Mwanzoni mwa mwezi huu wa pili 2022 kuliibuka ghafla na kwa kasi ya ajabu jitihada za makusudi za kujaribu kuwaondoa wamasai katika ardhi zao za kimila huko Ngorongoro kwa madai ya kwamba binadamu wamekuwa wengi huko Ngorongoro na hivyo wanaharibu ekolojia.
Vita hii ya kuwaondoa wamasai ilikuwa spear headed na nguli wa habari za michezo ndugu MAULID KITENGE ambapo alifanya ziara huko Ngorongoro na kutuambia WaTz kwamba eti ‘HALI INATISHA HUKO NGORONGORO’.
Wengi wetu tulihisi kuna jambo nyuma ya pazia, kwamba ghafla tu mtu wa michezo anaenda kushikia bango jambo lisilo la kimichezo; kiasi tulipata hisia kwamba amaelipwa pesa ili kueneza propaganda kwa maslahi ya waliomtuma.
Haya sasa, imekuja kugundulika kwamba hilo eneo la Ngorongoro anataka kuuziwa kampuni ya uwekezaji toka Falme za kiarabu inayomilikiwa na ‘Royal family’ kwa ajili ya kuendesha uwindaji wa kujifurahisha (game hunting), kampuni hiyo inaitwa OBC.
Sasa namuuliza ndugu yangu Kitenge, HUONI AIBU kuwasaliti WaTanzania wenzako?!
By Laurel Sutherland on 18 February 2022 - In northern Tanzania, more than 70,000 Indigenous Maasai residents are once again facing eviction from ancestral lands as the government reveals plans to lease the land to a UAE-based company to create a wildlife corridor for trophy hunting and elite...
================================
Update: 22/03/2022
Tanzania inakusudia kuendesha mnada wa vitalu vya uwindaji, ambapo wawindaji wataruhusiwa kuwaua Tembo, Simba na wanyama wengine wazee. Mnada huo unakusudiwa kuzalisha TZS bilioni 69.6, na 25% ya fedha hizo zitaelekezwa kuzisaidia jamii zinazoishi jirani na vitalu hivyo.
=================================
Msemaji wa Serikali kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema haya.. Serikali HAIJALIPIA kuweka tangazo la Tanzania katika jengo refu kuliko yote Duniani liitwalo Burj Khalifa lililopo katika Jiji la Dubai. Tangazo hilo limewekwa kwa lengo la kuitangaza Tanzania kutokana na uhusiano mzuri uliopo...
==================================
Video mbali mbali za miaka ya nyuma (10+ years) zinazohusu kuwaondoa wamasai ili kuwapa waarabu vipande vya ardhi ya Ngorongoro vilihusisha ukiukwaji wa haki za binadamu
=============================
“Mtanikumbuka....” By JPM.
==================================
Update: 22/03/2022
Tanzania inakusudia kuendesha mnada wa vitalu vya uwindaji, ambapo wawindaji wataruhusiwa kuwaua Tembo, Simba na wanyama wengine wazee. Mnada huo unakusudiwa kuzalisha TZS bilioni 69.6, na 25% ya fedha hizo zitaelekezwa kuzisaidia jamii zinazoishi jirani na vitalu hivyo.