Mauaji ya Polisi wetu ni Ujambazi, Ugaidi au Retaliation? Nini kifanyike kukomesha hali hii?

Point namba mbili ya waislam..
Anaetakiwa kuboresha maisha ya wananchi ni serikali na sio mashehe,hao mashehe wenyew wapo hohe hahe watawaambia nn wananchi?
Sio kila sheikh ni kada wa ccm kama Alhadi Mussa Salim.

Sema hivi,serikali ikae chini na wananchi wake,kwanza wajue tatizo lipo wapi na watashirikiana vipi
 
Nàshauri tena,Mhe.Magufuli mteua DCI mstaafu Balozi Adad Rajab kuwa waziri wa mambo ya ndani.
 
Police wajikite na usalama wao hali sio salama tupo busy kutoa wanajeshi wetu kwenda Congo wakati hapa kwetu mauaji ya police yakishika kasi...mbaya sana hii inatakiwa kiundwe kikosi kazi haswa sio hao hao wakamate viroba,risiti za TRA hao hao tena wawepo katika kikosi cha kuzuia ujambazi mkubwa..
 
Ndani ya week isiyozid mbili au si zaid ya siku kumi wahusika watapatikana wakiwa hai
 
Wako bize kuteka wapinzan na wasanii wakati IS wanafanya yao!
 

Mkuu Paskali! Kwa kweli nami nimesikitishwa sana na hii kadhia. Wakati umefika sasa wa Ngosha MAGU kuteua IGP kutoka jeshini, kabisaa!
 
Does not this sound a little strange? 7pple where killed and barred unknowingly, and just a day after 7 police killed? Does this not sound like a retaliation or a revenge? Serikali iwe makini na kujua rais anatakiwa kuwa moja lkn kuna wengi wenye uwezo zaidi yake. Anaongoza watu na sio wanyama.
 
Mwenyewe nimeumia mkuu,ila ukisema no prosecution,no kesi ni kifo moja kwa moja huoni watu wataitumia hiyo chance vibaya?police wakiwa na uhusiano mzuri na wananchi , majambaz hayatafurukuta hata kidogo!
 
USHAURI WANGU ISSUE HII SASA IKABIDHIWE JWTZ FOR ACTION ! TUSICHEZE NA NYANI TUTAVUNA MABUA !
 
Thanks very objective.

Paskali
 
Uonevu wa polisi ndio sababu ya haya yote
Mimi waliwahi nipiga faini 2 bila sababu kisa tu nimewapa leseni wakaniandikia bila kunisikiliza
Siku ingine tena wakaniandikia bila nisikiliza
Wakachukua 200000 yangu ili waniachie
Wamekula hela nyingi kisa gari kupata ajali
Wanapiga watu kama sio wanadamu

Wanabambikia watu kesi
 
Hapa nilipo nangojea nije nisikie kauli ya Waziri aliyekwishajikatia tamaa Mwigulu Nchemba kuhusiana na hili sakata ndipo nitachangia huu uzi.
 
Nguvu zinazotumika kuwateka watu wasio na hatia na kuwatesa zingetumika kupambana na magaidi hawa tungefika mbali
 

Ni msiba pole wafiwa.
Adhabu ya papo kwa papo itazidisha mauaji...Principle ya tit for tat au jino kwa jino Haifai kwa sababu hio ni jungle law
Hili sio mara ya kwanza wala ya pili. Ni matudio na tunakumbuka ya Sitaki Shari ilipo vamiwa.
Sina uhakika na mafunzo ya polisi wetu kwa sasa jee ni ya kukabiliana na wapinzani tu ? Jee wanafundishwa sayansi ya investigation ya kisasa?
Mara nyingi yanapo tokea matokeo kama haya polisi wetu huta target wavaa kanzu...kuvamia misikiti na kukamata wenye ndevu....na tangu wafanye hivi hawajawahi kuthibitisha kesi hizi..
Hata hili utaona watu wanasema ugaidi..na ukisha sema ugaidi basi ujue kuna wenye ndevu na kanzu watavo teswa na kukamatwa hovyo.
Na haya hayakuwepo miaka ya nyuma hasa polisi wetu walipokuwa wakifunzwa na walimu na nchi rafiki.
Nadhani mentality ya polisi wetu imebadilishwa na mafunzo wanayo yapata kutoka kwa US ambao mara nyingi kwa sasa ndio role model wetu.
Kwao US uhalifu wa kama hivi ukitokea kwao basi mshukiwa wa mwanzo ni waislam ....sasa hivi fikra zao ndo wanapandikizwa askari wetu.
Mimi nadhani bado hayujapata chanzo cha jinai hizi...
Na hii ndio kazi moja wapo ya vijana wa Intelligence TISS wafanye uchunguzi wa kisayansi kutaguta chanzo , nani anahusika na kwa malengo gani. Huku ndio kunawahusu TISS na sio kawa Roma mkatoliki.

Kusema tu ni magaidi na kuanza kuvamia misikiti na masheikh haku ondoi tatizo kwa sababu tuna end up kukamata wrong person kwa sababu tu ya hisia za mafunzo walopata.
Pia tujiulize why polisi tu ? Sio magereza wala jeshi wala mgambo wala raia wa kawaida?
Jee polisi wao kwa wao hakuna chuki baina yao ?
Ndio maana nikasema Tiss iingie kufanya uchunguzi wa kina na kuukabidhi serikalini.....ili tukomeshe jinai hii kujirudia.
 
Kaka kwa taarifa yako asilimia kubwa ya Polisi Jamii ilipoteza MWELEKEO. Kama ilivyokuwa jeshi la mgambo kukamata maliza za watu na kuishia kugawana hadharani.
 
Hao ni magaidi. Tofautisheni Kati ya magaidi na majambazi. Duniani hakuna jambazi wanaopanga ambush kwa police. Kwanza ni marafiki wa siri na wanaishi kwa kutegemeana. Ukiona jambazi anauawa ni kwamba ameenda kupiga kazi bila kutoa taarifa, au amepiga kazi na hajatoa mgao. Wale ni magaidi, na ni walewale ambao wenzao waliovamia kituo cha polisi ukonga. Wanaanza kujireorganize
 
Mh Shibuda Leo umeongea points...

Tangu lini mpenda pombe akatambua jema na baya? Usilazimishe watu wote wafikiri kama wewe ndiyop uone wanasema point. Umuhimu wa hoja unategemea na wewe umesimama wapi na unataka kwenda wapi.

Hakuna siku dunia watu wote wanawaza na kuwa na chaguo moja. Unapashwa kupima hoja kwa kuzingatia universality na siyo wewe utakavyo.
 
Hawa jamaa wanaweza kuchukua hiyo zone kirahisi sana mana tunakoelekea polisi watagoma kwenda huko na waliopo wanaweza wasiende makazini sababu ya hofu
 
Hao vilema viwete nk watakuwa walipanda Lori hali wakiwa hivyohivyo au walikuwa wakigombana wenyewe kwa wenyewe wakati safari inaendelea au walitaka Kuwaibia wenzao kwenye gari wakala mkong'oto.[emoji12]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…