Maulid Kitenge, propaganda ulizotumwa kuzifanya kwa wana-Ngorongoro hazitakuacha salama

Maulid Kitenge, propaganda ulizotumwa kuzifanya kwa wana-Ngorongoro hazitakuacha salama

Modes futeni tena ili ile adhima yenu ya kuwa na nchi isiyo heshimu freedom of speech
itimie, licha ya Mabalozi kuitambua kama ngome ya freedom of speech Tz baada ya twitter.
Ni kweli waarabu washafanya yao kwa kikanga?
Zaidin ya comment 300, 95 zinamtuhum Kikanga
kupokea ngawira/ njuruku kutoka waarabu na siri kali.

View attachment 2110586

View attachment 2110587

View attachment 2110588

View attachment 2110589
Hizi tweet zimejaa neno Wamasai, Wamasai. Hii ni harufu ya kueneza na kurutubisha Ukabila.
Na tukumbuke, Wamasai wameenea Nchi nzima hivi sasa, na Tanzania hakuna Ubaguzi wa Kikabila.
 
Ngorongoro Conservation Area siyo ya Wamasai pekee, ni ya Watanzania wote, na inahitaji Mjadala wa kina.
Itakuwa aibu na fedheha kubwa kwa Taifa letu kama hii World Heritage itapotea kutokana na kuogopa kelele za Wanaharakati wameigeuza Ngorongoro kuwa mali ya Wamasai.
Hii ni hatari.
Serengeti nayo iwe wa Wakurya?
Ruaha iwe ya Wakaguru?
Mazingira ya Ngorongoro ya Binadamu kuishi na Wanyamapori yanakubalika, lakini ni lazima kuwe na Ulinganifu wa Kiekolojia, 'Ecological balance'.
Majumba yanajengwa ndani ya Ngorongoro. Hii siyo sawa.
Ngorongoro ikipotea, sisi sote tutaingia katika fedheha isiyo na kipimo.
Kumtukana Maulidi Kitenge kwa kuandika kilichopo, hakuisaidii Tanzania wala Wamasai wanaoishi Ngorongoro.
Malisho yakiharibiwa, Wanaharakati hawataonekana kuwafadhili Wamasai.
Watakimbilia kusikojulikana.
Tuiokoe Ngorongoro.
Utafiti ulifanywa ndio maana wakaruhusiwa kukaa toka 1959.
Wanachodai ni utafiti upi umefanyika kuona kuna athari hizo?
Wanadai hizi habari zimeshikiwa bango na wawekezaji kama uficho
wa kuwatoa ili wapate kuingia.
 
Modes futeni tena ili ile adhima yenu ya kuwa na nchi isiyo heshimu freedom of speech
itimie, licha ya Mabalozi kuitambua kama ngome ya freedom of speech Tz baada ya twitter.
Ni kweli waarabu washafanya yao kwa kikanga?
Zaidin ya comment 300, 95 zinamtuhum Kikanga
kupokea ngawira/ njuruku kutoka waarabu na siri kali.

View attachment 2110586

View attachment 2110587

View attachment 2110588

View attachment 2110589

Acha utoto watu kuwa wengi kupinga jambo hakuondoinukweli kuwa kuna shida ngorongoro na lazima hatua za haraka zichukuliwe kunusuru hii hifadhi! Si kila mtu tweeter ana akili timamu wa kuchambua kila hambo! Shida yenu mnafikiri watu walio tweeter wana akili sana kuliko wengine hivyo kila wanachosema ni kweli!

Tweeter kimekuwa kichaka cha watu wenye stress zao kwa hiyo kila jambo wanalipinga!
 
Usiandike kishabiki hali ya Ngorongoro inasikitisha,inakatisha tamaa & ina huzunisha.
Ni kweli Waasai wapo ngorongoro miaka mingi wakishi na wanyama pori na mifugo yao.Wakati huo Mamlaka inaanzishwa idadi ya watu ilikuwa 8,271 na idadi ya mifugo ilikuwa 30,000.Nyumba za wamaasai zilikuwa aina ya combi

View attachment 2109828

Leo idadi ya Maasai ni 120,000 huku idadi ya mifugo yao ikifikia zaidi ya 1,000,000 na makaazi yao yakiondoka katika uasilia na kwenda kwenye usasa.Leo hii mabati msouth yamejaa Ngorongoro.Mmaasai anajenga nyumba za kisasa hadi maghorofa yamejengwa ndani ya hifadhi mgeni akitembelea Ngorongoro anakutana na Kondoo,Mbuzi na Ng'ombe kwa wingi kuliko Simba au Nyati.

