano ili kuwasilishwa Bungeni kupitishwa kuwa Sheria.

Maokoto_
 
Wapenda umbea tafuteni hii “Karume aliuliwa sababu ya Muungano”.
Muswada wa Marekebisho ya Katiba kufanya mambo ya Fedha na Sarafu kuwa ya Muungano uliwasilishwa kwenye Bunge la kawaida, tarehe 10 Juni 1965, na kupitishwa kwa kasi isiyo kawaida. Wakati huo, Mwalimu Nyerere alikuwa safari nje ya nchi.

Kutokana na Mwalimu kutokuwepo nchini, mzigo wa kutia sahihi Muswada huo kuwa Sheria ulimwangukia Makamu wa Kwanza wa Rais, Sheikh Abeid Amani Karume kwa wadhifa wake kama Kaimu Rais wa Jamhuri ya Muungano kipindi hicho. Siku hiyo, Juni 10, 1965, mjini Dar es Salaam, Karume aliwekewa mezani Muswada huo; naye bila ya kuhisi chochote, alitia sahihi hima Muswada huo kuwa Sheria na kuanza kutumika siku hiyo hiyo ya kupitishwa na Bunge na kabla hata wino haujakauka.

Ni dhahiri Karume hakujua (kama ambavyo tu hakujua alipotia sahihi Hati ya Mkataba wa Muungano mwezi mmoja kabla ya hapo) alichokuwa akitia sahihi. Wala Wabunge kutoka Zanzibar kwenye Bunge la Muungano, siku hiyo, hawakujua madhara ya Muswada waliopitisha kwa Zanzibar. Chini ya Marekebisho hayo, michango yote ya Zanzibar, hisa na mapato ya riba kwenye EACB, yalifanywa kuwa mali stahiki ya Serikali ya Muungano.

Bado kuna ukinzani wa kisheria miongoni mwa wanasheria kuhusu uhalali na uwezo wa Bunge la wakati huo, wa kufanyia marekebisho Katiba ya Mpito ya mwaka 1964, kwa kuongeza jambo la Fedha kuwa la 12 juu ya Mambo kumi na moja asilia ya Muungano.

Maokoto_
 
Back
Top Bottom