christelly
JF-Expert Member
- Dec 29, 2016
- 1,462
- 1,466
Na bado ,kila cku nawaambia uvumilivu wa binadamu yeyote huwa na mwisho....nilikuwa najiuliza siku nyingi hivi MTU unawezaje kuwa gaidi na kujitoa muhanga ???? Haki kwanza ndiyo amani hufuata ,not vice versa!!!!Kisifanyike chochote juzi kuna Wabunge wameomba hilo swala lijadiliwe bungeni kuna wanawake jenista mhagama na mwenzie bila hata aibu wanasema ni uchochezi!
Yakasikika makofi ya Wabunge wa ccm waaaa...waaaa....waaaa....
Acha tuendelee hivi hivi
Wanabodi,
Taifa bado liko kwenye shock ya nini haswa kilichotokea kwa askari wetu?.
Mauaji haya ya Polisi Wetu ni Ujambazi tuu, ni Ugaidi au Retaliation?. Wakati vyombo vya uchunguzi vikiendelea na kazi yake, Sisi Watanzania kama taifa lazima tujiulize, Nini Kifanyike Kukomesha Hali Hii?,
Kwanza nikiri nimesikitishwa na vifo hivi vya vijana wetu askari polisi kushambuliwa na kuuwawa na majambazi wenye silaha.
Swali ni jee huu ni ujambazi tuu wa kawaida, uvamizi kwa lengo la kuiba silaha, ni ugaidi, ambush au nini haswa?.
Hili kuwaweka polisi wetu kwenye risk na kuwa an easy target, kwa majambazi wanaotumia silaha, niliwahi kulizungumza hapa kwa kirefuhttps://www.jamiiforums.com/threads/hili-la-polisi-kuruhusiwa-kuwanyanganya-silaha-majambazi-na-kupandishwa-vyeo-limekaaje.1071133/page-5
Kwa tukio kama la jana,jee mnadhani huu sasa ni wakati muafaka wa kuzibadili sheria zetu za jeshi la polisi ili kuwalinda polisi wetu wawe licenced to kill officially na serikali itangaze rasmi kuwa ujambazi wa kutumia silaha adhabu yake ni kifo cha papo kwa papo, no prosecution no kesi, bali ni hukumu ya kifo there and then ili kuwaogofya kabisa majambazi wote wanaotumia silaha wasithubutu?!.
Kama ni ugaidi au retaliation, tufanye nini?.
Natoa pole kwa rais wetu wa JMT, waziri wa Mambo ya Ndani, IGP na familia za askari hao!
RIP Askari Wetu.
Nini Kifanyike? .
Ijumaa Kuu Chungu!.
Paskali
Nawe kesho utauawa, you will be mistaken, kuna mtu atakupigia mwizi utauawa, acha kuongea kama hujaenda shule. You will be mistaken for a jambazi and you have it! Waingereza hizi taratibu waliziweka after a long time of experience and public chekability............. then they created those concepts and went on to teach them formally and informally!Awali ya yote natoa pole kwa Familia ambazo zimepoteza Ndugu,jamaa, na hata Marafiki. Tukio hili limenishtua sana kila mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi hii atakuwa ameguswa kwa namna moja au nyingine japo kuna watu vichwa vibovu kiukweli wanasikitisha na kushangaza kabisa namna wanavyocomment,! Hawa Polisi ni Ndugu zetu,Majirani zetu na hata Rafiki zetu. Jeshi la Polisi sasa liache kucheka na majambazi, wafuate maelekezo ya Mkuu nategemea kusikia vifo vingi vya Majambazi kuanzia sasa, Majambazi si Wa kupeleka mahakamani maana kule tunajua, watu hutishiwa kutoa ushahidi kwa kuhofia maisha yao matokeo yake yanarudi mtaani yakidunda.,, hapa kikubwa ni kuyaua tu ikiwezekana hata hadharani .. Hapa hautosikia haki za binadamu wakijitokeza kusemea hili la Jana.
Jambazi hastahili kuishi anastahili kufa......
Nionavyo mimi ni makundi ya maharifu yanakusanya silaha.
Halfu kitu kingine kule yanakotokea haya ni kule kule kwenye pwani isiyokuwa na ulinzii. Ulinzi uimarishwe katika njia chocho za bahari.
Ninaomba JWTZ wafanye operation maalumu katika misitu iliyokatika maeneo hayo. Kunaweza kuwa na kambi maalumu ya uahrifu.