Lazima Tanzania ichukue hatua kali na madhubuti kuokoa Ngorongoro.Kumezuka NGOs nyingi tena nyingine zikiasisiwa Kenya zipo pale kwaali ya kutetea ujinga na kuona Ngorongoro inakufa.Hii vita asili yake kubwa ni Kenya ambayo inaumizwa sana na uwepo wa Ngorongoro,Serengeti na Kilimanjaro.Kenya kupitia idara yake ya ujasusi inafahamu wazi ushindani wa utalii ni vivutio na wakiangalia hizo Mbuga tatu wanaona bora waiumize walau moja ambayo ni Ngorongoro.

Hizi NGOs nyingi zinawadanganya wamaasai Ngorongoro ni mali yao,serekali haina chao sasa huu ujinga ungemalizwa na vingozi wenye maamuzi mazito ikiwemo kuirejesha Ngorongoro TANAPA na kuifanya HIFADHI kama zilivyo Manyara,Serengeti,Kilimajaro au Mikumi.Wamaasai wahamishwe wote Tanzania bado ina mapori mengi.
Umenena vyema mkuu.Kwa kuongezea kutokana na kupanda kwa bei ya nyama ya kondoo kwenye soko la dunia,kumepelekea idadi ya kondoo kuwa kubwa zaidi ya ng'ombe na mbuzi.
Kondoo ana sifa ya kula nyasi na kutafuna mpaka mizizi na hivyo kuharibu ecology ya eneo husika.
Wakati huo hifadhi za nchi jirani huwezi kuta kondoo akichungwa.
Ndugu zangu tuwe makini tusiwe marisho ya mifugo ya nchi jirani na kupelekea kuua mbuga zetu na za kwao zikinawili.
 
Acha utoto watu kuwa wengi kupinga jambo hakuondoinukweli kuwa kuna shida ngorongoro na lazima hatua za haraka zichukuliwe kunusuru hii hifadhi! Si kila mtu tweeter ana akili timamu wa kuchambua kila hambo! Shida yenu mnafikiri watu walio tweeter wana akili sana kuliko wengine hivyo kila wanachosema ni kweli!

Tweeter kimekuwa kichaka cha watu wenye stress zao kwa hiyo kila jambo wanalipinga!
Wamepinga kwa facts sio kama wewe.
Wanahoji mwaka 1959 kipindi wanakaa huko utafiti ulionyesha hakuna shida.
Kwanini sasa hawapeleki utafiti unaonyesha wao wanavyo tishia kutoweka kwa Ngorongoro?
Si Ngorongoro yenyewe wala tafiti zingine, zaidi ya wanasiasa na wawekezaji uchwara wa kiarabu.
 
Utafiti ulifanywa ndio maana wakaruhusiwa kukaa toka 1959.
Wanachodai ni utafiti upi umefanyika kuona kuna athari hizo?
Wanadai hizi habari zimeshikiwa bango na wawekezaji kama uficho
wa kuwatoa ili wapate kuingia.
Kama wanataka kuwatoa wamasai ili waweke wawekezaji wa mahoteli si wafanye hivyo tu badala ya kuendelea kuwanyanyasa kisaikolojia?
 
Kwani kafanya nini ? Nijuze tafadhali kwa kifupi tuu
Anataka Wamasai na mifugo yao waondolewe Ngorongoro, ilihali wamekuwa wakiishi huko for decades.

