Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na yeye Maulid si anajifanyaga mwarab koko....hivi hawa watu hawajuwi historia ya waarab na watu weusi kweli au ni kule kujidharau tu.Inashangaza sana mtu bila huruma unapokea pesa ili uende kusambaza propaganda za kuwafukuza waTz wenzako kwenye ardhi yao ya asili ili waarabu waje kuua Simba na Tembo, hawa ndio walikuwa wanauza wenzao utumwani kwa waarabu sababu ya vipande vya fedha, shenzy kabisa
Kwakweli, kwa historia ya tuliyofanyiwa na hao wanaojiita waarabu, na bado kukinasibisha nao kwa kiwango hicho, ni utumwa tu kwa kweli..Na yeye Maulid si anajifanyaga mwarab koko....hivi hawa watu hawajuwi historia ya waarab na watu weusi kweli au ni kule kujidharau tu.
Mwanzoni mwa mwezi huu wa pili 2022 kuliibuka ghafla na kwa kasi ya ajabu jitihada za makusudi za kujaribu kuwaondoa wamasai katika ardhi zao za kimila huko Ngorongoro kwa madai ya kwamba binadamu wamekuwa wengi huko Ngorongoro na hivyo wanaharibu ekolojia.
Vita hii ya kuwaondoa wamasai ilikuwa spear headed na nguli wa habari za michezo ndugu MAULID KITENGE ambapo alifanya ziara huko Ngorongoro na kutuambia WaTz kwamba eti ‘HALI INATISHA HUKO NGORONGORO’.
Wengi wetu tulihisi kuna jambo nyuma ya pazia, kwamba ghafla tu mtu wa michezo anaenda kushikia bango jambo lisilo la kimichezo; kiasi tulipata hisia kwamba amaelipwa pesa ili kueneza propaganda kwa maslahi ya waliomtuma.
Haya sasa, imekuja kugundulika kwamba hilo eneo la Ngorongoro anataka kuuziwa kampuni ya uwekezaji toka Falme za kiarabu inayomilikiwa na ‘Royal family’ kwa ajili ya kuendesha uwindaji wa kujifurahisha (game hunting), kampuni hiyo inaitwa OBC.
Sasa namuuliza ndugu yangu Kitenge, HUONI AIBU kuwasaliti WaTanzania wenzako?!
Tanzania, siding with UAE firm, plans to evict Maasai from ancestral lands
By Laurel Sutherland on 18 February 2022 - In northern Tanzania, more than 70,000 Indigenous Maasai residents are once again facing eviction from ancestral lands as the government reveals plans to lease the land to a UAE-based company to create a wildlife corridor for trophy hunting and elite...www.jamiiforums.com
================================
Update: 22/03/2022
Tanzania kuendesha mnada wa vitalu vya uwindaji; wawindaji kuruhusiwa kuua Tembo, Simba na wanyama wengine wazee
Tanzania inakusudia kuendesha mnada wa vitalu vya uwindaji, ambapo wawindaji wataruhusiwa kuwaua Tembo, Simba na wanyama wengine wazee. Mnada huo unakusudiwa kuzalisha TZS bilioni 69.6, na 25% ya fedha hizo zitaelekezwa kuzisaidia jamii zinazoishi jirani na vitalu hivyo.www.jamiiforums.com
=================================
Serikali: Hatujalipa kuweka tangazo jengo la Burj Khalifa lililopo Dubai
Msemaji wa Serikali kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema haya.. Serikali HAIJALIPIA kuweka tangazo la Tanzania katika jengo refu kuliko yote Duniani liitwalo Burj Khalifa lililopo katika Jiji la Dubai. Tangazo hilo limewekwa kwa lengo la kuitangaza Tanzania kutokana na uhusiano mzuri uliopo...www.jamiiforums.com
==================================
Video mbali mbali za miaka ya nyuma (10+ years) zinazohusu kuwaondoa wamasai ili kuwapa waarabu vipande vya ardhi ya Ngorongoro vilihusisha ukiukwaji wa haki za binadamu
=============================
“Mtanikumbuka....” By JPM.
==================================
Update: 22/03/2022
Tanzania kuendesha mnada wa vitalu vya uwindaji; wawindaji kuruhusiwa kuua Tembo, Simba na wanyama wengine wazee
Tanzania inakusudia kuendesha mnada wa vitalu vya uwindaji, ambapo wawindaji wataruhusiwa kuwaua Tembo, Simba na wanyama wengine wazee. Mnada huo unakusudiwa kuzalisha TZS bilioni 69.6, na 25% ya fedha hizo zitaelekezwa kuzisaidia jamii zinazoishi jirani na vitalu hivyo.www.jamiiforums.com
Kwa kweli, hii kampeni ianze mara moja, tumekuwa wengi 😂😂Waanzishe na kampeni ya kuwaondoa wakazi wa Dar es Saalaam kwa kuwa wamekuwa wengi kiasi cha kutishia ekolojia ya bahari ya Hindi, mikoko na matumbawe.
Wawekezaji au wauwaji wa simba na tembo?bora uwape wawekezaji hayo maeneo kuliko wamasai wanayoyaharibu. mwekezaji atayattunza, ila masai asiyejenga hata choo wala hana pa kuzika, unamwachaje? fukuzia mbali kabisa. kuna faida zaidi kwa nchi mwekezaji akipewa badala ya hao masai wasiojielewa.
Na wameanza kuwasafirishaWawekezaji au wauwaji wa simba na tembo?