Maulid Kitenge, propaganda ulizotumwa kuzifanya kwa wana-Ngorongoro hazitakuacha salama

Lazma mjue ...kua wamasai au kuwaondoa watu humo Ngorongoro basi hadhi iliyonayo itaondolewa kabisa ...someni kupitia UNESCO kuhusu Ngorongoro
 
Ngorongoro has ever since being a place of maasai and wild animal period

Sent using Jamii Forums mobile app
Lazma mjue ...kua wamasai au kuwaondoa watu humo Ngorongoro basi hadhi iliyonayo itaondolewa kabisa ...someni kupitia UNESCO kuhusu Ngorongoro
Niko UNESCO jikoni shughuli za binadamu kuzidi uwiano kati ya binadamu na wanyama zimesababisha mchakato wa UNESCO kuondoa hadhi ya Ngorongoro kwenye list yao....
 
Hoja ni kwamba, hao watu ipo siku watazidi na hiyo itasababisha wanyama kukimbia kutokana na makazi ya binadamu kukua zaidi.

Kwa mtindo wa sasa, ngorongoro miaka 50 ijayo haitakuwepo.
Bora uwepo wa mwanadamu na uhai wake kuliko mnyama,
Ni upumbavu kuthamini uhai wa mnyama kwa ajili tu ya utalii na kudharau uhai wa mwanadamu.
 
Kwa hiyo kwako wewe wanyama pori ni muhimu kulipo binadamu
 
Bora uwepo wa mwanadamu na uhai wake kuliko mnyama,
Ni upumbavu kuthamini uhai wa mnyama kwa ajili tu ya utalii na kudharau uhai wa mwanadamu.
Wewe kenge Dunia haiwezi kua salama na wala maisha hapa Duniani hayawezi kuwepo bila hao wanyama.

Maisha ya hapa Duniani yanategemea a complete ecosystem inayohusu viumbe vyote vya wanyama.

Kwa akili zako fupi unadhani wanyama hawana umuhimu. Umuhimu wao hauko kwenye kuwaangalia tu, tunategemeana for survival.

Mataahira kama nyie msioelewa kitu kaeni kimia
 
 
Ni kweli waarabu washafanya yao kwa Kitenge?
Zaidin ya comment 300, 95 zinamtuhum Kitenge
kupokea ngawira/ njuruku kutoka waarabu na siri kali.







 
Lazma mjue ...kua wamasai au kuwaondoa watu humo Ngorongoro basi hadhi iliyonayo itaondolewa kabisa ...someni kupitia UNESCO kuhusu Ngorongoro
Nimesoma. Imesema capacity ya Ngorongoro ni wamasai 20000 na mifugo 275000. Ikizidi hapo itakuwa overgrazing na itaathiri hadhi ya hifadhi. Pasiwe na kilimo cha kudumu. Wewe umesoma nini? Au wamasai hawajazidi 20000?

Amandla...
 
Kitenge mod warekebishe
 
Ngorongoro Conservation Area siyo ya Wamasai pekee, ni ya Watanzania wote, na inahitaji Mjadala wa kina.
Itakuwa aibu na fedheha kubwa kwa Taifa letu kama hii World Heritage itapotea kutokana na kuogopa kelele za Wanaharakati ambao wameigeuza Ngorongoro kuwa mali ya Wamasai.
Hii ni hatari.
Serengeti nayo iwe ya Wakurya?
Ruaha iwe ya Wahehe?
Mikumi iwe ya Wakaguru?
Mazingira ya Ngorongoro ya Binadamu kuishi na Wanyamapori yanakubalika, lakini ni lazima kuwe na Ulinganifu wa Kiekolojia, 'Ecological balance'.
Majumba yanajengwa ndani ya Ngorongoro. Hii siyo sawa.
Ngorongoro ikipotea, sisi sote tutaingia katika fedheha isiyo na kipimo.
Kumtukana Maulidi Kitenge kwa kuandika kilichopo, hakuisaidii Tanzania wala Wamasai wanaoishi Ngorongoro.
Malisho yakiharibiwa, Wanaharakati hawataonekana kuwafadhili Wamasai.
Watakimbilia kusikojulikana.
Tuiokoe Ngorongoro.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…