Mauaji ya Polisi wetu ni Ujambazi, Ugaidi au Retaliation? Nini kifanyike kukomesha hali hii?

Naomba hili liangaliwe.

upo ushahidi mwingi umetolewa si vizuri kuuweka hapa.

kuna haja ya jeshi la polisi kuzingatia haki Za binadamu wakati WA kutekeleza majukumu yao hasa kwa wanaokamatwa kwa kesi Za ugaidi.
 
Naomba hili liangaliwe.

upo ushahidi mwingi umetolewa si vizuri kuuweka hapa.

kuna haja ya jeshi la polisi kuzingatia haki Za binadamu wakati WA kutekeleza majukumu yao hasa kwa wanaokamatwa kwa kesi Za ugaidi.
Na sio kwa watuhumiwa wa ugaidi pekee, hata kwa raia wanaokamatwa kwa makosa mbalimbali. Sidhani kama raia aliyewahi kupitia mikononi mwa polisi anaweza kutoa habari za uhalifu mahali
 
Jeshi la Polisi la Tanzania ni kama Mbwa na bwana wake akiamrishwa anatekeleza bila kujiuliza nn impact ya haya wanayofanya
 

Wafunguwe kanda maalum kama ilivyo kule tarime.
 
Kisifanyike chochote juzi kuna Wabunge wameomba hilo swala lijadiliwe bungeni kuna wanawake jenista mhagama na mwenzie bila hata aibu wanasema ni uchochezi!
Yakasikika makofi ya Wabunge wa ccm waaaa...waaaa....waaaa....
Acha tuendelee hivi hivi
MUNGU HUYU!
 
jeshi lijali haki Za binadamu, ripoti Za tume Za haki Za binadamu tz karibia kila mwaka Hawa hawakosekani ,kwanini?
 
Kimtazamo wangu hii ongoing operation ya kukusanya silaha inayofanywa na kikundi ambacho hakuna akijuaje.Vyombo vya ulinzi wanatakiwa wawe makini sana,wanatumika na wanasiasa hadi watu hawawapendi.Kwenye ukweli wao wamekuwa wakipindisha,kwenye haki wao wanafanya dhulma,kumekua na kuteswa na watu wasiojulikana kila kukicha,wapo radhi kukesha mtaandaon kujua nan katukana nani ili wampate kuliko kudeal na core functions zao,kwa nini hao wasiwashindwe?.Watu wamekua wakipotea huku majibu yanayotelewa na zaid ya vituko.Chuki hii si nzu kabsa maana wanakosa support pind wanapoihitaj na kwa kua wote tupo kwenye jamii moja what goes around,comes around..lazma nao yawakute tu.
Kuna mambo ambayo ukiangalia na kusikiliza unaona kabisa kuna watu wana. misuse wanausalama wetu,na cha ajabu wao wamekubali kuwa upande mmoja na kukandamiza wengine.
Niseme tu death is real,na wote tutakufa,ila vyombo vyetu vinatakiwa vitende haki na vifanye kaz kwa weled si "mzuka" na watapata support nzur tu.
Huu mtindo wa kuuwa askar na viongoz wengne kwenye huo mkoa kwangu naona si just ujambaz,waende watafute sabab ni nini na wajirekeshe ili raia wawape taarifa sahihi kwenye kila tukio.Raina wapenda aman bado tupo weng,watupe support na wawe fair tu.Above all,R.I.P kwa fallen servicemen wote wa hili tukio
 
unaongolea polisccm

saivi polis akifa watu wanashangilia polis punguzeni kutumika pia hamtendi haki.
 
Tukiwa vijana wadogo wakati huo kijijini,kuna Mzee alikuwa mtemi sana,anapiga mpaka wazee wenzake mbele za watoto na wake zao.Ilikuwa nj zile enzi za "wababe" ndio wanaheshimika,kuna siku aliwahi kumpiga kerebu mzee mwenzake mbele ya mwanae wa kiume.

Kile kitendo kilimuuma sana yule dogo,akakaa na kinyongo moyoni bila kusema,siku ya siku Mzee mbabe tukasikia ameokotwa korongoni kijiji cha Muhunze akiwa hana kaptula ya ndani wala shati,na jana usiku alionekana kilabuni akinywa pombe,miaka kumi baadae ikaja kugundulika alitandikwa na yule dogo ambaye alishuhudia baba yake akitandikwa kerebi kama miaka mitano iliyopita.

Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana,saikolojia ya binadamu ni ngumu kuielewa.Unapofika na kusikia kuwa Masheikh ambao ni mababa wa familia na viongozi wa dini wamelawitiwa na kuminywa korodani mpaka kupoteza uwezo wa kusimamisha,unategemea hii chuki inakaa wapi?

Unapombambikia mtu kesi ya uwizi,anasota rumande kwa mateso na karaha,tambua huyu ana ndugu na watu wanaompenda walio tayari kulipa kisasi ili kuridhisha nafsi zao.

Wapo watu wanaofungwa bila makosa,wapo wanaobambikiwa kesi kwa sbb za kisiasa,haya yote yanajenga chuki kati ya raia na askari polisi.

Polisi unafika kwenye kijiwe cha bodaboda unasomba pikipiki 20 kisa wamezidi muda wa "serikali" wa saa sita usiku,na ili wazitoe pikipiki zao,basi kila mtu anatakiwa kutoa elfu50....hii chuki inamea kama mmea kando ya kijito
 
polisi waweke siasa pembeni wafanye kazi kwa kutumia taratibu za kazi zao watafanikiwa
 
Mkuu Pascal heshima kwako. Kwanza nitoe pole kwa jeshi la polisi na kwa familia na ndugu wote waliopatwa na misiba hii. Mimi nitachangia upande wa recruiting and training za polisi wetu. Mkuu, utaratibu wa kuajiri na mafunzo kwa vijana wetu nadhani haupo sawa, huwezi kuajiri watu kwa kujuana, watu wenye elimu zao halafu, wasio na wito, utayari, kujitoa halafu unawapeleka kwenye mafunzo ambayo kimsingi hayaendani na wakati tulionao. Unamchukuaje mtu ambaye amemaliza chuo, hajaoa, hajamaliza hata mkopo wake wa bodi, ambaye kwao waliuza rasilimali zilizokuwepo akasomea halafu unampeleka kwenda kupambana na jambazi. Automatically ndo maana linapotokea tukio la uhalifu polisi hufika baada ya nusu saa au saa moja na wakikaribia hupiga risasi hewani ili kukwepa kukabiliana na majambazi live. Inawezekana mbinu za mafunzo , aina ya askari wetu (watoto wa wakubwa) hawawez kuifanya hii kazi kwa ufanisi au wanaogopa kutokana na kwenda huko kama sehemu ya kukulia au kutafta kipato na si vinginevyo. Naamini utaratibu wa zaman uliokuwa unatumika kuajiri wana usalama ilikuwa nzuri, huko mitaani kuna watu ukiwapeleka huko kufanya kazi kama hiyo wataifanya vyema. Mkoa wa Mara kwa mfano kuna watu wakiskia risasi ya jambazi wanaanza kukimbia kwenda inapotokea, huku Pwani hawa waswahili ni kinyume. Sikatai jeshi kuwa la wasomi, ila wasomi wawepo wachache wenye kupanga mipango ila wale rapid responders si lazima wawe wasomi amabao huenda huko huku akikumbuka amesoma miaka mingi hajatimiza malengo yake n.k. Tuachane na huu utaratibu wa sasa wa kuajiri kwa kujuana huku tukijaza watoto wa vigogo kwenye majeshi yetu ambao wakifika huko akili zao ni kuzichanga na si vinginevyo, hivi mmewahi kujiuliza Kwanini polisi wakitumwa kwenda kumkamata mwanasiasa wanaenda kwa mbwembwe ilihali shughuli kama hii ya kupambana na wahalifu /majambazi kabla ya kufika eneo la tukio huanza kufyatua risasi hewani ili kuwa alert majambazi kukwepa kupambana nao? Mtaala wa mafunzo ndani ya jeshi letu ubadilishwe ili kuendana na wakati na ufocus miaka mingi ijayo. Jeshi letu inawezekana ni worse kulikon tunavyofikiria, wamejaa wapiga dili, watoto wa vigogo, wavivu na watu wasiokuwa na mori, uzalendo. Tutengeneze kikosi imara, wenye ari. Kuna vijana huko vijijin ukiwachukua na kuunda kikosi maalum ndani ya jeshi letu let's say "First Responders" na mbinu mpya tutasonga mbele. Asante.
 