Tatu viongozi wa dini ya kiisilam, wale wanaowaza mema, wakae na wajadili namna ya kukomesha mitazazmo mibovu ya baadhi ya watu walio nao juu ya maisha. Bila shaka wanafahamu haya ni kwa nini yanatokea kwa kuwa eneo yanakotokea haya ni kule kwenye wingi wa wafuasi wao ambao wameshindwa maisha. Wanatakiwa wawape elimu sahihi namna wataboresha maisha yao badala ya kutafuta njia za kiharamia au kutaka kuharibu nchi ili wakose wote. Hii ni roho ya shetani yule mwenye wivu.
Nne jeshi la polisi lirudi katika misingi ya kutenda haki. Waacha uharamia wa kudhulumu na kuonea raia. Polisi waache unyanganyi wa mali na haki za raia ili jamii iwaone kuwa ni sehemu yake na iwape ushirikiano. Polisi wamejitenga na wananchi ki malengo na ndiyo sababu wananchi wako kimya hata wanapoona mipango miovu inatokea. Ninasema hivi kwa sababu, bila shaka hata katika tukio hili kulikuwa na watu karibu. Hao jambazi hakutoka hewani na hakuyeyeyuka baada ya ushetani wake. Watu walimwona akiingia na alikoelelkea wanajua. Jeshi la polisi linahitaji kuhamasisha umoja kati yake na raia ili raia walisaidie kuzuia matukio ya kishetani kama haya.
Tano serikali iache kuwatumia polisi vibaya. Inawajengea chuki dhidi ya wananchi. Wanachi wanaoan polisi ni watesi wao na si wasaidizi n ahivyo kujitenga nao mbali. Viongozi wa ccm na serikali wawekeane mikakati ya kudhibiti matumizi ya jeshi la polisi yasiyo halali. Yanalidhalilisha jeshi letu na kuliweka katika wakati mgumu sana wa kutengwa na umma.
Serikali itambue kwamba hii ni karne nyingine. Budget za serikali ziangalie suala la technolojia ya ulinzi na usalama ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu. Ikiwa tetemeko lilitokea Bukoba na hapakuwa na hata kipimo cha kutambua kabla hatua stahiki zikachukuliwa, na bado serikali ikasema haikuleta tetemeko, niina mashaka na uwepo wa technolojia ya ulizini wa mipaka yetu hasa katika bahari na sehemu zisizokaliwa na watu. Kuliko kutumia nguvu kubwa kudhibiti wapinzani, ninaomba serikali iwekeze kweney technolojia surveillance ndani na nje ya mipaka yetu. Polisi wanaoonyesha uharamia kama kunyang'anya mali za mahabusu kwa nguvu, kutetea uharlfu ndani ya jeshi, kuonea na kusingizia raia, wanatakiwa kuondolewa kwenye kikosi hivi kwa sababu hawa ini hatari kwa jeshi lenyewe. Wanaweza kuuza taarifa hata mipango ya dani ya jeshi kwa maslahi ya 1000,000. Ondoeni maharamia kati ya polisi, sukeni jeshi letu upya, kisha liwezeshwe kwa technolojia inayoona na kutoa taarifa ya matukio hasa katika maeneo yenye wasialam wengi kama huko pwani na mkuranga.
Watanzania ninaomba sana tuendelee kuishauri serikali japo inakataa kushauriwa. Hii la kukataa ushauri wa wanaoongozwa tulichukue kama tatizo linalohitaji tiba kama maradhi lakini hatwezi kujenga taifa pasipo kushauriana na kusikilizana. Ccm ninyi ndio wenye viburi, ninaomba muwe wa kwanza kujirekebisha. Tambueni bila taifa lenye amani ccm haipo.
Viongozi acheni kujenga matabaka miongoni mwa wananchi. Acheni kuwadharau watanzania na kuwabagua, huku mkifanya kebehi za wazi kwa viburi. Migawanyikio mnayoijenga ndiyo inayoondoka mishkikamano na mioyo ya uzalendo . Bila kuwa na umoja na uzalendo, hakuna suluhu rahisi ya matatkzo yanayoinuka.
NINAOMBA NISIITWE MCHOCHEZI MAANA SERIKALI INADHANI IKIWAUNGA WATU VINYWA NDIYO INASHINDA, KUMBE INAJENGA ROHO MBAYA ZA KIKATILI NA MTAWANYIKO UANOANZA KULIGHARIMU TAIFA KWA KASI HII YA AJBU.