Kuna jamaa Mmasai kule twitter anasema Kitenge na jamaa yake mmoja walitengewa Mil.100 ili kutangaza hayo
 
Kwa hiyo wamemaliza "kutupanga" machinga wameamua kuhamia kwa wamasai ? Ngoja tuone🐒
 
Kuliko kujengwa mahotel ambayo mtazania hatoweza kuafford kulala hapo ni bora ndugu zetu wabaki kama ni kweli kuna muwekezaji anataka kuwekeza
 
Usiandike kishabiki hali ya Ngorongoro inasikitisha,inakatisha tamaa & ina huzunisha.
Ni kweli Waasai wapo ngorongoro miaka mingi wakishi na wanyama pori na mifugo yao.Wakati huo Mamlaka inaanzishwa idadi ya watu ilikuwa 8,271 na idadi ya mifugo ilikuwa 30,000.Nyumba za wamaasai zilikuwa aina ya combi

View attachment 2109828

Leo idadi ya Maasai ni 120,000 huku idadi ya mifugo yao ikifikia zaidi ya 1,000,000 na makaazi yao yakiondoka katika uasilia na kwenda kwenye usasa.Leo hii mabati msouth yamejaa Ngorongoro.Mmaasai anajenga nyumba za kisasa hadi maghorofa yamejengwa ndani ya hifadhi mgeni akitembelea Ngorongoro anakutana na Kondoo,Mbuzi na Ng'ombe kwa wingi kuliko Simba au Nyati.

Lazima Tanzania ichukue hatua kali na madhubuti kuokoa Ngorongoro.Kumezuka NGOs nyingi tena nyingine zikiasisiwa Kenya zipo pale kwaali ya kutetea ujinga na kuona Ngorongoro inakufa.Hii vita asili yake kubwa ni Kenya ambayo inaumizwa sana na uwepo wa Ngorongoro,Serengeti na Kilimanjaro.Kenya kupitia idara yake ya ujasusi inafahamu wazi ushindani wa utalii ni vivutio na wakiangalia hizo Mbuga tatu wanaona bora waiumize walau moja ambayo ni Ngorongoro.

Hizi NGOs nyingi zinawadanganya wamaasai Ngorongoro ni mali yao,serekali haina chao sasa huu ujinga ungemalizwa na vingozi wenye maamuzi mazito ikiwemo kuirejesha Ngorongoro TANAPA na kuifanya HIFADHI kama zilivyo Manyara,Serengeti,Kilimajaro au Mikumi.Wamaasai wahamishwe wote Tanzania bado ina mapori mengi.
Kweli kabisa unayosema ni kweli tupu. Mimi nilisafiri jumanne kutoka Musoma kuja Arusha nilipita barabara ya mbugani Serengeti na Ngorongoro ukweli ni kwamba kuna nyumba za bati, kuna shule na idadi ya mifugo ni kubwa mno alafu nimeona wanawake wa kimasai wapo barabarani wanauza asali na shanga kwa hiyo machinga wameshaanza Ngorongoro. Sitashangaa kuona maghorofa na flyover zikijengwa ngorongoro crater. Kuna kipindi nilikuta kuna mahubiri yanafanyika tena speakers zimefungwa alafu ni usiku. Hata sielewi tuna fanya nini kwa zawadi hii adimu tuliyopewa na Mungu. Idadi ya watu imeongezeka sana Ngorongoro wakati huu ni muafaka kuwaondoa ndugu zetu wanaoishi na kuwapatia makazi mengine nje ya Ngorongoro. Pia serikali ihamishe hoteli zote kutoka Ngorongoro zijengwe nje ya crater watalii waingie crater na kurudi kulala nje ya crater. Mungu ibariki ngorongoro
 
wakati huu ni muafaka kuwaondoa ndugu zetu wanaoishi na kuwapatia makazi mengine nje ya Ngorongoro
Tatizo hua linaanzia kwenye utekelezaji wa maagizo ya "kuwaondoa", wasije wakawahamishia kwenye makazi yao ya milele
 
Utafiti ulifanywa ndio maana wakaruhusiwa kukaa toka 1959.
Wanachodai ni utafiti upi umefanyika kuona kuna athari hizo?
Wanadai hizi habari zimeshikiwa bango na wawekezaji kama uficho
wa kuwatoa ili wapate kuingia.
Si kweli!
 
Wewe jamaa ndo mkuu wa wilaya au ndo Mkurugenzi hapo Ngorongoro?? Mbona Kama unaogopa kutumbuliwa....maulid apo anahusika vipi wakati yy alikua akichambua magazeti?
Hee kumbe Banda bovu limemuangukia kwa sababu ya kusoma tu gazeti..sasa huyu mtoa hoja hata hili haelewi.
 
Back
Top Bottom