Maulid Kitenge, propaganda ulizotumwa kuzifanya kwa wana-Ngorongoro hazitakuacha salama

Asante Mwalimu ...humu humu shule inapigwa
 

Katika hili Nampongeza sana Maulid Kitenge ,Oscar Oscar na EFM kutujuza yanayo endelea ngorongoro creater hakika inasikitisha sana tena sana! Ni lazima hatua kali na za haraka zichukuliwe kuinusuru ngorongoro! Kamawe wao kuzaliwa na kukulia ngorongoro hakuwapi uhalali wa kufanya ubharibifu kwenye hii hifadhi!

Itakuwa jambo la aibu sana kama serikali itanyamazia na kuacha yanayo endelea kwenye bonde la ngorongoro...nina hakika kabisa kama wataachwa haitachukua miaka miwili hifadhi hii itapotea kabisa!
 
Asante Mwalimu ...humu humu shule inapigwa
Mkuu hapo ni kimalikia tu kimetumika ili kuliweka hili swala katika mtazamo wa kitaalamu, kwa wale watu wanaohusika na maswala ya uhifadhi ili waweze kutoa ufafanuzi kama haiwezekani kuthibiti kukua kwa makazi na shughuli za binadamu katika hifadhi ya ngorongoro badala ya kujikita kwenye kuwahamisha masai pekee.............ladha ya eneo la hifadhi ya ngorongoro kama kivutio cha utalii ni uwepo wa wamasai na ng'ombe wao humo.
 
Great!!! Mwalimu

Aproach kama hizi ndo zitumike mizania na Uyunesco

Asante sana Mwalimu wa Ikolojia na jamii
 
Great!!! Mwalimu

Aproach kama hizi ndo zitumike mizania na Uyunesco

Asante sana Mwalimu wa Ikolojia na jamii
And bad still, kuwahamisha wamasai kwenye makazi yao ya asili unaweza kujikuta unaua the maasai cultural heritage ambacho nacho ni kivutio cha utalii.........kwa hiyo utaona pale ngorongoro kuna vivutio viwili vya utalii kwa mpigo.
 
And bad still, kuwahamisha wamasai kwenye makazi yao ya asili unaweza kujikuta unaua the maasai cultural heritage ambacho nacho ni kivutio cha utalii.........kwa hiyo utaona pale ngorongoro kuna vivutio viwili vya utalii kwa mpigo.
Cc Wadau wa Uhifadhi Ngorongoro na TZ kwa ujumla
 
Ngoja ukweli niuseme hapa.

1. Kuna tofauti kati ya hifadhi ya Ngorongoro na eneo la Ngorongoro crater, Ngorongoro crater ni kaeneo kadogo sana ndani ya hifadhi ya Ngorongoro. Mgogoro uliopo sasa ni kuhusu hifadhi ya Ngorongoro kiujumla wake.

2. Karibu jamii (koo) zote za kimasai zilizopo hapa dunia, eneo la asili la tamaduni, mila na matambiko ya kimasai zinajikita pale Ngorongoro. Ni sawa na wayahudi na eneo la nchi ya Israel kule mashariki ya kati. Sio jambo rahisi sana kuelewa hiyo dhana kama hutoki kwenye hizo jamii.

3. Kuendelea kuwepo kwa wamasai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kutaiua ile hifadhi (maana idadi na shughuli zao zinazidi kuongezeka) na kuwaondoa wamasai kwenye hifadhi ya Ngorongoro kutaiua pia hiyo hifadhi (maana kutaondoa ikolojia na watunzaji wa asili, na hapo hapo kutatoa nafasi kwa shughuli zingine halali na zisizo halali kufanyika pale). Kwa kifupi sana, kwa hali ilivyo sasa hakuna namna kutaifanya hifadhi iendelee kuwepo vile vile baada ya miaka 30 ijayo. Kwanini? Kinachogombaniwa sasa sio kuilinda hifadhi ya Ngorongoro iendelee kubakia kama ilivyo bali kuitumia tu. Sio serikali wala wamasai, wote maslahi yao ni kuitumia Ngorongoro ili kuvuna.

SULUHISHO NI NINI?
Ikiwa tunataka hifadhi ya Ngorongoro iendelee kuwepo hata kwa vizazi vijavyo, basi Suluhisho kamili ni kuhakikisha shughuli zozote za kila siku za kibinadamu zinaondolewa kabisa pale Ngorongoro. Utalii upigwe marufuku (zibakie shughuli za kitafiti tu) na wamasai waondolewe kabisa mule hifadhini unless 'wamasai mahususi' wanaotakiwa kuishi kujima (kama wanyama) ili kulinda ikologia ya hifadhi.
 
Mkuu pamoja na ENGO ya Siasa kuimuda na Kiuhifadhi umo salute mingi sana...
 
Mkuu lazima muambiwe ukweli.
HAMENI NGORONGORO.
 
Habari za Magufuli wachana nazo maana tayari kashamaliza mwendo wake.

Ila ukae ukijua kuwa Ngorongoro lazima ibakie salama kwenye uhalisia wake.

Tunawajua watu kama nyinyi ndiyo mnatumiwa na maadui wa taifa kutaka kutukwamisha .
 
We ni mjinga fulani ambaye hata ni kikuuliza hili jina la Ngorongoro maana yake nini utabaki unavuja jasho tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Haijalishi mimi kutojua maana ya jina la Ngorongoro lina maana gani ila nikupe hakikisho kuwa nyinyi na kundi lenu kamwe hamtaweza kukwamisha miradi ya serikali hii ya awamu ya 6.
 
NGORONGORO IKABIDHIWE TANAPA!
 
Sijaelewa why mleta mada kamuattack maulid kitenge personally...haimake any sense..kwani yeye ndo ana maamuzi?? Ata simpo logic tu kama hali ilivyokuwa miaka 1950 sio sawa na sasa,wamasai wameongezeka pamoja na mifugo yako itabid waondoke tu kupisha hao wanyama..maana wasipofanya hivyo wanyama watakimbia hifadhi..Angalau hoja ingekuwa serikali iwalipe fidia kwa maendelezo ya kudumu waliyojenga huko kwenye hifadhi..wasiondoke bila kulipwa fidia na usumbufu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…