Mauaji ya Polisi wetu ni Ujambazi, Ugaidi au Retaliation? Nini kifanyike kukomesha hali hii?

Serikal inajitakia yenyewe coz wakiambia tujadil suala la utekaj na uvunjifu wa aman bunge linapga chini madhara yake ndio hayo wanadharau mambo madogo yanazaa makubwa ona mwaka jana waliuwawa pols watatu dar na jana polis sita apo kifuatacho si unaeza sikia tena kituo kizima cha polis kimetekwa
RIP KWA POLISI WALO TANGULIA MBELE ZA HAKI
 
Tulishasema huko nyuma kuwa kuminya uhuru wa watu kujieleza wanaopewa na katiba unaweza kuzalisha ugaidi
 
Our country isn't safe any more guys
 
Ni hasira za wananchi juu ya ufuska wa serikali, gaidi anaua wote polisi na raia ila hawa ni watu wema kwa raia ila polisi na serikali mjiandae simmesema tujifunze Uganda Burundi na Rwanda ?let's go
 
Acha unafiki na wewe kwa kujifanya humjui aliyetufikisha hapa .
Duh ndo tumefika huko?
Siasa zisitufikishe huko wandugu.
Ndugu zetu wanauawa na magaidi tunaleta siasa za kijinga.
No!lazima tubadilike...
Na hao magaidi watatumia udhaifu huu kutuangamiza kabisa.
Nasema tena hao sio majambazi ni magaidi!
Na wameandaliwa miaka mingi tu kwenye baadhi ya Nyumba za ibada ambazo zimeshapigiwa kelele humu humu.
Kuwapeleka somalia wamewapeleka wengi tu.
Walichokuwa wanasubiri ni mgalatia kuingia madarakani.
Niliwaambia hili muda mrefu
 
Umenena kuntu mkuu....big up
 
Ni Ugaidi(Kulipiza Kisasi),Jeshi Letu Lijisahihishe kuondoa uhasama kati ya Raia na Wao.
Sidhani kuna raia gani mwema akiharasiwa na polisi anakimbilia kupora silaha polisi na kuua. Basi ni bora aue tujue moja. Lakini uporaji wa silaha...! Hapana huyo ni jambazi au GAIDI. Lakini sio raia. (Ukipanda Mbeki shambani kwako au nyumbani kwako elewa jambo moja tu, kama Honda make hutalila wewe basi atakula mwanao au mjukuu Wako. Too maneno ya chuki dhidi ya serikali yanayopandikizwa na upinzani, mazao yake yataliwa na haohao wapinzani nyakati hizo nchi haikaliki wala haitawaliki) PASAKA NJEMA.
 
Naona rate ya vifo imekua juu mno,ina maana hawakuweza kupata mda wa kujibu hadi wakamalizwa wote.?
Je zile bulletproof na kofia za chuma hawakuwa wamevaa?,maana FFu mi huwaona wamevaa bulletproof na ile kofia ya chuma kwa lengo la kuzuia risasi,na ukivaa vile ili mtu kukumaliza lazima akulenge usoni na hawezi kama gari inatembea labda abahatishe,lakini hawezi kubahatisha kwa idadi yote ile.
Je hao polis walikuwa slow kureact baada ya ripoti ya mwanzo ya mlio wa risasi na kugundua kuwa wako under attack?
Au kama kawaida yao bunduki walikuwa wameziweka chini wakati wao wakiwa wananinginia kwenye bomba za defender?

Sijui inakuwaje wanajisahau,askari inatakiwa urelax ukishatoka kazini na unaingia kulala kitandani,mda wote inatakia kuwa macho,na mnapokuwa kwenye gari mko wengi kila mtu aangalia maeneo yanayowazunguka wakati mnapokuwa mnapita kitu kitakachowawezesha kuona tishio mapema kabla halijatokea,
sasa mko kwenye gari,silaha mmezilaza chini,mnaning'inia kwenye bomba huku mko busy kupiga story za manchester united,wala hamjali kutupa jicho huku na kule kucheki usalama,matokeo yake ndo haya,,

i wish i could be RPC
 
we unachekesha serikali iko inaangalia shilawadu, na selikali inapenda sana wimbo wa dume suruali. hatuna selikali wala bunge. twende hivyo hivyo liwalo na liwe
 
Awali ya yote natoa pole kwa Familia ambazo zimepoteza Ndugu,jamaa, na hata Marafiki. Tukio hili limenishtua sana kila mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi hii atakuwa ameguswa kwa namna moja au nyingine japo kuna watu vichwa vibovu kiukweli wanasikitisha na kushangaza kabisa namna wanavyocomment,! Hawa Polisi ni Ndugu zetu,Majirani zetu na hata Rafiki zetu. Jeshi la Polisi sasa liache kucheka na majambazi, wafuate maelekezo ya Mkuu nategemea kusikia vifo vingi vya Majambazi kuanzia sasa, Majambazi si Wa kupeleka mahakamani maana kule tunajua, watu hutishiwa kutoa ushahidi kwa kuhofia maisha yao matokeo yake yanarudi mtaani yakidunda.,, hapa kikubwa ni kuyaua tu ikiwezekana hata hadharani .. Hapa hautosikia haki za binadamu wakijitokeza kusemea hili la Jana.

Jambazi hastahili kuishi anastahili kufa......
 
Reactions: UCD
Ni kweli kwamba ujambazi upo tena kwa kiwango cha hali ya juu sana. Lakini bado siamini kwamba haya yanayoendelea ni ujambazi bali ni retaliation. Yako mambo ambayo yamekuwa yakijitokeza hapa nchini katika siku za hivi karibuni ambapo raia wametekwa na kuteswa wananchi na vinavyodaiwa ni vyombo vya ulinzi na u salama. Je hatuna wataalamu wa kuchunguza na kutambua the real course? Au intelligence zetu ziko sensitive kwa lema na Tundu pekee. I think it's high time we became serious ili kujua chanzo halisi. This is our country tuipende na kuijenga kwa pamoja
 
Hao watu unaota wapewe haki ya "license to kill" wana elimu, uwezo gani yakuweza kupambanua mambo kwa haraka.?

License to kill in Tanzania ni kutangaza vita na wananchi.
 
Tatizo wananchi hawatoi ushirikiano ili kujenga jamii bora duniani
 
Magufuli alitoa go ahead kwa police kuua majambazi,kikaja kile kimama cha tume ya haki za binadamu na wanachama wake ambao ni chadema wakapinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…