Jambazi Mwenye silaha aende kuua tu polisi tu bila visasi? Jambazi si angeenda kuiba bank na kwa matajiri?Sidhani kuna raia gani mwema akiharasiwa na polisi anakimbilia kupora silaha polisi na kuua. Basi ni bora aue tujue moja. Lakini uporaji wa silaha...! Hapana huyo ni jambazi au GAIDI. Lakini sio raia. (Ukipanda Mbeki shambani kwako au nyumbani kwako elewa jambo moja tu, kama Honda make hutalila wewe basi atakula mwanao au mjukuu Wako. Too maneno ya chuki dhidi ya serikali yanayopandikizwa na upinzani, mazao yake yataliwa na haohao wapinzani nyakati hizo nchi haikaliki wala haitawaliki) PASAKA NJEMA.
Umeongea vizuri sana ila kosa lako ni kuihusanisha uislam na uharifu au ugaidi.uislam ni dini inayohubiri amani.ukome kuhihusisha ugaid na uislam.Nionavyo mimi ni makundi ya maharifu yanakusanya silaha.
Halfu kitu kingine kule yanakotokea haya ni kule kule kwenye pwani isiyokuwa na ulinzii. Ulinzi uimarishwe katika njia chocho za bahari.
Ninaomba JWTZ wafanye operation maalumu katika misitu iliyokatika maeneo hayo. Kunaweza kuwa na kambi maalumu ya uahrifu.
Tatu viongozi wa dini ya kiisilam, wale wanaowaza mema, wakae na wajadili namna ya kukomesha mitazazmo mibovu ya baadhi ya watu walio nao juu ya maisha. Bila shaka wanafahamu haya ni kwa nini yanatokea kwa kuwa eneo yanakotokea haya ni kule kwenye wingi wa wafuasi wao ambao wameshindwa maisha. Wanatakiwa wawape elimu sahihi namna wataboresha maisha yao badala ya kutafuta njia za kiharamia au kutaka kuharibu nchi ili wakose wote. Hii ni roho ya shetani yule mwenye wivu.
Nne jeshi la polisi lirudi katika misingi ya kutenda haki. Waacha uharamia wa kudhulumu na kuonea raia. Polisi waache unyanganyi wa mali na haki za raia ili jamii iwaone kuwa ni sehemu yake na iwape ushirikiano. Polisi wamejitenga na wananchi ki malengo na ndiyo sababu wananchi wako kimya hata wanapoona mipango miovu inatokea. Ninasema hivi kwa sababu, bila shaka hata katika tukio hili kulikuwa na watu karibu. Hao jambazi hakutoka hewani na hakuyeyeyuka baada ya ushetani wake. Watu walimwona akiingia na alikoelelkea wanajua. Jeshi la polisi linahitaji kuhamasisha umoja kati yake na raia ili raia walisaidie kuzuia matukio ya kishetani kama haya.
Tano serikali iache kuwatumia polisi vibaya. Inawajengea chuki dhidi ya wananchi. Wanachi wanaoan polisi ni watesi wao na si wasaidizi n ahivyo kujitenga nao mbali. Viongozi wa ccm na serikali wawekeane mikakati ya kudhibiti matumizi ya jeshi la polisi yasiyo halali. Yanalidhalilisha jeshi letu na kuliweka katika wakati mgumu sana wa kutengwa na umma.
Serikali itambue kwamba hii ni karne nyingine. Budget za serikali ziangalie suala la technolojia ya ulinzi na usalama ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu. Ikiwa tetemeko lilitokea Bukoba na hapakuwa na hata kipimo cha kutambua kabla hatua stahiki zikachukuliwa, na bado serikali ikasema haikuleta tetemeko, niina mashaka na uwepo wa technolojia ya ulizini wa mipaka yetu hasa katika bahari na sehemu zisizokaliwa na watu. Kuliko kutumia nguvu kubwa kudhibiti wapinzani, ninaomba serikali iwekeze kweney technolojia surveillance ndani na nje ya mipaka yetu. Polisi wanaoonyesha uharamia kama kunyang'anya mali za mahabusu kwa nguvu, kutetea uharlfu ndani ya jeshi, kuonea na kusingizia raia, wanatakiwa kuondolewa kwenye kikosi hivi kwa sababu hawa ini hatari kwa jeshi lenyewe. Wanaweza kuuza taarifa hata mipango ya dani ya jeshi kwa maslahi ya 1000,000. Ondoeni maharamia kati ya polisi, sukeni jeshi letu upya, kisha liwezeshwe kwa technolojia inayoona na kutoa taarifa ya matukio hasa katika maeneo yenye wasialam wengi kama huko pwani na mkuranga.