Hii nchi iko salama nyie mnoendelea kujadili hili sua mtakua wapiga diri au wauzaji waunga mnataka kumkwamisha Rais acheni uchochezi kati ya Raia na Serikali aya ndo maneno ya Awamu ya Tano
 
Umeanza vizuri lakin umwpoteza mwelekeo ,he una maana kuwa RAIA na polisi na we kama RAIA haupo tayari kuwasaidia polisi kwa namna yyte?
 
Unajua kupukutika kirahisi? Kweli RAIA mzalendo WA nchi hiii unasema hivyo namheshimu mzee WA nyuki WA kanda ya NYANDA za juu.
 
Viongozi wakiislamu tena? Umepotoka mkuu. Hapo hakuna uislamu na mwenye mawazo kama haya siku mkiwaandama hao waislamu waziwazi (kwa sasa wanaandamwa kwa kificho) huo moto mtaupiga petroli na yatakuwabkama yale ya garissa.

Hao majambazi na hapo kuna uhasama wa wananchi na vyombo vya usalama na viongozi wa hayo maeneo. Si uliona waliwaua askari kisha wakaamuru wananchinwakachukue vitu vyao kama mbao, mkaa n.k. Hapo hakuna ugomvi wakidini, acha kichochea mengine tusiyoyaweza.

We unadhani Alshababi wakifika hapa kwetu siku utasikia central imetekwa na mjengo wote umewaka moto. Tusiombee hayo na tuache fitna hii. Mawazo hayo yakizoeleka na kuanza kuwatesa wasiohusika, vijana waliokata tamaa wataungana na hao majambazi na mziki wake mtahama dar.

Vita yao hawa sio kama ile ya kagera. Wanavizia na kuuwa na wanasepa. Nakusihi acha kupandikiza haya mambo ya chuki za kidini, hata wewe kutapona.
 
Nini maana ya Gaid?
 
Tuanze kwanza kukomesha utekaji...haya ya mauaji yatakoma endapo utekaji watu utakwisha..na usipokwisha basi polic wajiandae
 
Kuna jambo lingine linashangaza sana. Mtu anakamata lori la mkaa, linataifishwa alafu mkaa ule ule unauzwa na mwenye mali hapati kitu. Kwanini msimbwambie mkaa wako tutauza na utapewa nusu ya mali yako. Badala yake mtu anabaki masikini milele.

Mtu unakamata mbao, zinataifishwa na wauza tena kwa bei ya hovyo kabisa, mtu mwenye mali anabaki kiwa masikini na anamuona askari aliyetaifisha mali anakunywa mipombe na kubadilisha mademu. Hatari sana.

Safari moja (hiki kisa sikisahau), tulipanda fuso ya jamaa alibeba nazi anakuja temeke, kufika katikati hapo kwenye kizuizi jamaa wakazuia gari kisa dereva aliweka vigunia viwili vya mkaa vya 25kg. Dereva akajitetea kuwa jamani mm natoka pori kila siku kule mkaa rahisi, naenda kutumia huu mm sifanyi biashara. Au nilipe ushuru basi.

Askari wakagoma wakataka kuchukua mkaa, tukawekwa pembeni 2hrs. Dereva akabembeleza sana. Jamaa wamekomaa kwelikweli.

Dereva akawaita wote askari wakaja. Akapanda kwenye gari akawaambia haya shusheni huo mkaa niondoke lakini nawahakikishieni mkiiona hii gari kaeni mbali ntakuja kuwasaga wote hapahapa na kesi yake ni elfu 30.

Jamaa alifoka sana kuwa mnatuonea sisi watu wa pwani tu mbona ndugu zenu wanapita nao mkaa hapa hamwashiki, mm kila siku ndio kazi yangu napita njia hii kufuata mihogo na nazi sasa shusheni mm niondoke lakini mkae sawa.

Alikua askari mmoja akamwambia ondoa gari yako uende.

Haya mambo yapo na watu wanajenga chuki sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…