Mauaji ya watu wenye ualbino yameanza tena kipindi hiki cha uchaguzi

PureView zeiss

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2016
Posts
10,786
Reaction score
35,916
#HABARI Jeshi la polisi mkoani Kagera linawahoji watu 3 akiwemo baba mzazi wa mtoto Asimwe Novart (2) kwa tuhuma za kuhusika na kuibwa kwa mtoto huyo Mei 30 nyumbani kwao katika Kitongoji cha Mbale wilayani Muleba.

Mtoto huyo mwenye ulemavu wa ngozi aliibwa baada ya mama yake mzazi kulaghaiwa na watu waliomhadaa kwa kuomba msaada.

Itakumbukwa kuwa wiki chache zilizopita polisi mkoani Songwe lilimkamata mama mzazi wa mtoto aliyetekwa na kisha baba wa mtoto huyo kutakiwa kulipa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kumkomboa mtoto wake.

Kwanini haya mauaji yameanza kujitokeza tena kipindi hiki cha uchaguzi? Haya ni mauaji ya pili yanatokea katika mikoa hiyo ya kanda ya ziwa
 
Siku yangu imeharibika kuona mtoto mzuri hivyo ameenda kuchinjwa ili wapuuzi wafanyie kafara.
Nguvu ya Mwenyezi Mungu ikawaangamize wabaya wote wa Mtoto huyu.
Amen!
inakera na kufadhaisha
 
sisi watu weusi ni takataka mambo yetu meusi kama rangi zetu
 
Mmesema uchaguzi. Watakua tu chadema na uchaguzi wao wa kanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…