Watanzania ninaomba sana tuendelee kuishauri serikali japo inakataa kushauriwa. Hii la kukataa ushauri wa wanaoongozwa tulichukue kama tatizo linalohitaji tiba kama maradhi lakini hatwezi kujenga taifa pasipo kushauriana na kusikilizana. Ccm ninyi ndio wenye viburi, ninaomba muwe wa kwanza kujirekebisha. Tambueni bila taifa lenye amani ccm haipo.
Viongozi acheni kujenga matabaka miongoni mwa wananchi. Acheni kuwadharau watanzania na kuwabagua, huku mkifanya kebehi za wazi kwa viburi. Migawanyikio mnayoijenga ndiyo inayoondoka mishkikamano na mioyo ya uzalendo . Bila kuwa na umoja na uzalendo, hakuna suluhu rahisi ya matatkzo yanayoinuka.
NINAOMBA NISIITWE MCHOCHEZI MAANA SERIKALI INADHANI IKIWAUNGA WATU VINYWA NDIYO INASHINDA, KUMBE INAJENGA ROHO MBAYA ZA KIKATILI NA MTAWANYIKO UANOANZA KULIGHARIMU TAIFA KWA KASI HII YA AJBU.
Umeongea vizuri sana ila kosa lako ni kuihusanisha uislam na uharifu au ugaidi.uislam ni dini inayohubiri amani.ukome kuhihusisha ugaid na uislam.
Mkuu Panzi Mchanga, kwanza asante kuchangia uzi huu. Pili asante kunifuatilia tangu enzi za Kiti Moto.Paskali;
Nimekuwa nafuatilia thread zako. Na nilitaka nijue ni mtu wa aina gani. Wewe ni mwanahabari wa siku nyingi na baadhi ya vipindi ulivyokuwa unaendesha kama "KITI MOTO" ndani ya Channel Ten enzi hizo nilikuwa mfuatiliagi wako sana, na baadae TBC na baadae sijui unafanya nini sasa.
Ila kwa thread yako ya leo na kua attach thread ya nyuma; ambayo kimsingi haina uhusiano kabisa. Inawezekana uelewa wako ni mdogo. Kule kibiti kabla ya Jana; waliuliwa wenyeviti wa vitongoji. Hakuna wanachochukua-kwa hiyo kuhusisha jambo lini na ujambazi ni jambo la kipa unyuma kwa sasa.
Maeneo ya Kibiti na Mkuranga yanaelezwa ni maeneo ya biashara haramu. Kule Nyamizati maeneo ya baharini wanaishi watu ambao wanasemekana sio asili ya Tanzania na wanafanya biashara haramu. Manakuja na majahazi. Kuna uwezekano mifumo yetu iliwalea hawa watu kwa maslahi ya watu wachache; wakiwemo hao wenyeviti.
Ya Mkuranga yanashabihiana sana na ya Tanga; Lengo la hawa ni kuteta Mtafaruku (Terror) kwa malengo mengine. Na wanachofanya ni kunyamazisha mifumo ya utoaji taarifa kutoka ngazi ya chini. Tuangalie kwa mapana mambo yanayotokea Uganda (Senior Police killings), kule Kenya n.k.
Kwa hiyo Paskali; approach hapa siyo ya kutongoza wahalifu-Usipokula ubongo wao watakula wako.
Hii thread imekosa uzalendo na ni ya kichonganishi pia. Nasema hivi kwa sababu hujaja na solution; na pia ukirudia thread ulio attach .
Kama wewe ni Serikali ungefanyaje-ungeenda kuwatongoza wahalifu; najaribu kuwaza tu. Ungewambia jamani hatuta wanyang'anya silaha tena haraka haraka hata kama mkienda kuvunja benki- chukueni tu ila msiuwe mtu jamani!
Nangojea na haki za binadamu waje waseme tunalaani mauwaji ya polisi, kwa sababu walilaani mauwaji ya majambazi-What a shame
Ila kwa serikali kwa wakati huu inatakiwakupandisha security level to yellow kwa maeneo yote ya ukanda wa pwani; ingawa hii sii mara ya kwanza kutokea.
Niwape familia pole na watu wote walioadhirika kwa namna moja au nyingine.
Dini ya kiislam hapo imeingiaje? Badala ya kujadili hoja unaleta vilivyomo kichwani mwako!! Labda una nyepesi aliyeua ni muislam